KUFUKUZWA KWA BENO MALISA - Malisa na Nape: Adui yao ni mmoja, bora wapatane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KUFUKUZWA KWA BENO MALISA - Malisa na Nape: Adui yao ni mmoja, bora wapatane

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 18, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Malisa na Nape: Adui yao ni mmoja, bora wapatane
  Mwandishi Maalum

  Toleo la 239
  16 May 2012


  [​IMG]


  HABARI za kwamba Benno Malisa, Makamu na Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM kufukuzwa ndani ya kikao cha Kamati Kuu na Mwenyekiti wa CCM, zilivuta hisia za haraka.


  Kitendo cha Nape Nnauye, Katibu Mwenezi wa CCM kuitisha kikao cha haraka sana akiwa na Malisa ili kukanusha habari hizo, kinathibitisha jambo moja tu. Kwamba, jambo lenyewe lilitokea, na kama ungekuwa ni uzushi, Malisa ndiye angeitisha na kukutana na wana habari.


  Si mara ya kwanza kusikia Benno Malisa "akichafua" hali ya hewa ndani ya vikao vya CCM. Mimi nimetokea kumpenda na historia ni hakimu wa kweli, Benno Malisa awe ndani au nje ya CCM ataifaa CCM kuliko viongozi wa sasa wa CCM wanavyoweza kuelewa kwa sasa. Nijieleze.


  Benno Malisa hamuogopi Mwenyekiti kama walivyo wengi ndani ya chama hicho. Mwenyekiti ndani ya CCM ni taasisi na "mungu mtu". Hahojiwi, hapingwi, hakosolewi na haambiwi ukweli usiotiwa sukari kwanza. Matokeo ya tabia hii, ndiyo yanayoiangamiza CCM kwa kasi ya ajabu.


  Tumewahi kusikia Benno Malisa akihoji dhana ya kujivua gamba ina maana gani na akaomba muasisi akieleze kikao cha Kamati Kuu ili wajumbe wote waelewe. Tumewahi kusikia au hata kushuhudia ndani ya vikao Benno Malisa akihoji uharaka wa kuwafukuza wanaoitwa mafisadi ndani ya chama bila kufanya uchambuzi wa kina kubaini nani si fisadi ndani ya CCM. Malissa kwa fikra za haraka na za ajabu, alisema hana pingamizi na kuwaita hao mapacha watatu kuwa ni mafisadi, bali angependa kujua nani si fisadi ikiwa hao watatu ni mafisadi.


  Alipopuuzwa, kulitokea tishio la UVCCM kuasi na tayari vijana walisikika kutoka kila upande wa nchi wakijiandaa kuelekea Dodoma. Kikwete aliishia kufoka na kurusha vijembe. Mpango wa kuvuana magamba ukakwama, ukaibuliwa mkakati mwingine wa kupeleka masuala yote kwenye kamati za maadili. Wenye akili tukajua, hayo ndiyo mazishi rasmi ya dhana ya kuvuana gamba. Kama Kikwete ni muasisi wa dhana ya kujivua gamba, Benno Malissa ni muasisi wa kifo cha dhana hiyo.


  Alipojiuzulu James Ole Millya na kujiunga na CHADEMA, watu wasiofikiri haraka walikejeli na kutukana. Benno Malissa alisema anasikitika kwa hatua aliyoichukua Millya, aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha. Malissa hakuona kama ni vema kupiga teke sufuria ulilowahi kupikia chakula kitamu. Malissa anatamani hekima na hatua za kisiasa zichukuliwe haraka kuliko kubezana na kuitana majina wakati huu chama kinapopoteza wanachama kwa kasi kubwa.


  Tumewahi kumwona Benno Malissa wakati wa chaguzi ndogo za Igunga na Arumeru Mashariki akijitahidi kuonana na wapinzani kwa agenda zenye manufaa ya jamii nzima. Aliguswa na suala la vijana kujihusisha na uvurugaji wa mikutano ya vyama. Akaona njia ya haraka na ya kudumu ni kuongea na wapinzani ili vijana wa pande zote waonywe na kutulizwa ili wajifunze siasa. Alionekana muasi ndani ya chama chake, lakini kimsingi yeye alionyesha uongozi unaoonekana kukosekana ndani ya chama chake.


  Suala la uteuzi wa wakuu wa wilaya ambalo inasemekana alilihoji na kusababisha afukuzwe ndani ya kikao ni la msingi. Wengi wamehoji uteuzi huu. Wengi wa walioteuliwa wanafaa zaidi kuwa makatibu wa CCM wa wilaya na mikoa kuliko kuwa wakuu wa wilaya. Malissa amekumbusha makubaliano ya mwaka jana kuhakikisha watendaji hawarundikiwi vyeo. Suala hili lilikuwa mwiba na kuibua mjadala mkali ndani ya chama wakati wa mapendekezo ya kuwaondoa wabunge katika NEC. Hata hatua alizochukua Mwenyekiti Kikwete kuwaondoa akina Membe katika sekretariati zililenga kutekeleza makubaliano haya ya awali.


  Inakuwaje tena wabunge wanateuliwa kuwa wakuu wa wilaya? Inakuwaje makatibu na wenyeviti wa CCM na jumuia zake katika mikoa na wilaya wanateuliwa kuchukua wajibu mwingine wakati uhai wa chama unasuasua katika wilaya na mikoa yao?


  Inakuwaje Mwenyekiti wa chama kinachotawala athamini zaidi kazi za Serikali kuliko za chama pale anapowaondoa watendaji wa chama kuwapeleka serikalini? Mbona tathmini ya akina Mukama iliyotumika kuasisi dhana ya kujivua gamba ilidai kuwa ndoa kati ya serikali na chama inakiponza chama zaidi?


  Mbona watu wengi wanashangaa jinsi CCM inavyonywea mbele ya Serikali na kushindwa kuisimamia? Maswali haya, ndiyo aliyouliza Benno Malissa akaishia kufokewa na kuamriwa kutoka nje.


  Kwa wanaoona mbali, watakubaliana nami kuwa mustakabali wa CCM uko mikononi mwa vijana kama Nape na Malissa. Ukitazama hata picha za vikao vya CCM utagundua kuwa chama hicho hakina uhai kikiwa mikononi mwa wazee wachovu. Asilimia zaidi ya 70 ya wanaofanya maamuzi ndani ya vikao vya CCM ni wazee walio zaidi ya miaka 50. Hawa wamelindwa na mfumo na wanaendelea kufaidi matunda ya mfumo lakini hawana njia ya kuubadili mfumo ili uwe na uhai mpya.


  Damu na fikra za kina Nape na Malissa zinahitajika ili kuiokoa CCM. Hivi sasa si siri kuwa ndani ya CCM hakuna mtu mwingine nje ya Nape na Malisa mwenye uwezo wa kuongea na vijana akaeleweka.


  Vijana wana hasira, wamekata tamaa na hasa wale wa vyuo vikuu. Sera na misimamo ya CCM ni mizuri kwenye makaratasi lakini haielezeki kirahisi kwa vijana. Wanaoweza kujaribu kama wangeacha unafiki, ni Nape na Malissa.


  Tatizo ninaloliona ni kuwa hata hao vijana (Nape na Malissa) hawajaelewa kwa uzito suala ninalozungumzia. Nape alimburuta Malisa kuja kumuaibisha mbele ya kamera za waandishi. Ni sawa tu na Idd Amin alipodaiwa amemuua Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana nchini Uganda, Janan Luwum, aliwaita waandishi wa habari Ikulu, akapiga picha naye na mkewe na watu wote wakaona. Idd Amin akawatukana waandishi wa BBC kuwa ni wazushi kwa sababu Askofu huyo ni rafiki yake kama wanavyoona wenyewe.


  Askofu alipulizwa, alitabasamu tu. Usiku huo huo, Askofu aliuawa, gari lake likachomwa moto na kudaiwa alipata ajali na gari likaripuka na kumuua. Kwa hofu ya kugundua ujanja huo, mwili wa Askofu ulizikwa na jeshi kijijini kwao badala ya kuzikwa kanisani Kampala ambako umati ulikusanyika na kaburi likiwa tayari limechimbwa.


  Kwa kukubali kuja na Nape mbele ya kamera ili kukanusha kuwa hakufukuzwa kutoka nje ya kikao, Malissa anaweza kuwa amefanya kosa kubwa la kisiasa. Muda utaamua.


  Lakini kosa kubwa liko kwa Nape Nnauye. Adui wa Nape na CCM yake si CHADEMA, si waandishi habari anaowaita wazushi, si Benno Malissa. Adui wa Nape na Malissa kisiasa ni mmoja. Huyo ni uongozi wa juu wa chama chao, ambao ni mzito kusoma alama za nyakati, mwepesi wa kuchonganisha watendaji ili iwe rahisi kuwaongoza, na mwepesi wa kuwatosa wanapoingia katika mgogoro wakati wanautetea na kukitetea chama.


  Nape anachelewa kujiunga na Malissa katika mapambano yenye maslahi mapana ya chama kuliko kuutumikia uongozi unaomaliza muda wake.


  Mmoja wa vigogo wa CCM ambaye hutumiwa na chama katika ufumbuzi wa mambo mazito yanayokanganya, alipata kunon`gona: Ili CCM iweze kushinda katika chaguzi zinazokuja, haina budi kuwaruhusu wagombea wake waitukane hadharani.


  Alimaanisha kuwa lazima aina fulani ya uasi iruhusiwe ili kukiokoa chama. Nilipoona Wilson Mukama akimkemea Edward Lowassa wiki iliyopita, hekima ya mjumbe huyo kigogo ikadhihiri.


  Inahitajika semina elekezi ya mtu asiye wa CCM, asiye na maslahi ndani ya CCM, asiye na kundi, akae na Kamati Kuu na NEC, awaambie mambo haya kwa uwazi na ukweli. Kufukuzana na kutofukuzana kwa sasa, hakuisaidii CCM maana wanaofukuzwa na wanaobaki wote ni wale wale.   
 2. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,964
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kuna pengo kubwa la uongozi ndani ya ccm na bila wenye chama kuukubali ukweli huo na kurekebisha haraka iwezekanavyo chama hakitasalimika. 70% ya viongozi wa chama ni wazee ambao hawana mvuto tena kwa wananchi, hasa vijana, kwa sababu ni mafisadi na hawajali maslahi ya wananchi. Hao 30% waliobaki yawezekana ni vijana, na wanaweza kukubalika kwenye audience, lakini hawaaminiki ndani ya chama chao wenyewe.
  Hiyo inaonyesha hakuna daraja ya kati viongozi wanaoweza kuaminika ndani ya chama na wakakubalika kwenye audience ya watanzania wa leo.
  Kwa mantiki hiyo, ccm haina tena watu wa kuitetea kwa wananchi. Bila kuamka usingizini na kurekebisha mambo kama hayo, kifo kinawanyemelea kwa kasi ya kutisha. Maombi yangu ni kwamba wasirekebishe chochote ili ukombozi wa nchi yetu uwe rahisi kama kumsukuma mlevi!
   
 3. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Beno Malisa ni mchezaji mzuri aliyevaa na jezi chafu
   
 4. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Beno Malisa anapoteza muda wake kubakia CCM inayokufa. Beno na vijana wa aina yake wenye maono ya utaifa ndani ya CCM wanapaswa kufanya maamuzi magumu kabla mambo hayajaharibika zaidi. Kwa wajuzi wa historia ni kwamba CCM sasa hivi iko ktk awamu ambayo tukio dogo linaweza sababisha kishindo na kifo chake!
   
 5. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Magumashi za siasa za bongo.
   
 6. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Gazeti gani mkuu? well,wamesema kweli,hali ni mbaya sana ccm na Malisa akiacha uoga akaondokana nacho atakuwa amejijengea heshima na unyoofu wa nafsi yake
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Benno, utarogwa!!!! Chama kina wenyewe hicho, kila siku wanashinda kwa waganga.
   
 8. k

  kijiichake JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Jamani mimi natofautiana nanyi nyote , mleta uzi na wachangiaji. Ninachokiamini mimi kwa wakati huu ni kuwa! Ukimwona kijanana yeyote mwenye umri wa miaka 40 kuteremka bado yuko ccm, huyo atakuwa hana akili timamu, aidha amechanganyikiwa, au anatatizo la kutokuona kusikia na kufanya maamuzi, ama kalazimishwa, hao wakina nape na mallisa waachani tuu, hawajui watokako na waendako.
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Kazi kweli kweli mwenyekiti wa ccm anaogopa kivuli chake jamani,kumfukuza kikaoni si suluhisho,ukweli umebakia pale pale kuwaa JK ametoa nafasi DC ama zawadi ila hajaangalia weredi kama inavyotakiwa na kukubaliana ndani ya vikao!!!
   
 10. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,787
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
   
 11. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  hivi huyu malisa si ndio alikuwa bingwa wa kutoa matamko kipindi cha kampeni za 2010?kichwa maji tu huyu,ccm ndio inayomfaa
   
 12. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Nahisi hii atiko inetoka kwenye gazeti la Mtanzania. Kama ndivyo hakuna cha kujadili hap
   
 13. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  nasoma comments zenu, moja baada ya nyingine.
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hahaaaaaa....ole wake atakayempinga mwenyekiti atakufa ghafla.....
   
 15. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  CCM imebaki kuwa club ya watu wachache wasiokuwa na uchungu kabisa na nchi yetu! Kwa sasa club hiyo haitakiwi kuonewa huruma hata chembe bali inatakiwa kuachwa ili ife haraka sana.
   
 16. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  siasa mfu
   
 17. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  All in all, RIP ccm!
   
 18. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  " Kufukuzana au kutokufukuzana hakuisaidii CCM kwa sasa. Maana Wanaofukuzwa na Wanaobaki wote ni Wale wale"
  Nimeipenda hii!
   
 19. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapana mkuu ni Raiamwema! mi nimefurahi aliposema mwanasiasa wa ccm ili asikilizwe na umma anatakiwa akitukane kidogo chama na serikali yake! kama kweli duh! ni balaa nadhani alimaanisha chama kuruhusu kukosolewa kwa wazi na wanachama wake ili waonekane na umma kuwa wako huru kutoa misimamo yao.
   
 20. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Malisa alimpa kiasi gani mwandishi wa hii stori yake?
   
Loading...