lost files
JF-Expert Member
- Apr 17, 2025
- 847
- 2,545
Alfa Male ni nani?
Ni Jambo la msingi na muhimu kujiuliza Alfa Male ni nani?.
Mwanaume wa Kweli ni nani??
Katika ujuzi wangu wa masuala ya maadili na asili,naweza kumfananisha Alfa Male na Mnyama Simba,anapovuka barabara pamoja na kundi lake huhakikisha kwamba wanawake wote,watoto na simba wadogo wadogo wanavuka kwanza.Yeye anasimama na kuzuia barabara wengine wavuke.
Alpha Male analiangalia na kulitunza kundi lake Wakati wa vita na njaa,.Katika wakati wa Njaa yeye anakula mwisho,Wakati wa Amani yeye hula kwanza(Japo hili sio lengo)
Lengo ni kutimiza majukumu yake kama mwanaume,.Ameumbwa kujali na kutunza. Ameumbwa kuwa mlinzi,ameumbwa kufanya jambo lililo sahihi kwa manufaa ya kundi kubwa la watu..
Anafanya hivyo kwa sababu ni asili yake.Hafanyi hivyo kwa kutegemea malipo
Look deep inside your nature na then jiulize:Nini unataka kutunza(to take care of).
jambo gani muhimu zaidi kuliko wewe mwenyewe? Unataka Kujitoa kwenye nini bila kutarajia malipo yoyote? Je ni Mungu? watoto? jamii yako?? familia?taifa lako??
Kitu gani unakijali zaidi kuliko unavyojijali mwenyewe??kitu gani ambacho uko tayari kukitetea, kukilinda,kukisimamia na kukipigania kwa gharama yeyote?..
Ningependa kumtolea mfano Tundu Antiphas Mughwai Lissu.,Licha ya kuwa ni mwanasheria mkubwa na msomi kwelikweli,alikua na uwezo wa kutengeneza Pesa kwa kutumia elimu yake,au kuishi nchi za dunia ya kwanza na familia yake,,Lakini mara zote amekua akipigania haki za wananchi wa kawaida,.
Mara zote anaendelea kupambana kwa kile anachoamini ni bora kwa Mtanganyika na Mzanzibar,.Vita dhidi ya Ufisadi akiwa bungeni,Mikataba Fake.,Katiba Mpya,Muundo wa Muungano,Tume huru ya uchaguzi,,Mapambano hayo yote yalipekelekea tishio la maisha yake baada ya kushambulia na "Watu wasio julikana" and still aka survive..
Na ikiwa yote hayo amefanya bila ubinafsi,kwa lengo la kujali na kuwasaidia wengine,basi naweza kusema bila shaka huyu sasa ndio mfano mzuri wa Alfa Male.
Huo ni udhihirisho wa Uanaume, Unaonyesha kwamba una nguvu,Jasiri,unaweza kusimamia unachoamini,kiasi kwamba unaweza kufungwa au kushitakiwa kudai haki za wengine,
Kupambana sababu ya wengine ni sehemu ya wajibu wako.Na kadiri matatizo yanavyozidi unakua jasiri zaidi na zaidi..
Kwa kusema hayo, njia bora ya kutaka kugundua kama wewe ni mwanaume kamili jiulize,
Wajibu wangu ni upi?jambo gani ambalo wajibu wa lazima kulitekeleza?
Jibu la wajibu lazima liwe la kweli kutoka moyoni,sio litokane na standards ulizowekewa na Jamii,Lisitokane na mambo ulio kariri kutoka kwenye vitabu,au mambo ulio fundishwa na wazazi wako,,isiwe jambo ambalo umetoa kutoka kwa Wanaharakati wa mitandaoni,.
DOKEZO
Jambo ambalo limekua trend siku hizi wanaume kuvimbia wanaume wenzao,kuonesha magari,kiasi wana Pesa,kuita vijana wasomi Masikini,kuonesha idadi ya wanawake walio nao(wanaitwa Pisi).. Na Wamekuwa maarufu kwenye mitandao ya kijamii..
Kuponda single mamaz hakukufanyi uwe mwanaume kamili,Kusema vijana wasomi masikini hakukufanyi uwe Mwanaume kuzidi wengine,kua bully mtandaoni hakukufanyi uwe Alfa,. Hayo yote ni kinyume chake(Lift others).
Tabia ya kutafuta sifa mtandaoni,Validation,or kuseek attention sio tabia za Alfa ni utoto.
Tukipatikana wanaume 1000 tu kama Lissu na marehemu mtikila,hii nchi Maccm wataikimbia..