Benki ya Vijana ya CCM kuanzishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Benki ya Vijana ya CCM kuanzishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, May 20, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  12th May 2012

  Benki ya Taifa ya Vijana inatarajiwa kuzinduliwa wakati wowote mwaka huu.

  Uzinduzi utafanyika baada ya mchakato wa kufunguliwa kwa benki ya vijana ya taifa kuingia katika hatua za mwisho, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM –(UVCCM) Taifa, Martin Shigela amesema.

  Alisema hayo wakati akizindua kikundi cha wajasiliamali wa umoja huo katika kata ya Manyoni mkoani Singida.

  Alifahamisha kuwa mchakato wa kuanzishwa benki hiyo kupata usajili wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Alisisitiza kuwa taasisi hiyo itawezesha wajasiriamali wa kati na wadogo yakiwemo makundi ya wanawake kujikwamua kiuchumi.

  Aliongeza kuwa ni azma ya serikali ya CCM ya kuwawezesha vijana hasa kuwapatia mtaji. Alisema tayari UVCCM ngazi ya taifa imefanya mazungumzo na mifuko ya hifadhi ya Jamii pamoja na taasisi nyingine za fedha ambazo zimeonyesha nia ya kusaidia vijana wakiwemo waendesha boda boda na vikundi vingine.

  Awali akisoma risala ya kikundi hicho cha wajasiriamali, Katibu Uhamasishaji wa Kikundi Bahati Matonya alisema kikundi hicho kinakabiliwa na changamoto ya vitendea kazi zikiwemo zana za kilimo.

  Alisema hali hiyo inakwamishwa maendeleo ya shamba la kikundi lenye hekari zaidi ya 200 na kumuomba Katibu Shigela kusaidia kupata wafadhili.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Washe wa funguwe Bank lakini wajuwe tume ya uchunguzi wa pasa chafu Mh Zitto Kambwe na Vijana wake wako, tutawatuma kuzipitia jee hamuna pesa za Umma? mara hii ccm honga honga ya kutumia pesa za Umma kuimarisha chama itakuwa ngumu kwa vile mfereji waliokuwa wakitumia umebanwa.
   
 3. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  safi sana ndio maana naipenda ccm
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Watajikopesha wenyewe kwa wenyewe. Mabilioni ya JK yalienda kwa nini?
   
 5. H

  Hacha Member

  #5
  May 20, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbinu za kujaribu kuwa-win back vijana!!! Too late!!!!!!
   
 6. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  kwa definition ya rushwa hii nayo imo
   
 7. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Zitakuwa hizi hizi ambazo ilikuwa ziende kulipia mikopo yetu vyuoni wao wanafungulia Bank,,eti ya vjana wa ccm,,hatudanganyiki!
   
 8. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #8
  May 20, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Hata wakianzisha nini, wewe jiulize CCM ilikuja na propaganda za BENKI YA WANAWAKE NA IKFUNGULIWA KWA MBWEMBWE ZA HALI YA JUU, SASA JIULIZE NI WANAWAKE WANGAPI WA VIJINI KULE LINDI, LOLIONDO, UKEREWE NA KWINGINEKO WALIO KOPA KWENYE HIYO BENKI,

  WATAKUWA WANAKOPA WAKINA SOFIA SIMBA NA WAPAMBE WAO
   
 9. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ulaji tena huo!
   
 10. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Sukita si ilianzishwa na ccm pia? Iko wapi leo?
   
 11. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yewoooomiiiiiii! Naona sasa CCM wanatafuta sehemu ya kuhamishia hela zetu zote, ili CDM tukiingia madarakani tusikute kitu. Wemeshajua 2015 hawana chao.
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mimi nitaomba kuwa cashier.
  najua madili humo ndo mahali pake kwasababu kama waliweza kupinga ndani ya b.o.t kwenye benk yao kila anayewahi kuchukua hakuna wa kumuuliza.

  ccm=chukua chako mapema.
   
 13. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #13
  May 20, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wanaanza kuunda mikakakati na myanya na mazingira ya kupora pesa zetu za walipa kodi na maliasili zetu kwa uchaguzi ujao.Walikua wapi kuanzisha bank hii hapo awali??Kwanini iwe bank ya vijana wa CCM?Na kwanini isiwe bank ya vijana?Ni vigezo gani vitatumika kutoa mikopo?Hapa kunamawili,kwanza ni mradi mwingine wa wajanja ndani ya CCM katika mkakati wa chukua chako mapema kabla chama hakijaporomoka,au hongo kwa vijana CCM kwa jinsi mlivyo ovyo hata kama kunania nzuri katika hili na mengine ni vigumu kuwaamini kwani imekua kawaida kushuhudia wakati wote,nia na maazimio yenu wakati wote ni kama ardhi na mbingu.Imefikia wakati kua mnatoa maelezo na uchunguzi wa kimahesabu katika miradi mlioanzisha kabla ya kuanza mipya.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  wenye meno nafasi hiyooooooo
   
 15. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Kula CCM, kura CDM, mikopo CCM, mioya CDM. Kwanza ni mapesa yetu.
   
 16. tikatika

  tikatika JF-Expert Member

  #16
  May 20, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,669
  Likes Received: 2,198
  Trophy Points: 280
  hata wafungue kituo cha kugawa hela bure bado haitasaidia!
  Ikifika siku ya kufa hata uende India utarud mait!
   
 17. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hahahaaaaa, huuuuuuwiiiiii sipati picha watakavyoitafuna!!!!!
   
 18. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ndo mwarubaini wa matatizo ya watz? wapi sukita?
   
 19. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza....wanahangaika, sisi inakaribia kukata roho, kikubwa ni kuandaa matanga tu...NO WAY OUT....!!!!
   
 20. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,524
  Likes Received: 10,441
  Trophy Points: 280
  mimi nitajiunga kuchukua mihela hiyo.kura si ni siri.?
   
Loading...