Biashara gani Mwanachuo anaweza kufanya akiwa Chuoni?

Biashara gani Mwanachuo anaweza kufanya akiwa Chuoni?

Biashara nyingine ni ku print,

Hii inalipa maana stationery nyingi hufungwa saa moja jioni hivyo wewe ukiwa unatoa huduma muda wowote basi utazoeleka haraka maana muda mwengine mchana hakuna umeme hadi usiku na watu kibao wanataka ku print assignment zao.

Printer ya bei poa ni hp 315 inktank, niliona inauzwa duka la "discount kubwa" pale kariakoo kwa 290,000/= ukiinunua utaweza kuprint hadi karatasi elf 8, na wino ukiisha kuna vichupa wanauza elf 4 unajaza.

Rim ina karatasi 500 na inauzwa tuseme elfu 10 zile nzuri, ukifanikiwa ku print hio rim nzima kwa bei ya shilingi 100 kwa karatasi moja basi una elf 50 ukitoa gharama ya rim tayari faida elf 40, ikifika jioni stationery zikiwa zimefungwa unachaji hata 200 kwa page moja.

Pia utaweza kuprint hata rangi, hususani kwenye cover page za assignment ile nembo ya chuo ina rangi, wengine watapenda kutoa kopi ya rangi watie nakshi .

Pia hii printer unaweza ku scan documents kama vyeti, unaweza kuprint picha zile za passpprt size na hata zile za kuweka kwenye albamu, So ukijiongeza waweza kuitumia kwa mambo kibao.

Hii uzuri wake ni kwamba hata mwanafunzi mwenye hii printer ananufaika kujiprintia kazi lakini pia inakuwa kitega uchumi.
Hilo Duka kariakoo ni lipi??
 
I remember nilikuaa na pc na printer chumbani kwangu; nilikuwa napata hivo hivo tuu [emoji1] ingawa inabidi uwe na msimamo ukitenga muda wa kusoma
 
Hizo bei unamwekea mwanachuo gani mjomba? Mimi hapa naprint kwa gharama ya 100 kwa kuwa sipendi uswahili kwenye stationary. Na mara nyingi group assignment naprint mimi hivyo cover page na mengine yapo kwenye kompyuta za stationary ile. Sharti langu ni moja, huwa nataka niachiwe nifanye kazi mwenyewe kisha nilipe.
Tofauti na hapo, kuna watu wanaprint kwa 70 mpaka 50 maana ushindani ni mkubwa. Hiyo 200 hupati mtu kabisa. Kwanza tangu nianze chuo ni mara moja tu umeme ulishawahi nizuia kuprint.

Nilikuwa naprint cover page kwa sh 100 [emoji16] nyingine mara niwafanyie 100 mara 70 [emoji23][emoji23] basi sikuwahi kueleweka ila kipindi cha assignments nilikuwa nakamata sana wale funika bovuu
 
Nimekuelewa mnooh, [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Hiyo biashara kaiongelea kinadharia mno, ameifanya ionekane ina faida wakati sio kweli. Rim ina karatasi 400 ila hauwezi ukaziprint zote zikatoka vizuri, photocopy mashine zinafanya kazi kutegemeana na siku hiyo zimeamkaje,fundi anatakiwa awe karibu muda wote.

Mashine za lamination/printer/photocopy zina ugonjwa wa kusokota karatasi ikiwa hizo karatasi zina ubaridi, una hitajika umakini mno wa hizo mashine.Ugonjwa mkubwa wa hizo mashine ni rollers.
Sio biashara ya faida kihivyo.
 
Mie nilikuwa na support maan kaweka hoja vizuri, ila mie mwenyewe hata huo mtaji sina uwiiiiiiih
 
sambaza ubuyu wa Babu issa, hakika utapiga pesa.......weka kibanda cha kuuza ubuyu,andika ubuyu wa Babu issa,uza kuanzia robo na kuendelea....hakika mademu wote utawashika,pia kwa wanaume pesa zao utazipata kupitia mademu..... hahaaaha nakutania ndugu si unajua napenda utani.
Hahaha hii nilishawahi jaribu sema niliishia kuwakopesha mademu.
 
Hahaha hii nilishawahi jaribu sema niliishia kuwakopesha mademu.
Mkuu siku hizi sikuoni au yawezekana tunapendelea majukwaa tofauti.
On topic, ubuyu unauzwa na watu wengi sana hapa chuoni. Tena wenyewe ni biashara ya kufosi ambayo unawauzia friends tu. Pia unaishia kula na kuonjesha.
 
Wakuu habari zenu,

Natumaini ni wazima wa afya, poleni na majukumu ya kulijenga taifa. Lengo la bandiko hili ni kusaidia vijana walioko chuo na wanaotarajia kwenda chuo. Hoja ni kitu gani au biashara gani ambayo anaweza kufanya akiwa chuoni.

Asante, karibuni kwa maoni yenu.
Steshenare
 
Biashara nyingine

Nununua rim yenye karatasi 500 kwa elf 8 na boksi la peni 50 nadhani wanauza elf 5.

Unapoenda chuo kwenye begi lako weka karatasi za rim kama 100 hivi, Stepla ya kubania karatasi na peni ulizojumua.

Karatasi moja uza kwa hamsini, na mtu akihitaji zaidi mbanie hizo karatasi na stepla, Wateja wengi wapo kwenye vimbweta na madarasani.

Peni uza kwa 200.

Matokeo yake faida ya rim utapata elf 17 na kwenye peni faida itakuwa elf 5.

Changamoto ya hii biashara ni chenji, sana sana hizi 50, Hapa naona labda unaweza kutatua kwa kuweka masharti yako kuwa mtu inabidi anunue karatasi 2, 4, 6, 8, n.k
 
Mkuu harakati tu ndiyo zinanifanya kidogo nionekane mara chache
 
Biashara nyingine ni ku print,

Hii inalipa maana stationery nyingi hufungwa saa moja jioni hivyo wewe ukiwa unatoa huduma muda wowote basi utazoeleka haraka maana muda mwengine mchana hakuna umeme hadi usiku na watu kibao wanataka ku print assignment zao.

Printer ya bei poa ni hp 315 inktank, niliona inauzwa duka la "discount kubwa" pale kariakoo kwa 290,000/= ukiinunua utaweza kuprint hadi karatasi elf 8, na wino ukiisha kuna vichupa wanauza elf 4 unajaza.

Rim ina karatasi 500 na inauzwa tuseme elfu 10 zile nzuri, ukifanikiwa ku print hio rim nzima kwa bei ya shilingi 100 kwa karatasi moja basi una elf 50 ukitoa gharama ya rim tayari faida elf 40, ikifika jioni stationery zikiwa zimefungwa unachaji hata 200 kwa page moja.

Pia utaweza kuprint hata rangi, hususani kwenye cover page za assignment ile nembo ya chuo ina rangi, wengine watapenda kutoa kopi ya rangi watie nakshi .

Pia hii printer unaweza ku scan documents kama vyeti, unaweza kuprint picha zile za passpprt size na hata zile za kuweka kwenye albamu, So ukijiongeza waweza kuitumia kwa mambo kibao.

Hii uzuri wake ni kwamba hata mwanafunzi mwenye hii printer ananufaika kujiprintia kazi lakini pia inakuwa kitega uchumi.
💪😍😍🙏🙏
 
Kama ni wa Kiume Kama utakuwa na interest na hii biashara ya kupaka Rangi kucha wadada wa chuo basi hautojuta kuifanya ukiwa mazingira ya chuoni mana utakuwa unafanya mobile service yaani unawafata katika hostel zao humo humo unatoa huduma,kwa hela hizi za kula kwako na za kufanyia mambo mengine zitakuwa hazikusumbui

Kitu cha kwanza kama hauna ujuzi wowote wa kupaka rangi kucha unaweza ukamtafuta mtu mpaka rangi eneo ulilopo ukamwomba akufundishe,wengine wanaweza kukufundisha bure au ukalipia mafunzo inategemea na mtu utakae kutana nae.

Kama utakuwa na kichwa ya haraka kushika mambo basi ndani ya mwezi mmoja/miwili unaweza ukawa ushajua kila kitu about basics za upakaji rangi kucha na ukajua mahitaji yapi yanatakiwa katika hii biashara ya kuanza nayo.Na ukawa tayari kwa kuanza rasmi shughuli zako hapo chuoni.Pia
YouTube toturial zipo nyingi ya kitu kwa beginners.

NOTE: Biashara hii ukiifanya kwenye misingi sahihi kama biashara zingine pesa utaiona,ila kama utaamua ufanye hii biashara upate totozi uwale kweli utawapata tu. Mana ina changamoto nyingi ni wewe tu kusimama kwenye misingi yako ya biashara..

Changamoto nyingine ipo kwenye ku manage muda wa masomo chuoni na kufanya hii inshu mana inataka moyo wa kuweza ku manage muda wa masomo na hii harakati,

Unaweza mwenyewe ukatenga muda wako wa kupiga kazi kwamba kila ijumaa, jumamosi na jumapili unaenda kwenye hostels za kike unapiga kazi zako au katikati ya week pale kama hakuna kipindi class unaenda kupiga hii harakati hapo itategemea na time table yako 30000 au zaidi kwa week hukosi kupata.

NOTE: Kama ndo unaenda kuanza first year yasome kwanza mazingira ya hapo chuoni kwenu yapoje kisha ujitathimini mwenyewe mana unaweza ukawekeza nguvu sana kuitafuta pesa ukanogewa na pesa afu nguvu ya darasani ukaipoteza.

Sijaandika kwa mpangilio mzuri ila nazani utakuwa umepata at least kitu hapo,Mana na uzoefu na hii Biashara hapa chuoni kwetu.

"Biashara yoyote ya Urembo inayomuhusu Mwanamke inalipa"
🙏🙏💪💪
 
Wakuu habari zenu,

Natumaini ni wazima wa afya, poleni na majukumu ya kulijenga taifa. Lengo la bandiko hili ni kusaidia vijana walioko chuo na wanaotarajia kwenda chuo. Hoja ni kitu gani au biashara gani ambayo anaweza kufanya akiwa chuoni.

Asante, karibuni kwa maoni yenu.
Kama ni mwanamke iko ya kufanya kuna wenzie wengi tuu wanaifanya saa hivi mwambie ajiongeze tuu .
Naomba niishie hapo
 
I remember nilikuaa na pc na printer chumbani kwangu; nilikuwa napata hivo hivo tuu [emoji1] ingawa inabidi uwe na msimamo ukitenga muda wa kusoma
Ulikuwa unapata kiasi gani cha pesa?
 
Biashara nyingine

Nununua rim yenye karatasi 500 kwa elf 8 na boksi la peni 50 nadhani wanauza elf 5.

Unapoenda chuo kwenye begi lako weka karatasi za rim kama 100 hivi, Stepla ya kubania karatasi na peni ulizojumua.

Karatasi moja uza kwa hamsini, na mtu akihitaji zaidi mbanie hizo karatasi na stepla, Wateja wengi wapo kwenye vimbweta na madarasani.

Peni uza kwa 200.

Matokeo yake faida ya rim utapata elf 17 na kwenye peni faida itakuwa elf 5.

Changamoto ya hii biashara ni chenji, sana sana hizi 50, Hapa naona labda unaweza kutatua kwa kuweka masharti yako kuwa mtu inabidi anunue karatasi 2, 4, 6, 8, n.k
💪💪🙏🙏
I
 
ulikuwaunapata kiasi gani cha pesa?

Inategemea kama kipindi cha Assignment; nilikuwa per day nakusanya hata income ya 30,000 na profit kama ya 20,000 na huenda na zaidi maana nakuwa nachinja papers tuu na wino ambao hata 10000 haufiki......

Ila kwa siku nyingine, nilikuwa mpaka 15000 income, profit lies 10,000....japo pesa nyingi ni kwenye typing, scanning na kama itakuwa copier....ila printing kidogo sana [emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom