Benki za Ugiriki kufungwa kwa wiki moja

Benki za Ugiriki kufungwa kwa wiki moja

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
150629001507_greece_banks_shut_640x360_afp_nocredit.jpg

Raia wapigani foleni ili kutoa fedha katika mashine za ATM kufuatia kufungwa kwa benki nchini Ugiriki

Serikali ya Ugiriki imethibitisha kuwa benki zake zitafungwa kwa kipindi cha juma moja kufuatia uamuzi wa Benki kuu barani Ulaya wa kutoendelea kutoa fedha za kukabiliana na dharura.

Utoaji wa fedha katika mashine za ATM utadhibitiwa huku watu wakiruhusiwa kutoa Yuro sitini kwa siku,hatahivyo masharti hayo hayatawaathiri raia walio na kadi za benki za kigeni.

Katika hotuba iliopeperushwa na runinga za taifa hilo Waziri mkuu nchini Ugiriki Alexis Tsipras ameomba utulivu.

Mwandishi wa BBC mjini Athens amesema kuwa hakuna ishara za wasiwasi huku raia wakionekana kuelekea makazini kama kawaida.

Hatua hiyo ya benki kuu ya Ulaya inafuatia kuanguka kwa mazungumzo katika ya Ugiriki na mataifa ya Ulaya kuhusu makubaliano yanayokwisha siku ya jumanne ya kulikwamua taifa hilo kutoka kwa madeni yake,siku ambayo taifa hilo linafaa kulipa Hazina ya fedha duniani dola bilioni 1.6.

CHANZO: ​BBC
 
Kweli hakuna marefu yasiyo na ncha,ugiriki c ndo walikuwa wabobezi Wa marine navigation Hawa!
 
Ndio hawa hawa wazee wa Trojan Horse!!! Ustaarabu uliopo sasa Ulaya umejengwa kwenye misingi ya ustaarabu wa kale wa Uyunani(Ugiriki ya kale na Uroma. Huwezi amini hizo nchi zimegeuka MALI-SINA kiasi hiki....wala si lolote Ulaya kwa sasa!
Kweli hakuna marefu yasiyo na ncha,ugiriki c ndo walikuwa wabobezi Wa marine navigation Hawa!
 
ugiriki na ulaya nzima tatizo ni aging population, kule vijana wenye nguvu za kufanya kazi, na wenye taaluma ni wachache, Ulaya baada ya miaka kadhaa itakosa kabisa watu wenye uwezo wa kuzalisha, na kutegemea kuingiza watu toka africa, wacha waendelee kuto kuzaa watokomee katika uso wa dunia, watuachie miji yao wajukuu zetu wakaishi majasho ya babu zao, Asante Mungu.
 
Back
Top Bottom