Biashara nyingine ni ku print,
Hii inalipa maana stationery nyingi hufungwa saa moja jioni hivyo wewe ukiwa unatoa huduma muda wowote basi utazoeleka haraka maana muda mwengine mchana hakuna umeme hadi usiku na watu kibao wanataka ku print assignment zao.
Printer ya bei poa ni hp 315 inktank, niliona inauzwa duka la "discount kubwa" pale kariakoo kwa 290,000/= ukiinunua utaweza kuprint hadi karatasi elf 8, na wino ukiisha kuna vichupa wanauza elf 4 unajaza.
Rim ina karatasi 500 na inauzwa tuseme elfu 10 zile nzuri, ukifanikiwa ku print hio rim nzima kwa bei ya shilingi 100 kwa karatasi moja basi una elf 50 ukitoa gharama ya rim tayari faida elf 40, ikifika jioni stationery zikiwa zimefungwa unachaji hata 200 kwa page moja.
Pia utaweza kuprint hata rangi, hususani kwenye cover page za assignment ile nembo ya chuo ina rangi, wengine watapenda kutoa kopi ya rangi watie nakshi .
Pia hii printer unaweza ku scan documents kama vyeti, unaweza kuprint picha zile za passpprt size na hata zile za kuweka kwenye albamu, So ukijiongeza waweza kuitumia kwa mambo kibao.
Hii uzuri wake ni kwamba hata mwanafunzi mwenye hii printer ananufaika kujiprintia kazi lakini pia inakuwa kitega uchumi.