Kilichochangia kuchomwa hiyo bendera ni hiki.
Pale Iringa mjini ( ipogoro) bus stand, kumejengwa mabanda ya kisasa kwa tofali za kileo ( hydrafoam- spelling) ambayo JK aliyafungua na kusifia sana.Mabanda ni mengi sana na mazuri sana,binafsi nimeyaona na kuambiwa moja ya mashirika yetu ya umma yamemwaga pesa pale. Mabanda yale yalijengwa kwa jina la Machinga. Mkandarasi akajenga vizuri sana yakavutia wachoyo wachache,wachoyo hao ambao tayari wameshiba wakayachukua kwa majina ya watu wao ambao hawakustahili(sio chinga) kabisa( kwa maelezo ya wamachinga). Chingas wakakosa/wamekosa kama kawaida. Hii imechangia chingasi hawa kuja juu. Mabanda yapo ila wajanja wamehodhi.
Hii ni moja ya sababu za hao chingas kuchoma ili kitu.