Beta Male na Alpha Male

Wakuu hivi huwa hayo maneno mawili hapo juu huwa yanakuwa na maana gani, maana naona yanatumika sana kwa wakati huu?
Welcome to redpill society.

Ufafanuzi

BETA MALE

Kwanza Beta ni neno la kilatin lenye maana ya badae au ni kitu kinachofuata baada ya ile iliyo imara kwa maana nyingine beta ni " dhaifu"

Beta male ni Nani?

Beta male ni mwanaume dhaifu katika nyanja mbali mbali za kijamii uhusani kwenye upande wa mahusiano. Zifuatazo ni sifa za beta male

-Beta male ni mwanaume asiweza kusema "NO" kwa chochote kile anachoambiwa na mwanamke akiamini kwamba ndio ustaharabu au ugentleman.

-Beta male ni mwanaume ambaye Yuko tayari kufanya Jambo kwa ajili ya kumfurahisha mwanamke hata kama litamgharimu yeye kiafya au kiuchumi yeye anachoangalia ni mwanamke kufurahi.

-Beta male ni mwanaume ambaye yuko tayari kuwapuuza wazazi au jamaa zake wa karibu ambao ndio wana uchungu na yeye na kufuata matakwa ya mwanamke wake aliyekutukana nae ukubwani.

-Beta male ni mwanaume anaempa thamani kubwa sana mwanamke kuliko inavyopaswa na kuishusha jinsia yake, mara nyingi huwa yuko tayari kumuangamiza mwanaume mwenzake kwaajili tu ya maslahi ya mwanamke.

-Beta male ni mwanaume asielewa chochote kuhusiana na women manipulation.

-Beta male ni mwanaume anayeona fahari kudate/kuoa mwanamke ambaye tayari ameshakuwa damaged akiamini eti ni mkomavu wa kifikra hapa unakuta anaoa single mother, kahaba mstaafu n.k

-Beta male ni mwanaume ambaye anawekeza kwa mwanamke kabla ya kuwekeza kwake mwenyewe, hapa unakuta anamsomesha au kumkopea mkopo wa biashara mwanamke ilihali yeye bado anaishi nyumba ya kupanga.

-Beta male ni mwanaume ambaye anafanya Jambo ili aonekane yeye ni "real man" kwa mwanamke, pasipo kufahamu hicho cheo huwa Wanapewa wanaume mabwege.

-Beta male ni mwanaume ambaye anaona dawa ya mwanamke mjeuri na msaliti basi ni kumuongezea upendo na kumtoa outings za gharama na akishindikana sana anamuachia nyumba na mali zote walizochuma kisha yeye anaenda kuanza maisha upya.

Beta male ni mwanaume anayetumia zaidi emotions kuliko logic kwenye mahusiano.

-Beta male ni mwanaume mtiifu kwa mwanamke na mara nyingi huwa Wana dharauliwa Sana na wanawake.

-Beta males ni wanaume wanaoongoza kulizwa lizwa ovyo na wanawake kwenye mahusiano.

NOTE: KUNDI HILI LA BETA MALES KWA JINA LINGINE WANAITWA "SIMPS" au " WHITE KNIGHTS"

ufafanuzi kuhusu ALPHA MALES

Alpha ni neno la kilatin lenye maana la inayoanza au iliyo na nguvu zaidi. Hivyo basi Alpha Male ni mwanaume imara anayeitambua na kuilinda nafasi yake hapa duniani.

Zifuatazo ni sifa za ALPHA MALE

-Alpha Male ni mwanaume anayejali maslahi yake Kwanza kabla ya kuangalia maslahi ya watu wengine.

-Alpha Male ni mwanaume anayeishi kwa kufuata principals zake alizojipangia mwenyewe pasipo kuangalia watu waliomzunguka wanamchukuliaje

-Alpha Male ni mwanaume ambaye akiamua kufanya Jambo kwa ajili ya maslahi ya wengine, Basi anafanya pasipo kupendelea jinsia yoyote ile yaani atahakikisha manufaa yake yanamlenga kila mtu.

-Alpha Male ni mwanaume mwenye vision na siku zote anakimbizana na dreams zake.

-Alpha Male ni mwanaume asiyekuwa na muda wa kubembeleza mwanamke, siku zote yuko tayari kubwaga manyanga kwa mwanamke asiyeeleweka yaani hana muda wa ku-entertain dramas.

-Alpha Male ni mwanaume anayepeleka mambo yake kwa logic yakiwemo ya kimahusiano, yaani kabla hajafanya maamuzi anapima Kwanza faida na hasara zake.

-Alpha Male ni mwanaume anayeingia kwenye mahusiano/ndoa huku tayari akiwa na exit plan, hili mambo yakienda ndivyo sivyo anakuwa hana cha kupoteza

-Alpha Male ni mwanaume mwenye Kinga dhidi ya women manipulation na ni nadra kuingizwa mkenge na mwanamke.

-Alpha Male ni mwanaume mwenye upendo wa Hali ya juu kwa mwanamke wake, lakini upendo huo unakufa Mara moja pale tu mwanamke huyo anapo msaliti.

-Alpha Male ni mwanaume anayeitambua majukumu yake kwa mwanamke kama mume, na hawezi kubeba jukumu la mume kwa mwanamke ambaye bado hajamuoa.

-Alpha Male ni mwanaume ambaye hayuko tayari kula makombo ya mwanaume mwenzake, mara nyingi akitaka kuoa anatafuta mwanamke bikra na hawezi kabisa kuoa single mother au mwanamke aliyekwisha tumika Sana.

-Alpha Male ni mwanaume asiyejilinganisha hata kidogo na mwanamke, yaani yeye siku zote ana dominant traits na anazionesha pale inapobidi.

-Alpha Male ni mwanaume mwenye high level of masculinity and he uses it for better purposes.

-Alpha Male ni mwanaume asiyejali kabisa kuonekana yeye ni misogynist kwa maamuzi na mitazamo aliyonayo mathalani yeye anaiona ni sahihi.

-Alpha Male ni mwanaume anafanya juu chini kabla hajaondoka kwenye hii duniani aache legacy.

NOTE: ALPHA MALE NDIO MWANAUME AMBAYE KILA MWANAMKE ANA DREAM YA KUOLEWA NAYE KWA BAHATI MBAYA WAKO WACHACHE SANA KWENYE DUNIA YETU YA LEO.



Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Daahh huyo Alpha male ulivyokuwa Una mzungumzia nimeona Kama vile unaniongelea mimi kabisa yaani totally "

Yaani umenigusa kila angle in short alpha male Ni wabinafsi Yaani wanajifikiria wao kwanza kabla ya wengine Kipaumbele cha kwanza Ni maisha yao cha pili Ni kazi au Rasilimali zao na cha Tatu ndio mahusiano

Mara nyingi huwa hatudumu kwenye mahusiano cause huwa hatuwezi kuvumilia ujinga na mahusiano ya siku ili yaweze ku-exist yana hitaji usitumie logic kwenye mahusiano hapo ndio balaa huwa linaanza kwetu
 
LOUD & CLEAR👏👏👏
 
Basi mimi ni Alpha female maana umenielezea vizuri kabisa japo kwa upande wa kiume ila ndivyo nilivyo
Kwa kweli kuna watu mnajua mambo. Lakini nothing in the universe is absolute. Kwa hiyo ukimkuta mwanamume ni 100% alpha huyo atakuwa unfit kwenye jamii. Vivyo hivyo wale ambao ni 100% beta watakuwa walegevu mno hata make hat an is in is vs a lama kuishi na mume dhaifu. Cha msingi ndoavinahitaji give and take. No wonder great people hawakuweza kuwa na mahusiano imara.

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kifupi ni kwamba ili dunia iweze kupendeza ni lazima kuwe na watu wa aina tofauti tofauti just imagine kama dunia nzima kungekuwa na watu wa aina moja dunia ingekuwaje,ni kweli kabisa ndoa inahitaji uvumilivu na kubebana na ni kupitia haohao beta na alpa beta atakutana na mtu wa aina yake na alpha nae atakutana na anaemmudu ila mwisho wa siku mambo yataenda
 
Alpha Male ni mwanaume mwenye high level of masculinity and he uses it for better purposes.
Hapo ndipo wengi hukosea kuhusu Alpha males. Wengi wao hawatumii msuli bali maneno, na kuhamasisha Beta males wawafanyie kazi zao zinazohitaji msuli.
beta males ndiyo wanaotumia sana msuli kufanikisha maisha.
Watumwa , makuli na watu wengi wanaotumia msuli ni beta males.

Napoleon, Adolph Hitler, Mussolini, Haile Selassie hata Samora Machel ni watu wenye maumbile madogo lakini wenye hotuba za kuhamasisha watu na kukaribia hata kutawala dunia.

Kwa sasa hivi, Vladmir Putin. kim Dynasty etc ...
 
hapo anafuata mtu anayeitwa sigma male huyu ndio habari ya mjini.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…