Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 91
Hata mimi Binafsi sijafurahishwi na Jk hata kidogo, amekuwa anaficha sana uhalisi wake na pia hata utendaji wake tofauti sana na BEN, Ben alikuwa makini japo madudu yake. Jk is freaking with his ambitions. \sijui akipewa miaka mitano mingine itakuaje??Pamoja na matatizo yote ya Mkapa, kuna mtu anaweza kutupa walau mambo 10 tu ambayo rais wetu mpendwa JK amelifanyia taifa hili tunapoelekea kufikisha mwaka wa tano?
Binafsi nasema JK is a failure compared to Mkapa. Hata kina Mpendazoe ambao Phillemon Mikael anawakandia wanatumiwa na JK kumwandama Mkapa ili kuficha mapungufu ya JK.
Nipende au nichukie lakini binafsi sifurahishwi na utendaji wa serikali ya JK ambayo ilikuwa inatafuta namna zote za kumpunguza Magufuli lakini Mungu wa Israel na Mungu wa Yakobo bado anamsimamia mtumishi wake Pombe Magufuli.
Kwa maoni yangu, Mkapa aliona jinsi hali ya uchumi wa nchi ilivyokuwa isingewezekana kupata nguvu ya ndani ya kuiokoa kwa haraka. Nadhani ndio maana aliweka juhudi kubwa kutoka kwa wawekezaji wa nje. Ninaweza kukubaliana nae kwenye hilo. Kumbuka inflation ya 48% alipokuwa akichukua nchi.Mkapa ni kweli alikuwa kiongozi mwenye agenda ya kueleweka kuhusu nchi yetu iende vipi, na kuna mambo mengi aliyofanya yanayoonekana, mfano TRA, ujenzi wa barabara, etc. Nisicho elewa ni kwanini utawala wake ukaruhusu corruption za kiwango kikubwa kama tulizoziona? Ilikuwaje wawekezaji aliwaona kama ndo warithi halali wa mali za TZ kuliko watz wenyewe? Sikazi yangu kuhukumu ila nafasi ipo ya yeye kutuambia yoote kuhusu hizi tuhuma zinazomkabili. Nafikiri anayochance ya kufanya hivyo. J
K bwana...duuh, story zimekuwa story!!!Yaani, we acha tu!!
Ni kweli kabisa na pia Pinda is more Nationalist, ila napata sana wasiswasi na Jk maana sijaelewa sana itikadi yake..!! Hana sana tamaa ya madaraka sana Pinda labda aje kubadilika baadae sana....pombe alikuwa obedient kwa mkapa ...na kwa maana hiyo mgombea yeyote ambaye alikuwa obedient kwa mkapa angepata urais ...lillikuwa chaguo la mkapa kwa uwaziri mkuu...
pinda...alikwa low profile kama nidhamu ya kikazi inavyompasa kuwa mtiifu kwa dola ..always yeye ni nationalist....[taifa kwanza]...NI WAZI HAKUWA KWA KIKWETE ..na kikwete hakumtaka....
...kikwete alitakiwa kumuweka pinda uwaziri mkuuu kama compromise kati ya watu wa mkapa,nationalists[wataifa]....kama angesaidia kuondoa hisia za umtandao....kikwete alikataa...lakini mwisho wa siku alikwama..akarudi kwa wazee ...na kumuweka pinda...
hata mkiangalia uteendaji wa pinda sio mwanasiaasa hata kidoho...lakini pia sio charsimatic..yeye ni mtawala zaidi....angepata rais mwenye msimamo dhabiti...angefanikiwa sana kusimamia kazi...,tatizo kubwa ni kuwa rais wetu hana kauli dhabiti....za kimamlaka!!! aliyekuwa akimsaidia kwa kauli za namna hiyo ni lowassa....na ndio kusema pamoja na uzuri wa pinda anashindwa jambo moja na lowasa ...charsima!!!
pinda sio tishio sana kwa nafasi ya urais ..kwa wanamkakati wa mwaka 2015...haoneshi tamaa ya madaraka!!!..he is a goob PM with poor president!!
Ni kweli kabisa na pia Pinda is more Nationalist, ila napata sana wasiswasi na Jk maana sijaelewa sana itikadi yake..!! Hana sana tamaa ya madaraka sana Pinda labda aje kubadilika baadae sana.
Rais bora wa TZ next to Mwl. J. Nyerere
Aliingia madarakani kwa haki bila rushwa wala kununua vyombo vya habari. Alikuwa na hoja na alieleza WAZI nia yake ya kugombea urais.
Alianza kazi kwa kasi hakungoja wiki mbili au zaidi kupanga baraza la mawaziri.
Aliunda serikali ndogo kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
Alikuwa na falsafa binafsi, dira na msomi aliyependa kusoma na kujifunza.
Akapambana kijemedari kwelikweli na misukosuko ya Reli, MV Bukoba, Elnino na majanga mengine. Akapunguza mfumuko wa bei toka 48% 1994 na kubakia single digit enzi zote za utawala wake.
Akaboresha utumishi wa umma; kapunguza wafanyakazi hewa na kuboresha maslahi.
Akapunguza deni la nje na kuipa Tanzania heshima.
Akajenga miundo mbinu hususan barabara kwa kasi kubwa
Akavutia wawekezaji wenye tija kama TBL, NBC n.k
Akajenga EPZ alipanga zijengwe 22 nchi nzima
Akaimarisha majeshi yetu kwa kuwapatia motisha vitendea kazi na makazi.
Akajenga Uwanja wa Taifa
Akajenga Benki kuu Twin towers na kule Zanzibar. Twin Towers kama Bank of Canada, Toronto (kwa wanaojua)
Alikuwa na hoja zenye mashiko.
Alikuwa kiongozi kweli jasiri, mwenye kujiamini na hakuogopa mihadhara: iwe ya vyama vya siasa, vyuo vikuu au kimataifa. Alikuwa full of substance.
Ujasiri wake hata vita ingetokea enzi zake angetuongoza vyema sana kumshinda adui.
Hakuwa mwongo katika kauli na ahadi zake.
Alikuwa na maadili na na hekima na aliheshimu mamlaka na taratibu zilizopo.
Akawapa nguvu na haki zaidi wanawake.
Alipigania utandawazi kuwanufaisha wengi.
Alikuwa mchapakazi hakuwa mvivu.
Alikuwa makini na alipinga na kukwepa sana matumizi yasiyo lazima ya serikali.
Alisafiri ngambo pale tu ilipobidi. Alikaa ofisini na kufanya kazi.
Alijiheshimu hakuwa Fataki.
Hakuwa ombaomba, bali alipenda kujenga uwezo, kujitegemea na kuwasaidia ombaomba.
Akanunua ndege bora ya Rais, mafisadi wakaipinga.
Akanunua rada ya nguvu, mafisadi wakaipinga.
Alikuwa na vyeti vya nguvu na alifuzu vyema masomo yake. Alionyesha uwezo. Alikuwa na speech za kisomi.
Alihakikisha nchi inakaribia kupaa ndio akaikabidhi kwa JK. Tukadhani itapaa.
Na mengine mengi.
Huyo ndiye Benjamin William Mkapa, Rais ninayemkubali na kumrank second. Angekuwepo mpaka leo Tanzania ingekuwa emerging economy I am sure.
Mnaomsema vibaya mshindwe ka kulegea. Hamna shukrani. Ni kiongozi ambaye wanaokumbuka, tunamshukuru sana.
Mawazo yenu please objectively and for the better future of our country ,lovely Tanzania.
Kumekuwa na kauli kuwa watu wa pwani ya bahari ya Hindi hapa Tanzania ni wavivu na blah blah nyingi. They are generalist and simplistic. Huridhika kwa vitu vidogovidogo tu. Kwa mfano wengi wao wako nyuma kimaendeleo na tumeona marais wote waliotoka pwani hiyo; Mwinyi, Mkapa na Kikwete performance yao kiuongozi mgogoro mtupu! Wakati mbara tena wa Musoma Nyerere alifanya mambo makubwa.
Natafuta Contacts za Mkapa
Kaniki1974 8th May 2009, 01:34 PM
--------------------------------------------------------------------------------
Namba za simu, postal na e-mail address tu please, za Benjamin William Mkapa Rais mstaaf wa URT. Sihitaji physical address. Thanks.
Sijakupa mzee wangu. Nina maana ya ideology yake maana huwa napata shida sana kujua hiloSaana Saana Tu! Duh!😀
He's very coal minded(sic) Hic!! tena sana😀
Sijakupa mzee wangu. Nina maana ya ideology yake maana huwa napata shida sana kujua hilo
Sasa mzee wangu upo wapi?? Mimi naona bora watangaze kura za Maoni kama kweli wanataka kumsafisha Mkapa!! yeye mwenyewe aliwahi kusema kuwa akiondoka watu wataanza kumshambulia sana kwa ajili ya mambo yeke alikuwa sahihi kabisa. Kama amekosea akiwa madarakani adhibiwe kama mwanadamu mwingine na pia ndio raha ya ofisi ya umma, lakini pamoja na yote haya Mkapa is better than Jk kwa utendaji na ni mkweli sana kuliko Jk, hata kama kuna watu wanakataa hivyo. then sijajua Jk huwa ana washauri wazuri kama JkUsijichanganye, tulia! Mie nilikuwa narudia- sana sana tu!😉
Hujanipa nini, Ideology?
Sidhani kuwa Mkapa ana kesi za kujibu. Bali ana shutuma nyingi ambazo wanaomshutumu hawajaweza hadi leo kuzifikisha mahakamni ili azijibu. Hivyo hana kesi yoyote.Ben Mkapa
Lakini watanzania sisi ni watu wa ajabu sana, kwa sababu sheria zipo na tunazifanyia marekebisho mara kwa mara tunapo hisi mapungufu, kiongozi yeyote anaongozwa na sheria zilizopo na kamwe hawezi kuwa juu ya sheria, tunaona wenzetu zambia na malawi wanvyofanya ukivurunda sheria itakuvurunda pia, Mkapa sio Mungu, ana kesi nyingi sana za kujibu na kuna watu wana ushahidi naye sasa kwa nini asishtakiwe? kama kujitetea mahakama ipo akajitetee huko ndiko haki na ukweli utapatikana, tatizo letu sisi watanzania ni waoga sana wa kutekeleza mambo, ni mabingwa wa kutoa hoja tu.