Biashara gani Pasua kichwa....!!!!?

LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,401
1,312
Wakuu ili tuweze kuwa makini na aina za biashara pale tunapotaka kuwekeza na kufanya biashara ninaomba angalau tujuzane biashara gani ni pasua kichwa (biashara kichaa) yaani katika makundi haya: hutumia muda mwingi, usumbufu mkubwa, risk kubwa na pia faida hupatikana kidogo .... hii ni katika level ya ujasiriamali .... assuming that unaifanya kwa ufanisi wote na discipline ya biashara

hapa tunaweza kupata na ufumbuzi wa mojawapo ya biashara pasua kichwa

• yaweza kuwa biashara ya kuleta magari toka nje yasiyo na brand za kijapani .... kama vile volkswagon, hammer, Peugeot, Renault, BMW, range rover n.k ?
• Biashara ya kuleta mkaa kama agent wa wachoma mikaa na kuwauzia retailers ?
• biashara ya maji ya kunywa retail ?
• biashara ya kuuza vocha za simu ?
• biashara ya daladala ?
• biashara ya bodaboda ?
• biashara ya taxi ?
• gutter politics (siasa uchwara) ...?
• biashara ya udalali kishoka

na nyinginezo nyingi twaweza endelea kuzitaja na kuelezea

hakuna anayetaka kupasua kichwa kwa kufanya bishara kichaa ..... i stand to be corrected

kuna watu wanasafirisha samaki toka mwanza hadi dar..... duh .... hivi gari likiharibika ...presha hii

Biashara yoyote ya chombo cha moto kinachotembea barabarani,ie.daladala,tax etc

biashara ya daladala na taxi mbona poa tu?hapo issue ni dereva!ukimpata dereva mzuri unapiga hela!biashara kichaa ni yoyote ile mali kuoza!mfano,nyanya,viazi,kabichi nk.

au biashara ya kusafirisha nyanya,
we acha tu
nilitoaga nyanya kutoka lushoto kuja dar
kufika kariakoo kuna nyanya za arusha zimewasili lundo
sina hamu

mkuu pole sana

na inawezenkana ulubeba fuso nzima .... duh

biashara ya usafiri ni kichaa in TZ
-TRA
-Trafiki
-Sumatra
-Majembe-yono
-Mateja,wapiga debe ,dereva unproffesional

hapo ndio utaona ukichaa wa biashara hii ya usafiri in TanzaGIza

au biashara ya kusafirisha nyanya,

we acha tu

nilitoaga nyanya kutoka lushoto kuja dar

kufika kariakoo kuna nyanya za arusha zimewasili lundo

sina hamu

halafu usiombe hela umekopa pride au finca....

mi naona udalali,taxi na bodaboda kwani una weka ahadi na mtu usiyekuwa naye na ahadi..

Nilikutana na raia mmoja wa Chad, Hong Kong, akaniambia kama naweza tufanye biashara ya Utomvu wa mapapai! Anaitaji Debe mbili za Utomvu wa Mapapai kama naweza, Nikijiza Debe mbili anatatoa kila Debe $10,000 nilijiuliza sana hiyo biashara kwangu mimi nikaona pasua kichwa

Biashara zote pasua kichwa, usitegemee mteremko kwenye biashara, jipange vizuri tu, zote zinawezekana.

Nilikutana na raia mmoja wa Chad, Hong Kong, akaniambia kama naweza tufanye biashara ya Utomvu wa mapapai! Anaitaji Debe mbili za Utomvu wa Mapapai kama naweza, Nikijiza Debe mbili anatatoa kila Debe $10,000 nilijiuliza sana hiyo biashara kwangu mimi nikaona pasua kichwa

hahaha. Thats new aisee. Anaifanyia nini?

biashara ya utomvu wa papai ipo ,ila kwa bei ya dola 10000 kwa debe sidhani kuwa ni sahihi
utomvu wa papi una kitu kinaitwa papain.
hutumika ktk
kulainisha nyama
kudunga ng'ombe wa nyama kabla ya kuchinja ili nyama iwe laini
Uganda wanafanya export ya utomvu wa papai,na tanzania walikuwa wanafanya biashara ya utomvu miaka ya 60 hadi 1970s

Nilikutana na raia mmoja wa Chad, Hong Kong, akaniambia kama naweza tufanye biashara ya Utomvu wa mapapai! Anaitaji Debe mbili za Utomvu wa Mapapai kama naweza, Nikijiza Debe mbili anatatoa kila Debe $10,000 nilijiuliza sana hiyo biashara kwangu mimi nikaona pasua kichwa

Mkuu unasema kweli au unatani?
maana mimi nikotayari kuianzisha hiya project kama utaniunganisha nahuyo mchad

Mkuu unasema kweli au unatani?
maana mimi nikotayari kuianzisha hiya project kama utaniunganisha nahuyo mchad

mkuu .... hiyo project itakula kwako ... pasua kichwa hii

biashara ya daladala na taxi mbona poa tu?hapo issue ni dereva!ukimpata dereva mzuri unapiga hela!biashara kichaa ni yoyote ile mali kuoza!mfano,nyanya,viazi,kabichi nk.

Nakubaliana na wewe,Biashara nyingi za Perishable goods,zenye kuweza kualibika,pasua kichwa kinoma,hata kuleta kuku kutoka Mikoani,lazima ulie tu,Mara wamekufa njiani,mara wameshuka uzito,mara ndumba,utapata wazimu tu!!

• Thanks
Reactions: LAT
biashara ya utomvu wa papai ipo ,ila kwa bei ya dola 10000 kwa debe sidhani kuwa ni sahihi

utomvu wa papi una kitu kinaitwa papain.

hutumika ktk

kulainisha nyama

kudunga ng'ombe wa nyama kabla ya kuchinja ili nyama iwe laini

Uganda wanafanya export ya utomvu wa papai,na tanzania walikuwa wanafanya biashara ya utomvu miaka ya 60 hadi 1970s
Mkuu, unakumbuka bei kwenye miaka ya 1970 ilikuwa sh ngapi?

Similar Discussions

Back
Top Bottom