shaks001
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 1,246
- 1,070
Nimewahi kufanya kazi NMB,ninachojua ni kwamba pesa haiwezi kutoka akaunti moja kwenda nyingine bila idhini ya mteja,kuna kitu kinaitwa "standing order" yaani unajaza fomu ya makubaliano baina yako mteja na benki ili ikifika tarehe fulani pesa kiasi fulani kitoke kwenye akaunti yako na kiingie kwenye akaunti nyingine,mfano akaunti ya mtoto bila wewe kwenda benki kujaza fomu(Automatic debited and credited).Hilo la kwanza!
La pili(na hili ndilo linawakumba wengi), ni utapeli!Hapa kuna ushirikiano "mchafu" kati ya watumishi wa benki na wa kampuni za simu(baadhi wasio waaminifu) na hawa matapeli kwa kuvujisha taarifa za mteja.Hapa kidogo tuwe makini maana katika hili benki kama taasisi haihusiki na wala usijisumbue kudai haki yako maana moja kwa moja unaingia katika kundi la watu/wateja ambao hawakufuata masharti ya benki na hivyo kuitwa ulikuwa "mzembe".
Kinachofanyika ni kwamba kuna hao matapeli wanakupigia simu na kujitambulisha kuwa wao ni staff wa benki fulani,wanachofanya ni kucheza na saikolojia tu,kwanza watakutaja jina lako kabla hata hujawatajia,watataja namba yako ya akaunti,watakutajia kiasi kilichoingia, kilichotoka karibuni,nk.Baada ya hapo watajifanya kama wapo bize ofisini wanapokea simu nyingine watakuweka hewani kidogo huku kwa mbali ukisikia sauti za watu kama vile ofisini panavyokuwa bize(kumbuka hii ni katika kukuteka wewe akili ukiamini kwamba kweli hao jamaa wapo benki).Kisha baadae watakwambia kuna taarifa zako zinaonekana hazijaboreshwa kwa hiyo wanatka kuziboresha.Watakuuliza ulijaza fomu za kuboresha akaunti, utasema ndio;baadae baada ya kukuzungusha na maswali meengi na wewe kuamini ni watu wa benki watakuuliza,hivi namba yako ya SIRI ulitumia ile ile ya mwanzo ambayo ni.....(watataja no ya uongo mfano 1234), wewe haraka haraka utasema hapana natumia 1980.Ndugu yangu, UMEKWISHA!
Baada ya muda wa dakika kama mbili au tatu kama ulijiunga na huduma za kibenki kwa simu, wanai-swap line yako hutoweza ku-access huduma za kibenki kwa njia ya simu kuanzia muda huo,watahamisha kiasi cha pesa kilichomo kwenye akaunti yako kwenda kwenye no "fake" za simu zao na baada ya sekunde kadhaa hizo pesa zilizohamishwa kwenye hizo no zao zinahamishwa tena kwenda kusikojulikana na zile line zao pia wanazi-swap.Yaani ni wizi unaotumia akili sana hata jeshi letu la polisi nadhani kwa kutokuwa na wataalamu(sina hakika), wanashindwa kabisa kusaidia kutokomeza wezi hawa.
Kama huna utaratibu wa kwenda benki kuangalia salio ndugu yangu baada ya siku kadhaa hata ungekuwa na milioni 50 zinalambwa zote.Hawana ujanja wa kuhamisha kiasi kikubwa kwa siku moja ndio maana wanakuondolea access ya kuweza kuangalia hata salio kwa simu yako ili wao wapate nafasi ya kuendelea kuzihamisha.So ni vizuri kila wakati jaribu kuingia kwenye akaunti yako kama umejiunga na huduma za kibenki kupitia mitandao ya simu,ukiona huwezi kuona kitu usijiridhishe kusema tu kuwa ni tatizo la kimtandao, chukua hatua mbele zaidi.
Ndio maana hapo juu kuna wadau wamechangia kuwa muhanga wa tatizo hili aweke wazi mazingira ya kuibiwa ili watu wamshauri.Mi namshauri kama aliitoa no yake ya siri kwa mtu yeyote na pesa imeibiwa kupitia eidha ATM au kupitia mtandao wa simu,basi hapo benki haihusiki kwa namna yoyote maana wanashauri na kutoa matangazo kila siku, USITOE NAMBA YAKO YA SIRI KWA MTU YEYOTE.(Labda hapa kwenye neno 'yeyote' hatujapatilia maanani), yaani hata mkeo/mumeo.
Ila kama pesa imehamishwa ndani ya benki,yaani "account to account"; tafuta mwanasheria wako fungua kesi kifua mbele maana hiyo ni kesi nyepesi mno na uzuri ushahidi unao yaani benki itakulipa tu hakuna namna.
Kumradhi:
Najua kwa komenti hii naweza nikawa nimewaharibia " wapiga dili"hao lakini ni bora uokoe mamia na kupoteza makumi.