Benki ya Dunia: Mafukara waongezeka Tanzania

Benki ya Dunia: Mafukara waongezeka Tanzania

Serikali za wanyonge Mara nyingi huzalisha wanyonge wengi zaidi ili ziendelee kutawala maana haziwezi kutawala bila kuwepo wanyonge wa kutawala.
 
Fukara siyo masikini!,Ufukara ni ukosefu wa Cash hata kama una asset kiasi kikubwa sn lakini huna Cash basi wewe ni Fukara!Kwa hivo ni kweli mafukara ni wengi kwa sb hakuna mzunguko mkubwa wa pesa kwenye biashara lakini mabank yakianza kukopesha biashara then hiyo namba inaweza kupungua tena!

My point here is like Ufukara waweza kumkumba tajiri yeyote...Lakini huo siyo umasikini!

Hicho ni Kiswahili cha kikwenu. Fukara ni hohe hahe (zaidi ya umaskini). Ukosefu au upungufu wa pesa taslimu hauwezi kuitwa ufukara. Hilo ni tatizo la ukwasi.
 
Hao world bank ndio nini?

Nani aliyewachagua?

Sisi tulishiriki kuwachagua?

Tuna wawakilishi?
 
Shida ni umaskini wa kipato, wanachi huko vijijini rasilimali hasa ardhi wanazo za kutosha ila nyenzo za kuzifanya kuwa productive ndio tatizo kubwa. Lazima serikali ibuni interventions za kuwezesha hilo.
 
Mkuu wetu amesisitiza tuzidi kuzaliana
 
Ripot ya bank ya dunia imetoka

Ripot hiyo inaeleza kuwa tanzania ni miongon mwa nchi chache zenye mafukara wa kutupa

Bank hiyo inadai kuwa ndan ya mwaka huu mafukara wameongezeka na kufikia milion 13

Ripory inadai kuwa kas ya kuzalina imeongezeka kushinda kas ya uzalishaji, maisha ya watanzania walio wengi ni magumu kupindukia na mpaka sasa hakuna juhud zozote ambazo zimechukuliwa na selikal ili kupunguza wimbi la mafukara nchini

Kumbuka riport inasema mafukara ndo wameongezeka wala siyo masikin nahisi kuna tofaut kubwa sana kati ya masikin na mafukara, nahisi mafuraka ni wale walala hoi wa mwisho yaan wale masikin wa kutupa

Chanzo ni riport ya world bank na gazet la mwananchi

Mayala B
Kwa nini wasiongezeke ilhali korosho hazilipwi taslimu,pamba imedorola na mfumuko wa bei uko juu? Pia "jiwe" hutamba yeye ni wa WANYONGE!
 
Na rofa je
Lofa ni kutoweza kujihimili kwa namna mbalimbali. Ukishindwa kujihimili kwa kufanya maamuzi sahihi basi utakuwa umeangukia kwenye ulofa.

Tafsiri yake ni inategemea na jinsi muhusika atakavyolitumia.
 
Ripot ya bank ya dunia imetoka

Ripot hiyo inaeleza kuwa tanzania ni miongon mwa nchi chache zenye mafukara wa kutupa

Bank hiyo inadai kuwa ndan ya mwaka huu mafukara wameongezeka na kufikia milion 13

Ripory inadai kuwa kas ya kuzalina imeongezeka kushinda kas ya uzalishaji, maisha ya watanzania walio wengi ni magumu kupindukia na mpaka sasa hakuna juhud zozote ambazo zimechukuliwa na selikal ili kupunguza wimbi la mafukara nchini

Kumbuka riport inasema mafukara ndo wameongezeka wala siyo masikin nahisi kuna tofaut kubwa sana kati ya masikin na mafukara, nahisi mafuraka ni wale walala hoi wa mwisho yaan wale masikin wa kutupa

Chanzo ni riport ya world bank na gazet la mwananchi

Mayala B
Tuwekee hiyo ripoti ukiweza ili tujisomee wenyewe, tafadhali.
 
Fukara ni masikini zaidi. Kwa lugha ya kawaida "Masikini wa Kutupwa" au kwa jina jingine Hohehahe: Mtu ambaye hali yake ya maisha si nzuri, mtu asiye na mbele wala nyuma, masikini sana.
Msije mkajiingiza kwenye mambo ya takwimu wenyewe!
 
Kama huna uchumi wa kuingiza buku mbili jero kwa siku, ujue unaongelewa wewe hapa.
 
Ripoti za Benki ya Dunia ni ripoti za kibeberu na zenye lengo la kukandamiza nchi ambazo zimeamua kujitambua. Kama wewe hujajitambua utasifiwa kila siku. Ni sawa na mwanamke malaya kinachomfanya aendelee kuwa malaya ni kila mwanaume lzma amsifie. Sasa kama wewe siyo malaya kwa nini usifiwe ? Ni lini umesikia Marekani anasifia Maendeleo ya China au Urusi ? Kila siku ni kelele tu kama ambazo zimeanza kupigwa na hao unao waamini kuliko wewe unaeishi Tanzania na kushuhudia miradi mikubwa ya maendeleo ikifanyika. Miradi ya Umeme ndy chimbuko la Ustawi wa Viwanda hapa nchini na kamwe hatuwezi kuwa na maendeleo kama umeme wetu siyo wa uhakika.
Anayefahamu shida za familia zako na ni wewe mwenyewe kwa sababu ndy unayeamua kula nini wakati wa asubuhi, mchana na usiku. Mgeni hawezi kukwambia unaishi maisha magumu !!! Huo ni mtazamo wake akilinganisha na namna ambavyo yeye mzungu anaishi.
umejitahidi, umesahau kuwa DUNIA ya leo mataifa machanga hayana siri, hata makusanyo kodi ma hela zilizoingia hazina leo WB wanajua.
 
Ripot ya bank ya dunia imetoka

Ripot hiyo inaeleza kuwa tanzania ni miongon mwa nchi chache zenye mafukara wa kutupa

Bank hiyo inadai kuwa ndan ya mwaka huu mafukara wameongezeka na kufikia milion 13

Ripory inadai kuwa kas ya kuzalina imeongezeka kushinda kas ya uzalishaji, maisha ya watanzania walio wengi ni magumu kupindukia na mpaka sasa hakuna juhud zozote ambazo zimechukuliwa na selikal ili kupunguza wimbi la mafukara nchini

Kumbuka riport inasema mafukara ndo wameongezeka wala siyo masikin nahisi kuna tofaut kubwa sana kati ya masikin na mafukara, nahisi mafuraka ni wale walala hoi wa mwisho yaan wale masikin wa kutupa

Chanzo ni riport ya world bank na gazet la mwananchi

Mayala B

hivi tanzania watu wana itakia nini .na wewe unashabikia umetembea nchi za watu tena zilizo tajiri ukaona wazawa wenyewe walivo choka tena na kulala nje.
hizi takwimu na ujinga ujinga bado mnabebeshwa tu
 
Kwahiyo waTz tunakuwa mafukara kisa WB wamesema? Na siku wakisema tumekuwa matajiri ndio tunajihisi matajiri? Huu utumwa wa kisaikolojia utaisha lini lakini?
 
Back
Top Bottom