Beyonce ajifungua watoto mapacha

Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,012
8,126
Beyonce Knowles and Jay-Z 'welcomed twins earlier this week'

beyonco 1.jpg


Ni nyakati za furaha kwa wapenzi/wanandoa Beyonce na J-Z baada ya kuwakaribisha mapacha wao wachanga kabisa mwishoni mwa wiki hii. Gazeti la US Weekly liliripoti.

Kulikuwa na siku za mijadala katika mitandao ya kijamii kuhusu kujfungua kwa mwanamuziki nguli mwenye miaka 35 katika kituo kimoja cha afya huko Los Angeles nchini marekani. Mdogo wa mwanamziki huyo, Solange Knowles alionekana akirandaranda kwenye kituo hicho cha afya, ndipo mapaparazi walipojisogeza ili kufahamu undani wa jambo hili.

Mwanzoni mwa mwaka huu mwanadada huyu alipiga picha mbele ya ua kubwa huku kashikilia tumbo lake na kupost kwenye ukurasa wake wa instagram kwamba wamebarikiwa kwa kutarajia kuleta zawadi nyingine.

beyonce-pregnant.jpg



Supastar wa miondoko ya Hip Hop Jay Z, mwenye miaka 47 Jumanne iliyopita alionekana akiondoka kwenye kasri lao lililopo Beverly Hills na kuelekea kwenye kituo hicho cha afya na mara ulinzi katika kituo hicho uliimarishwa.

beyonce 2.jpg



Mapacha hawa wanaungana na Blue Ivy, binti wa wapenzi hawa mwenye umri wa miaka mitano.

beyonce 3.jpg



Wapenzi hawa walioana mwaka 2008 baada ya kuishi miaka mitano ya uchumba.




643017036.jpg


Chanzo: Beyonce and Jay-Z 'welcomed twins earlier this week' | Daily Mail Online

beyonce 4.jpg


Haya sasa fans wa wanamuziki hawa jaribuni kubashiri majina watakayopewa mapacha hawa
 
Mda mwingi wanalazimisha kujificha. Tokea mwezi wa tano Beyonce kapotea katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kisa tu siku za kujifungua zi karibu. Alipojifungua mtoto wa kwanza alijificha miezi takriban sita bila kuonekana
Siyawezi haya kwakweli.
 
Bora hawa mastaa wakubwa wanapata watoto kwenye ndoa zao lkn njoo Bongo bahat mbaya wanaweza kuigiza mambo mabaya kutoka mamtoni
Hahaahahaaaa. Bongo wenyewe wanasema tafuna mifupa ungali bado na meno. labda siku za mbele watabadilika
 
Sioni raha mimi hapo naona karaha tu.
Waswahili wanasema siri ya mtungi aijuae kata. Ma celebrity wengei wangekuwa hawapendi maisha yale wangeamua kuishi maisha ya kawaida. lakini kila kukicha ndio wanazidi kujikita kwenye wanachokifanya
 
Wale mnaosema inabidi uwahi kuoa na kupata mtoto, hili la J kupata mtoto akiwa na miaka 47 mnasemaje?

Kama unategemea watoto kama non current asset wahini kuoa na kupata watoto. Mengi kazaa watoto ana miaka zaidi ya 70.
Tofautisha Bongo na huko kwa watu maan ht wazaz wakiondoka mtoto ana uhakika wa Ku exist lkn kwetu bila mwenywe kuwepo c ajabu familia yako kupotea kwenye uso wa Dunia mfano ulizia mapato wanayopata familia ya Marehemu Michael Jackson
 
Wasije tu wakatoza hela kufahamsha dunia watoto wao ni jinsia gani,mana wale kila kitu kwao ni biashara
 
Back
Top Bottom