stujadiliane
Member
- Jun 2, 2017
- 66
- 84
Ndugu wanaJF, Mimi ni mtanzania mzalendo na wa kipato cha chini ambaye Benki yangu ya NMB Tanzania imenifanya sasa ni wewe omba omba baada ya kuibiwa pesa zangu zote ambazo nimezilimbikiza kwa miaka kadhaa.
Nakumbuka niliamua kuweka pesa zangu benki ili ziwe salama. Nimezungushwa vya kutosha katika kujaribu kutafuta haki yangu lakini bado nimekuwa nikiwasiliana na meneja tawi la NMB Tanzania Kinyatta road bila kupata mafanikio kwa miaka kadhaa.Nimejaribu kuomba msaada NMB Tanzania makao makuu mpaka sasa sijapata msaada.
Naomba Msaada ili nirejeshewe pesa zangu kwani pesa zangu zilikuwa zikihamishwa kutoka kwenye account yangu na kuingizwa kwenye account nyingine bila idhini yangu.
Hivi punde nitaweka vielelezo vyote vya barua ya Polisi,barua ya meneja NMB Tanzania Tawi la Kinyatta jijini Mwanza na barua ya meneja makao makuu.
Nataka muone benki ya wazalendo NMB Tanzania ilivyoyafanya maisha yangu kuingia shimoni.
----------Update------------
Asante wadau, nitaweka vielelezo vyote ninavyo kwani kesi hiyo ilifika polisi.Vielelezo vyote vinavyoonesha pesa zilivyohamishwa ninavyo na account zilipokuwa zinahamishiwa ninazo pia.
Katika barua ambazo nilizituma nilipomwandikia Mkurugenzi Mkuu wa NMB Tanzania niliambatanisha na vielelezo vyote.
Niliweka
1. Barua ya kufungulia kesi
2. Niliweka bank statement inayoonyesha pesa zangu zilivyo kuwa zikihamishwa kwenda kwenye account mbili tofauti.
Nilisambaza nakala hizo kwa...
a) BoT Mwanza
b) BoT Taifa
c) Mwanasheria mkuu
d) Mwanasheria wa mkoa wa Mwanza
e) Waziri Mkuu
f) Waziri wa Katiba na Sheria
g) Mkuu wa Mkoa Mwanza
h) Meneja wa tawi la Kinyatta NMB Tanzania,
i) RCO mkoa wa Mwanza.
Kati ya hao ni Mwanasheria wa Mkoa angalau alionesha kujali kwa kuniita ofisini kwake.
Aidha nakiri kupokea barua kutoka makao makuu NMB Tanzania, lakini haikuonesha msaada zaidi ya kusema tuwasiliane.
Miaka kadhaa imepita sasa naendelea kuzunguka meneja wa Tawi NMB Tanzania Kinyatta Mwanza ameishanipa maelekezo ikiwemo kunitaka niandike barua ya kuomba nilipwe lakini hata baada ya kuandika ni miaka sasa hakuna majibu.
Naomba msaada kwa Waziri wa Fedha anisaidie kwani wale ambao pesa zangu zilihamishiwa kwenye account zao wapo na tulishakutana Polisi na wakadai account zao hazitumiki.
Sielewi na sielewi naomba msaada wa haraka.