Bi. Khadija Mkomanile, mwanamke jasiri wa Vita vya Maji Maji

Nilikuwa mfuatiliaji mzuri sana wa historia na matukio ya zamani ktk blog yako. Siku hizi siioni hewani kulikoni?
 
King Kong...
Unjitesa bure kwa fikra isiyo na ukweli.

Hivi karibuni hapa jamvini nimemzungumza Mzee Aikaeli Mbowe.

Lakini siwezi nikamueleza kwa mapana kwa kuwa sikumfahamu vya kutosha.


Kwaheri kaka yangu, mzungumzaji wangu Jimmy Mdoe
 
Majina ya Kiislam au ya Kiarabu? Kumbuka Waziri wa mambo ya Nje wa Iraq wakati wa Saddam Hussein alikuwa mkristo mwenye jina la kiarabu "Tariq Aziz"
Lengo la Mleta mada ni kuwafanya watu wajue kuwa walioshiriki vita vya majimaji ni Waislam

Hata kama wapo Wakristo kamwe hawataji kwasababu ana laana ya Udini
 
Nafuu umemfahamu huyu Mlaaniwa Mohamed Said
 
Wee we we!!! Ukionesha kuwa aliyeandika kitabu anaitwa Francis Daudi utapingwa sana na Mohamed Said

Yeye anataka kuaminisha watu kuwa aliyeandika ni Muislam, hujui uzushi wa huyu Mzee?
 
Eti Wanakwepa majina ya kiislam, kwani wasipokwepa itawasaidia nini na wakikwepa inawasaidia nini?

We Mzee una uelewa hafifu sana, Ilmu ya juzuu inakuchanganya akili
 
King Kong III,
Historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika imejaa visa na mikasa mingi ya Waislam na sababu ni kuwa wao ndiyo walikuwa wengi kwenye harakati.

Hupendi kusoma historia hii?
Uongo na Uzushi utakunyima Firdaus Mzee
 
Msanii,
Historia ya.Maji Maji ina mengi.

Soma barua ya Nduna Abdulrauf Songea Mbano kwa Sheikh Mataka Hamim Massaninga unaweza ukaelewa.
Mzee wetu
Nimekusoma nimekuelewa. Kiukweli kuna mengi yamefukiwa fukiwa kwenye historia ya nchi yetu.

Badala ya kuhijack history just iwekwe wazi maana mimi siamini katika religion superiority bali kwenye class struggle. I have mind dominations ya hizi dini kubwa mbili yaani Islam na Ukristo kujitwalia mamlaka hata ya watu kufikiri kwa uhuru.

Ubaguzi wa kweli unaanzia kwenye dini ndo maana mnachora mistari kuwa hili jina la Islam hili la Kikristo. Shame ni kwamba hakuna anayejihoji wala kuhoji kuwa kama ni sahihi kuwaza in the core of dini establishment kwa nini alizaliwa Mmakonde na Mmasai....

Ukristo na Uislam ndiyo uliochangia pakubwa biashara ya Utumwa na baadaye unafiki wa kuiabolish ili ifanyikie kizani kama sasa. Angalia madhila ya bintizo wanayoyapata Uarabuni wakishauzwa na so called mawakala wa kazi za Arabuni ambao inawezekana mnakunywa nao kahawa kilingeni, angalia namna waafrika wanavyokimbilia utumwani Ulaya hata wengine kufia baharini......

Turejee kwenye passage uliyotuwekea. Pls tuwekee usuli kuhusu huyu shujaa wa kike aliyeshiriki vita jadidi ya Majimaji ambayo unaiita Jihadi Kuu ya Majimaji
 
Mzee Mohamed wewe mashujaa wako ni waislamu tu,sijawahi kuona ukiwasifia wakristo waliopigania uhuru.
Mzee anayeujua ukweli na kulazimisha utumike Kidini ili kueneza haiba ya kibaguzi.

Hakuna mtu aliyewahi kusema Wakatoliki au Wakristo ndiyo waliopambana tupate uhuru. Bali Watanganyika wenye malengo yanayofanana kwa minajili ya uhuru wa nchi yetu
 
Msanii,
Walioandika historia ya uhuru waliandika historia siyo.

Nimeisahihisha historia hiyo na kuwarejesha wale wote waliosahauliwa.

Ingia.Google utakuta yaliyoandikwa kuhusu Bi. Khadija bint Mkomanile.
 
Mzee hizo ni chuki tu jamaa kaamua kutoa info kuhusu waislam wewe anzisha thread yako kuhsu Christian tutajifunza tatizo mnapenda mabeef yakijinga tu.
 
Kwahiyo hivyo Vita vya jihad vilitumia ushirikina? Hayo maji Ni ushirikina.
Sidhani Kama ni sahihi kusema Vita vya maji maji Ni Jihad.
 
Kusema ukweli, Mzee Mohamed Said umekuwa Mwalimu nzuri sana wa kutupatia elimu kubwa juu ya Viongozi waliokuwa vinara katika kupigania Uhuru wa Tanganyika na hatimaye Tanzania baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar!

Mwenyezi Mungu akujalie maisha marefu uweze kutufunza mengi!
 
Obe...
Amin.
 
Hakuna kitu kinachoitwa jina la kiislam au jina la kikristo. Kuna jina la kiarabu au 'kizungu'. Uislam umetumika kueneza tamaduni za kiarabu kama ambavyo ukristo umetumika kueneza tamaduni za kizungu. Matokeo yake utambulisho wa kiafrika umepotea kabisa sababu ya kuwa brainwashed.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…