Bi Sirleaf aridhia duru ya pili Liberia

Bi Sirleaf aridhia duru ya pili Liberia

Mwanakili90

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Posts
1,568
Reaction score
246
17 Oktoba 2011 12:49

Rais wa Liberia Ellen Johnson-Sirleaf amesema
ameridhia kukabiliana na duru ya pili ya
uchaguzi dhidi ya aliyekuwa mwanadiplomasia
wa umoja wa mataifa Winston Tubman. Huku takriban kura zote zikiwa
zimeshahesabiwa, Bi Sirleaf alipata kura nyingi
zaidi lakini alishindwa kuvuka asilimia 50
inayotakiwa kupata ushindi. Bw Tubman alisema atagombea tena katika duru
hiyo baada ya chama chake kudai kuwepo
udanganyifu na kudai kujitoa. Huu ni uchaguzi wa pili Liberia tangu kumalizika
kwa miaka 14 ya vita vya wenyewe kwa
wenyewe mwaka 2003. Bi Sirleaf, ambaye alipewa tuzo ya amani ya
Nobel wiki iliyopita, alishinda uchaguzi wa
mwaka 2005 na kuwa mwanamke wa kwanza
Mwafrika kuchaguliwa kuwa rais. Alimshinda aliyekuwa mcheza soka George
Weah, ambaye kwa sasa ni mgombea mwenza
wa Bw Tubman. Bi Sirleaf alisema yuko tayari kwa ushindani
lakini pia alikuwa ana uhakika wa kushinda. Ikiwa aslimia 96 ya kura zote zikiwa
zimehesabiwa, yeye ana asilimia 44 dhidi ya 32
za Bw Tubman, tume ya uchaguzi imetangaza.
Waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 74. "Duru ya pili ni karibu sana," alisema James
Fromayah kutoka tume ya taifa ya uchaguzi
(NEC). Imepangwa kufanyika Novemba 8.

Source:BBC
 
safi hakuna uroho wa madaraka hapo!duu inanikumbusha kenya-mwai kibaki wakati raila ana wabunge 109 kibaki 33 akakatisha matangazo ya matokeo akaenda viwanja vya ikulu na kuapishwa haraka haraka kuwa kashinda
 
Huyo mpinzani wake kama ana akili atengeneze 'coalition' na mshindi wa tatu ili apate kura zake ili amshinde huyo mama. Huyo mama fisadi sana halafu nasikia ni 'freemanson'
 
Huyo mpinzani wake kama ana akili atengeneze 'coalition' na mshindi wa tatu ili apate kura zake ili amshinde huyo mama. Huyo mama fisadi sana halafu nasikia ni 'freemanson'

Ckutambua ilo kabla.
 
Huyo mpinzani wake kama ana akili atengeneze 'coalition' na mshindi wa tatu ili apate kura zake ili amshinde huyo mama. Huyo mama fisadi sana halafu nasikia ni 'freemanson'

we si mzima,tena familia yako ikupeleke milembe mapema kabla hujazidiwa
 
we si mzima,tena familia yako ikupeleke milembe mapema kabla hujazidiwa

Kwanini si mzima? mchango wake kwa thread hii una matatizo kwani hadi umwelezee kama c mzima? mi sijaona tatizo
 
Back
Top Bottom