Hii ni kwa mujibu wa blogu ya Mbeya Yetu. Jana Bi harusi mmoja aliingia mitini; hakutokea kabisa kanisani wala kwenye ukumbi wa sherehe. Wanakamati walishikwa na butwaa huku wengine wakilia. Licha ya Bi harusi kuingia mitini, sherehe iliendelea kama kawaida ukumbini jana usiku. Bwana harusi alishindwa kuja ukumbini kwa machungu aliyokuwa nayo. Kwa mujibu wa blogu hiyo sababu ya Bi harusi kuingia mitini bado haijafahamika. Sikupenda kuweka picha lakini kwa vile leo ni April fool watu wasingeamini hii habari.
Maandalizi ya ukumbi wa harusi kama yalivyokuwa yanaonekana jana.
Wanakamati wa harusi baada ya kupewa taarifa yakuingia Bi harusi kuingia mitini. Baadhi yao waliangua kilio ukumbini hapo.
Wazazi wa bwana harusi wakishuusha maombi ukumbini hapo.
Wazazi na ndugu wa bwana harusi wakiwa mbele ya wageni waalikwa.
Dada za bwana harusi pamoja na wazazi wakipokea zawadi kwa niaba ya bwana harusi ambaye naye alishindwa kuja ukumbini kwa machungu aliyokuwanayo
Baadhi ya waalikwa wakiwa haamini kilichotokea
Mama mzazi wa bwana harusi akitambulishwa bila kuwepo kwa maharusi.
Kwa picha na habari zaidi tembelea blog ya Mbeya yetu:
Mbeya Yetu