Best Universities in Tanzania (2016)

Hata wazazi best wamezaa vilaza. Swali ni kwako wewe je ni best?
 
Ni kweli kabisa sababu kubwa ni ile undergraduate kujisomea mwenyewe unajenga uwezo mkubwa sana wa kujitegemea sasa huku juu baada ya degree ya kwanza ukifanikiwa kusoma utaratibu wa chuo walimu, vitabu kufundishwa unawakimbiza mpaka unawaonea huruma waliotoka vyuo vya kufundishwa ushahidi niao siwezi kuuweka hapa lakini najivunia kusoma OUT kwenye Interview huwa wanashangaa kama kweli nimesoma OUT.
 
sina uhakika na KIU , OPEN UNIVERSITY kuwa no 6 interesting
 
Umbuzi huu, nani kapanga huu uongo....
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
eh! hii hatari,SEBASTIAN KOLOWA MEMORIAL UNIVERSITY ya 31?nakataa.
 
hii ni orodha tu, hakuna chuo chochote cha kusinda any public university, au hivi vyuo vya private hamjui kama Mara nyingi vinapokea rejects,angalau kozi za afya


ubora wa chuo haupimwi kwa wanafunzi wangapi wanalipata div one kuingia pale..hicho kigezo hutumika kwa asilimia ndoho sana..

ubora wa chuo hupimwa kwa haya
1. Management ya chuo ikoje, yaani ina ubora gani
2. kuna prof walimu wangapi chuoni
3. kuna madactari walimu wangapi
4.TA na AL wangapi
5. Miundo mbinu ya chuo ikoje kwa maana ya facilities za kufundishia zikoje.

5.carriculum ya chuo ikoje.
6. Ubora wa elimu na mitihani inayotungwa ikoje! ni standard nk

so acha ujinga
 
 
watu wa education na sociology hamna vitu vya kufanya et, chuo bado hakijachanganya ndio maana wakati mwinge huwa naona bora serikali isiwape tu mikopo kama watu wenyw ni wendawazimu kama mtoa mada ya nini kupoteza pato la taifa
 
Na wataendelea kukushangaa sana..! Unajisifia kufanya interview zaidi ya moja..! Kweli OUT ni noma. Hivi ni interview ngapi hadi sasa..!?
Unafikiri wote wanafanya kazi moja kama wewe? Maslahi yanapokuwa mazuri na vyeti vizuri una uwezo wa kubadili kazi.Pole
 
....umewahi kusoma OUT?!, au unakurupuka tu ku-judge kitabu kwa kuangalia cover!
Mimi nimesoma DIT then OUT, aisee OUT ni hatari, mm naona kama inatakiwa iwe namba 1
 
Hii ranking ni sawa na kushindanisha "wagonjwa", nani mgonjwa zaidi? Weka ranking ya Africa nzima ili tujue tuko wapi badala za shindanisha "wagonjwa".
Hili nilishawahi kulisema ,ninalisema na nitaendelea kulisema .kuna watu mnajaribu kuvibeza vyuo vya private tu katika mapungufu lakini hamviangalii vyuo vya serikali pia ambavyo vimejaa uozo uliopitiliza . Trust me kuna vyuo vyuo vya private vinatoa quality education kwamfano KCMC pale kitabu kinapigwa si mchezo na sikatai kuwa kuna vyuo vya vya private vimejaa uozo lakini ukifanya utafiti utagundua elimu yetu imeshuka tu kiujumla ndo maana leo unaweza kuwachukua vijana 10 kutoka vyuo mbalimbali vya bongo na ukawafanyia interviews utagundua ninachokisema utakutana na vituko vya kuvunja mbavu no matter in what university hao vijana wanatoka na kwanini huwa hata hamjiulizi kwa nini wa Kenya na waganda majirani zetu huwa wanatubuluza sana likija suala la usahili katika kazi wakati tuna level sawa ya elimu ya chuo kikuu .kaa chini na tafakari acheni upambe wa kushabikia wagonjwa wanaoumwa ugonjwa unaofanana mimi kwangu hii ranking list ni upuuzi mtupu na usio na tija kwa taifa letu na maendeleo ya sekta ya elimu . Solution tuwe na elimu inayomwezesha mtu kujitambua na kupambana na kutatua changamoto zake na za jamii inayomzunguka ikiwemo uwezo wa kijiajiri amalizapo masomo pamoja na ubunifu katika carrier yake ili kuleta tija kwa taifa lake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…