Michael Uledi
Senior Member
- Mar 29, 2023
- 132
- 322
Msiba wa Mzee wangu Bernard Kamilius Membe umekuja kwangu na mafundisho makubwa mengi sana kuliko nilivyowahi kudhani kama siku siku ningeweza!Lakini kubwa nimeona uwepo wa "knowledge gap" kubwa kati ya kizazi na kizazi ndani ya Taifa ambayo labda ndio inafanya tuone hayo ambayo yanatokea kwenye Social Media hususani kwa vijana wa Taifa la Tanzania.
Naona kuna umuhimu sana wa kuanzisha "Idara ya Nyaraka na Elimu kwa Umma" kwa ajili ya Viongozi wakubwa wa taasisi muhimu na nyeti na Viongozi wa Kitaifa ambao wamefanya makubwa katika Utumishi wao kwa Taifa la Tanzania!
Vijana wengi wameamua kumthihaki Mzee Membe kwa sababu ya kukosa taarifa sahihi tu na angalau kumjua kidogo tu!Leo muulize kijana wa miaka ya 1980 Je,Mkuu wa kwanza wa Idara ya Usalama wa Taifa lako aliitwa nani?,hajui,hawajui na hawatojua kamwe!Muulize kijana huyo huyo Mzee Mwaikambo ni nani katika Sekta ya Bima/fedha?hautopata majibu ya maana!
Mitaala yetu ya elimu ya kisekta pia hajatambua mchango wa viongozi ndani ya sekta zao husika!Nenda leo kamuulize Mwalimu wa Chuo Kikuu pale UDSM-SJMC kuwa Mkurugezi wa kwanza wa Shirika la Utangazaji la Taifa alikuwa nani?hatokupa majibu!Madhaifu makubwa ya elimu ya Tanzania!Ni aibu ya mwaka and no body cares!
I.Vijana wangejua angalau gharama ya kumtengeneza Bernard Kamilius Membe mmoja wa viwango vyake wangeshangaa!Gharama ya muda na gharama ya fedha!Mimi sitoshangaa leo nikiambiwa gharama ya kumtengeneza KACHERO wa viwango vya Mzee Membe si chini ya Tshs Milioni 500 na labda uchukua miaka 15 mpaka 20 kuweza kumuiviaha katika hatua mbalimbali!
II.Kwa mujibu wa takwimu za haraka haraka ndani ya Jeshi la Nchi moja Ulaya,niliwahi kusimuliwa na Mzee mmoja ambaye siwezi kumtaja kuwa gharama ya kumtengeneza Ofisa mmoja(Cadet training cost per person) wa Jeshi la Marekani ni zaidi ya Tshs milioni 100 ndani ya mwaka mmoja kwa miaka ya 2010.
Mzee Bernard Kamilius Membe anastahili heshima kubwa kwa Taifa lake la Tanzania!Nataka vijana wa jamii Forum mjue haya!
III.Ofisa wa viwango na kariba ya Mzee Membe ndani ya "Chombo cha Mungu" uwa ni mmoja kati ya watu ambao wamesacrifice matamanio yao mengi binafsi ya kiakili,kimwili na kifamilia dhidi ya maslahi ya Taifa lao!Wakati Vijana wengi wa "kisasa"wanadhani "Kazi ya Mungu" ni kazi ya starehe na kukupa heshima mjini ukweli ni kwamba ni kinyume chake kabisa! Kazi za ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa ni kazi ambazo sio nzuri sana!
Mh Membe apewe heshima yake na vijana wa Taifa hili!
Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app