Bernard Membe same old story

Nataka Sana kuamini Bernard Membe ana kitu 'interesting'anakuja nacho lakini nashindwa.

Nionavyo Mimi story ya Bernard Membe itaishia kule kule ilipoishia ya Lowasa na Mrema na wengine...

Umeandika ukweli mtupu. Wanajidanganya. Ataishia Kulia mwenyewe kama mtoto mdogo. System aliyoitumikia miaka yote na kuitetea sababu ilibeba malengo yake, imebadilisha gia juu kwa juu. Asipoangalia itamsambaratisha mazima
 
Mada Kama hizi ambatanisha na picha za karibuni za Bashite ziwe Kama appetizer. Kiba100.
 
Good analysis.

Hata wabunge wanaotaka kutetea viti vyao wengi huenda wakaishia nao kulalama wakati miaka mitano walikuwa na uweze wa kuweka sheria nzuri za uchaguzi

Ina maana anashindwa kuona hilo? Namsikitikia sana
 
Membe ni walewale hana jipya hiyo Tume waliiona bora kwa sababu waliamini kuwa watapewa nafasi ya kuongoza nchi ila kwa sababu sasa hivi yuko nje ya mfumo ndio anaiona ina walakini angekuwa na maono angekaa kimya sasa anadhalilishwa haki na watu wadogo kama kina Musiba
 
Na yote haya ni kwa sababu...they never thought the same 'system' will marginalize them someday!!
 
Mkuu The Boss, nakupa kongole kwa hoja murua ambazo umezianisha. Lkn nafikiri ni lazima tuangalie mazingira ambayo matukio ya mabadiliko yanapotokea, hali kadhalika na usimamizi wake unavyokuwa.

Kipindi cha Mrema alikuwapo Mwl. Nyerere, ambaye aliweza kuzuia mabadiliko kwa hoja murua kabisa, na hata kuweza kumnadi barabara mgombea wa CCM aliyeteuliwa. Baada ya Mkapa lilikuja kundi la mtandao ambalo liliweza kufanikisha chaguo lao na hata kuweza kumpa JK hatamu za uongozi wa awamu ya nne.

Awamu ya tano imekuja kwa uongozi wa bahati nasibu. Hali ambayo ilitokana na wanamtandao kukosa mrithi wa JK na hatimaye kujikuta wote wakiikosa nafasi ya mmoja wao kumrithi mtu wao.

Ujio wa JPM ulikuwa kama embe dodo ambalo limeokotwa pasipo kutarajia. Hali ambayo imempelekea kuendesha siasa kwa hisia badala ya msingi ya chama. Sasa kinachokea kwake ni kuwa ametengeneza uadui na CCM Asilia na kuamua kuambatana na machotara wa siasa andamizi.

Mkuu, kwa vyovyote vile, tusijaribu kulinganisha jitihada na matokeo ya vita hivi vya kugombea madaraka kwa mazingira ya sasa ya kisiasa. Membe bado ni mtu muhimu ambaye anaweza kubalisha "rules of the game" za siasa za wakati huu hapa nchini.
How can he change the rules wkt hata hio fomu hatopewa?!
Walimuwahi...zengwe lile la kumfuta uanachama
 
Umeandika ukweli mtupu. Wanajidanganya. Ataishia Kulia mwenyewe kama mtoto mdogo. System aliyoitumikia miaka yote na kuitetea sababu ilibeba malengo yake, imebadilisha gia juu kwa juu. Asipoangalia itamsambaratisha mazima
To be honest sio Membe tu...bali Ccm wao kwa wao wataisoma namba humo ndani...upinzani is no longer an issue..wameshadhibitiwa
 
Kila mtu ni mbinafsi, ila Waafrika tumezidi. Yanayotokea ni kwa sababu ya ubinafsi wao, as a result what goes around comes around.
It is all coming down to 'Mh. ataamkaje siku hio'
Wananchi tunabaki wapendwa watizamaji
 
Katika watu wasioamini wanaccm mimi ni mmojawapo, wengi wao hawana uwezo wa kweli wa kufanya siasa, kwani udhaifu wao unajificha kwenye nguvu za dola. Hii inapelekea wanapokuwa nje ya nguvu za dola kuwa wadhaifu sana. Huyo Membe ni mmojawapo ya wanaccm wadhaifu kabisa, kwani bila mbeleko ya vyombo vya dola hana lolote.

Sioni Membe akipata lolote kutoka kwenye hizi kelele zake, kwani nguvu za kupita kiasi zilizo kwenye katiba kwa rais, pia zina baraka zake. Watu wanamshangilia tu ili alete mpasuko huko ccm kama ataweza, lakini sioni jipya lolote toka kwake. Wapinzani wasitegemee lolote kutoka kwa Membe, maana nguvu zake ziko ndani ya system, nje ya hapo ni kama bunduki isiyo na risasi.
 
Mungu apishe mbali. Amen
Namnukuu Membe akihojiwa na DW jana:

"nisipopata haki yangu ya kugombea ndani ya ccm ntaitafuta nje ya ccm"
"unaweza kupanda basi toka mtama kwenda dar lakini ukishushwa njiani unapanda hata bodaboda kufika unakokwenda" mwisho wa kunukuu.

Membe anaenda ACT au chadema!

Wafuasi wa upinzani jiandaeni kudeki barabara zigo hilo laja.
 
Membe: nina maadui sita nikishinda Urais watahamia kenya

Adui moja wapo wa membe alikuwa yupo Chadema subiri tuone

Hata Wewe utakuja kuwa victim,kama sisi basi kizazi chako. MATAGA unafikiria leo yako tu ukipita buku 7 unakesha hapa.
 
Back
Top Bottom