Benki Zetu zijikite Kibiashara Kuuliko Kumtegemea "Baba Wa ubatizo"

Quinine Mwitu

JF-Expert Member
Oct 19, 2014
5,267
5,665
Juzi nilienda Bank moja ya hawa jirani zetu wakenya,kwa lengo la kufungua account ili niwe nachukulia mshahara wangu kupitia benki hyo,baada yakuridhishwa na huduma zao,mwanzo nilikuwa benki ya hapahapa kwetu,si kuridhia baadhi ya huduma,
Nilipofika kuomba bank statement huku benki kwetu,nikakuta kidogo nyomi haipo kama kule kwa wenzetu,sasa nikawa najiuliza nini kimesababisha hali hii,nikawa nakumbuka baadhi ya thread zikisema kuwa moja ya benk zetu CRDB imesitisha mikopo kwa muda,tatizo likiwa wafanyakazi wengi hewa walikuwa wana account zao benki zetu,ikiwemoCRDB,NMB nk,sasa kama hiyo ndio sababu kwanini hizi benk zisiwe zinajikita kufanya biashara au kwa lugha nyingine ziingie kwenye ushindani wa kibiashara kama zilivyo benki zingine,kuliko kutegemea kubebwa na serikali,maana kuna kipindi nimewahi sikia wafanyakazi wa serikali waichangia benki ya NMB ili iwe na nguvu,sasa huku kubebwa kutakuana ufanisi endapo kama mbebaji nae atakuwa na nguvu ya kufanya hvo,
Wenye ujuzi wenye ufahamu zaidi wa hili tupeni elimu nini kifanyike ili taasisi zetu za kifedha ziweze kujitegemea?
 
Back
Top Bottom