Bendera ya Tanzania na maana yake inaheshimika?

kanywaino

Senior Member
Sep 10, 2010
171
19
LEO ALFAJIRI MIDA YA SAA 11.30 NILIKUWA MAENEO YA AKIBA PALE CBE.KWA UPANDE WA PILI KWENYE OFISI ZA TaESA(WIZARA YA KAZI) PALE NIKAONA WANAPANDISHA BENDERA MUDA HUO,NILIVYOMWANGALIA ALIYEKUWA ANAPANDISHA HATA SIJAMWELEWA ALICHOKUWA AKIKIFANYA...NAOMBA MSAADA NIFUNDISHWE KAMA NINACHOJUA NI WRONG....MIMI NILIVYOFUNDISHWA WAKATI NASOMA NIKUWA BENDERA INAHESHIMIKA,INAPIGIWA SALUTE NA MUDA WA KUPANDISHWA NA KUSHUSHWA NDIO SINA UHAKIKA ILA SIDHANI KAM NI ALFAJIRI VILE.NAOMBA KUJUZWA KAMA SHERIA YA BENDERA KILA NCHI INAJIWEKEA AU NI STANDARD KILA UENDAKO?MNISAIDIE NATAKA KUJUA.
 
nakumbuka wkt nikiwa dogo nilikamatwa tanganyika jeki kisa nilikuwa natembea wakati bendera
inapandishwa mbele ya kituo cha polisi kama sikosei kushusha ni 12 jion kupandisha 12 asubuhi
tena inaopgwa filimbi wote mliopo eneo hili MNASIMAMA wima.lakini siku hizi kama ya sisism tu sio ishu tena
unakuta inashushwa muda sio na mambo mengine yooote kinyume hata washushaji wenyewe
hawazijui hizo sheria!
 
frola umesema vyema. Namshukuru sana mleta mada hii. Siku hizi sisi wenye nchi hatujui miiko na maadili ya nchi hii. Ujinga huu umo sana serikalini. Tuziangalie rangi za nembo ya Taifa (coart of arms) kisha tuangalie rangi za baadhi ya nembo/beji/chochote chenye alama ya bendera yetu kama vile leseni ya kuendeshea magari, hakika kinachofuata moyoni ni sikitiko kubwa. Angalia vibendera toka china vilivyojaa mitaani vilivyo na rangi zisizoeleweka, bado tunaziita alama hizi BENDERA YA TAIFA! Ninashauri serikali ianzishe kampeni maalumu ya kuifufua bendera halisi yenge rangi zilizokoza. Pia jinsi ya kuiheshimu bendera yetu. Sikumbuki vizuri lakini wiki hii nimepita mahali usiku na kukuta bendera ya Taifa ikipepea!
 
Vyama vingi ndiyo vimeleta dharau na kutoheshimu mambo muhimu kama haya.
 
kwa kweli bendera yetu haiheshimiwi na haitunzwi ipaswavyo, ukipita baadhi ya sehemu utakuta bendera chafu kweli na imechanika ovyo ovyo , ama kubaki kipande kabisa. hv nani mwenye majukumu ya kuitunza?!
 
Nachojua mimi ni kwamba rangi nyeusi katika bendera yetu ya taifa inaashiria - GIZA.
 
Back
Top Bottom