Nini maana ya bendera ya taifa kupandishwa asubuhi na kushushwa jioni?

GoPPiii.

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
1,787
3,050
Kwanza niwasaalimu ndugu na jamaa zangu ni matumaini yangu mko swadakta na mnapambana bado,hamjakata tamaa,na hongereni kwa wale ambao bado mko mjini kwani mkuu alisema atakaebaki mpaka miezi hii ni mwanaume.

Pili niende kwenye lililonifanya niwaandikie siku ya leo,nimekuwa nikiona bendera ya taifa ikipandishwa asubuhi na mapema na kushushwa jioni na filimbi hupigwa ili kuwafanya watu wasimame ili kulipa tukio hili heshima yake.

Maswali yangu ni,

1.Nini tafsiri ya jambo hili,kupandishwa asubuhi na kushushwa jioni?

2.Kuna maeneo ambayo bendera huwa haitolewi yaani inapandishwa hata usiku na ni yapi hayo?

Shukrani.

Philips X2560
 
Tazama Ramani utaona nchi nzuri,
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka !

Sent from my TECNO_N9 using JamiiForums mobile app
watu wanaeza fanya shuka
Itaibiwa mkuu.
Tazama Ramani utaona nchi nzuri,
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka !

Sent from my TECNO_N9 using JamiiForums mobile app
Yaani haya majibu yooote ni kiashiria tosha kuwa watanzania wengi hawana elimu ya uraia vichwani mwao.
 
Yaani haya majibu yooote ni kiashiria tosha kuwa watanzania wengi hawana elimu ya uraia vichwani mwao.
hahahahaha na wewe ujatoa jibu mkuu

kwa mimi navyo fahamu ni suala la heshima bendera ina sheria zake ili ieshimiwe ni pamoja na kupandishwa asubuhi na kushushwa jioni, iwe katika hali nzuri (isiwe imechanika, chakaa na mfanano wa huo)

haitakiwi kubebea vitu, kukanyagwa, ama kuburuzwa, kufanya ivo unakuwa umedharau taifa lenye bendera iyo.

hata pale unapotaka ipeperuke usiku kucha lazima kuomba ruhusa maalumu toka polisi wa eneo hilo na wanao husika.

Ufahamu wa mtaani: niliambiwa kupandishwa asubuhi ni kuonesha kwamba serikali inaingia kazini na ukomo wake ni saa 12 jioni, kuanzia hapo nchi inakuwa chini ya jeshi(polisi, j.w.t.z, magereza na mfanano wake) hivyo muda wa jioni bendera za majeshi ndo hupandishwa (sijui kama ni kweli hili)
 
Shukran kwa kunipa mwanga...

Philips X2560
 
Bendera haipaswi kushushwa/kupandishwa jioni na asubuhi, Bendera inatakiwa ikiishapandishwa mlingotini iendelee kuwepo hapo hadi pale tu itakapohitajika kushushwa aidha kwa uchakavu au kwa tukio maalumu linaoihusu nchi, mfano kupepea nusu mlingoti wakati wa majanga kwa taifa au kuondoka kwa majeshi kutoka kwenye nchi iliyotekwa.

Bendera kama zilivyo alama nyingine za taifa kama vile picha ya Rais aliyeko madarakani au vibendera vya mezani ni ishara ya uhai na uwepo wa taifa kwa kila siku iwe usiku au mchana kwa mwaka mzima. Usiku unapoingia haina maana kuwa serilkali inakwenda kulala, ni tabia iliyojengeka hapa kwetu ya kushusha na kupandisha bendera ifikapo jioni au asubuhi hasa kwa nia ya kufanya gwalide.
 
Serikali inapumzika inaachia vyombo vya ulinzi na usalama

Sent using Jamii Forums mobile app
Jibu zuri kutoka kwa Msamaria mwema. Chukua hili hapa!
Mchana Rais anatawala hadhi saa 12 jioni, ikifika Usiku Jeshi linatawala huku likihakikisha Usalama wa Nchi upo(ndio maana kunakuwepp na CDF). Tatizo lolote likitokea anaulizwa CDF!
 
Kwa hiyo mchana rais anatawala jeshi linalala. Rais akilala jeshi linaamka. Maajabu.
 
Back
Top Bottom