Benno Malisa aishambulia vikali CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Kaimu mwenyekiti wa UVCCM Benno Malisa amekishambulia kwa maneno makali chama CDM kwa madai kuwa kimekuwa kikiisakama serikali ya chama chake.
Akifungua kikao cha baraza kuu la UVCCM huko Dodoma amesema wapinzani ni wadanganyifu wakubwa na muda wao wa kutamba majukwaani umefika mwisho.Katika hali ya kushangaza Malisa aliwataka vijana baada ya kikao chao wajibu vikali mapigo ya upinzani kwa njia yoyote watakayoona inafaa kwa kile alichodai uvumilivu wake umefikia mwisho.

Source:Mwananchi
 
Malissa the Bogus Youth Wing President in the word
 

Hapo nilipopanenepesha pamenivutia! Kumbe amesahau kuwa vijana wao wengi sasa wanatembea kwa kutumia mikongojo!
 
Nadhani njia mojawapo watakayotumia uvccm kuwajibu wapinzani ni pamoja na kuendelea kuwachinja kama walivyoanza sasa.
 

Hapo kwenye red: Beno Malisa anasema nini? Nji yoyote maana yake nini? Igunda wamepotea watu, Arumeru wamechinjwa, wabunge wa CHADEMA wamevamiwa huko Mwanza. Je, wananchi wa Tanzania waendelee kuamini kuwa serikali ya CCM bado inayo nia na dhamira ya kutunza amani nchini? Usalama wa raia na mali zao ukoje?
 
Asiwachuuze mjipatie kesi mhangaike nazo, nawashauri vijana jihadharini na mipango ya hujuma ipangwayo na ccm, msishiriki, mwachieni Mwigulu na @Nape.
 
Last edited by a moderator:
Hili chama zee lina matatizo, kila siku wanaamrishwa wajibu mapigo, ujumbe huwa haufiki au wanaogopa?
 

Kwa kauli hii ya Malisa amekivua nguo chama chake
 
haya ni mambo ya siasa za maneno kushusha presha shemeji malissa uko jibu haya
 
Anamaanisha kuwachinja viongozi wetu hata kwa CHENSOO
 
haya nasubiri majibu nani anaweza leta ya uhakika karibu hapa
 
Malisa, the ever bogest politician of the era
 
Malisa yupo ndani ya "black box" so let him dig the grave of CCM
 
Hivi hana habari kuwa vijana wanaikimbia CCM kila kukicha? Ni vijana gani hao wakujibu mapigo.
 
Ni sawa na babu mzee akisikia au akiona kaburi lazima mifupa imcheze ndio hali iliyompata Malisa
 

Malisa unatumia na nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…