Interesting Histories, Interesting Stories

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,264
INTERESTING HISTORIES INTERESTING STORIES

Kuna mtu kaniandikia anatafuta kazi imshughulishe kaniomba msaada.

Nimemwandikia hayo hapo chini na nimeweka hapa ili mwingine yeyote atakae shughuli ya kufanya aone labda In Shaa Allah yatamfaa:

"Umesoma kitabu cha Abdul Sykes?
Unaweza kupata mengi ya text show.

Kuandika mimi ni kurudia ambayo tayari nimeyaandika.

Ukiingia mohamedsaidsalum.blogspot.com unaweza pia kupata makala nyingi nilizoandika za watu wengine tofauti.

Mtafute Ali Migeyo, Ali Msham, Iddi Faiz Mafungo, Salum Mpunga na Yusuf Chembera (hawa historia zao zinakwenda kwa pamoja), Haruna Taratibu (unaweza kumuunganisha na Omari Suleiman), Rashid Ali Meli (huyu unaweza ukamuunganisha na Iddi Faiz Mafungo).

Hawa wote ni katika kundi la wazalendo waliokuwa TANU mstari wa mbele.
Ali Migeyo ana nini muhimu katika historia ya Tanganyika.

Tanganyika Intelligence Summary ripoti za kikachero za Special Branch zinamtaja Ali Migeyo kuwa, "Illiterate," yaani hajui kusoma wala kuandika.

Kuwa Ali Migeyo anajua kuandika kwa Arabic Script kwa wakoloni bado hujajua kusoma wala kuandika.

Ali Migeyo kafungwa Jela ya Butimba na Waingereza kwa kupigania uhuru wa Tanganyika mwaka 1953 na akafungwa na serikali ya Tanzania huru mwaka wa 1965 kwa kupigania haki na usawa.

Salum Mpunga ana nini?

Mwaka wa 1955 Salum Mpunga alisafiri na mwenzake Ali Mnjale kutoka Lindi kuja Dar-es-Salaam kumfuata Nyerere aende Southern Province akawasaidie kuondoa propaganda kuwa Waislam wameunda TANU Lindi kuleta vita vipya vya Maji Maji kama walivyofanya akina Nduna Abdulrauf Songea Mbano.

Haruna Taratibu akimuusudu sana Dedan Kimathi na Mau Mau bila hofu alitoa kadi yake ya TANU akaiweka mezani kwa DC Mzungu aiangalie.

Kuna mswada wa kitabu cha Ally Sykes very interesting (haupo kwenye blog).

Katoroka nyumbani kaacha shule ana miaka 16 akajiunga na KAR 1942 ili aende Burma, Vita Vya Pili Vya Dunia kumfuata kaka yake Abdul Sykes.

Akiwa Lower Kabete mafunzo ya kijeshi akakutana na Peter Colmore kijana wa Kiingereza na yeye yuko jeshini.

Urafiki wa hawa wawili ulidumu kuzikana na Colmore ndiye aliyemtajirisha Ally Sykes akawa millionaire katika umri mdogo sana.

Wawili hawa walikuwa katika biashara pamoja enzi ya Tanganyika lakini ilivurugika baada ya uhuru.

Hii ni moja ya changamoto za uhuru.

Mtafute Colmore katika blog unaweza kumtia katika text show alikuwa mtu maarufu sana katika broadcasting na entertainment Afrika ya Mashariki na mtu wa kwanza katika nchi hizi kurekodi muziki na kuuza.

Ninachoweza kufanya ni mimi kupiga video nikamzungumza kwa labda dak. 45.

Utaiangalia na utaandika kwa ajili ya text show yako.

Kazi zangu hazina hatimiliki ila naomba acknowledgement tu."
Kazi kwenu waandishi na watafiti.

1701187993424.png

Ally Sykes na Peter Colmore, Paris 1963
1701188104043.png

Haruna Iddi Taratibu
1701188150933.png

Kitabu cha Maisha ya Ali Migeyo
1701188213437.png

Kulia wa kwanza ni Haruna Taratibu na kushoto wa kwanza ni Iddi Faiz Mafungo kati ni Juliusn Nyerere kushoto kwake ni Saadan Abdu Kabdoro na kulia ni Sheikh Mohamed Ramiya Railway Station Dodoma 1955/56

 
Alikua anapambania haki ipi iliyompelekea akaishia kufungwa
Mpaji...
Ali Migeyo alikuwa anapigania uhuru wa Tanganyika.

Uhuru ulipopatikana akawa bado anapambana na serikali kutafuta haki kwa wananchi akawekwa kizuizini.
 
Back
Top Bottom