Madilu,
Umenimaliza mzee wangu lakini bado hujafunika kabisa!
kinachomfanya mke huyu kugawa sio chupi na pili kinachokuuma zaidi bado kakibeba mwenyewe, mal;i sii yako mjomba!. Na kile kinachotakiwa na huyo mzinifu wa mkeo sio chupi yake hata akiwa uchi wa nyama mzee bado atafurahia ushindi...hiki ndicho chanzo na utatuzi wa zengwe hili unaanzia hapo sio ktk chupi.
Ndio hao viongozi wa CCM wanavyozidi kufurahia ushindi hadi huko Dodoma kwa sababu tumeshindwa ku attack the real issue...Mzee wangu ukisha fumania mkeo, nguo zake haziwezi kuwa suluhisho kwani fedha zimekwisha teketea, pili wewe kama machinga huwezi kumwambia kitu kuhusu Victoria secret ya mtumba hali mjomba pembeni huagiza toka Ulaya na zikaletwa tena kwa dozen kutokana na kodi yako.
Leo kila mmoja wetu hapa kaganda ktk TV, radio, JF kufahamu nani kaingia na nani nje tena wengine tunaomba jamaa zetu wawe ktk kundi hilo la Chukua Chako Mapema...
Kuchoma bendera ya CCM hakuwezi kubadilisha maamuzi ama maonezi ya hawa viongozi wa manispaa ila unazidi kuwapa sababu ya kuendeleza yale wanayoyafanya. Tumeyaona Kenya na South Afrika (Soweto) miezi michache tu iliyopita.
Kuna wale waliosema tujiulize kuhusu hawa machinga kilichosibu hasa kufikia wao kuchoma bendera hiyo. Kwanza
Kuhusu elimu zao, nadhani tutakubaliana kuwa elimu sio kukaa darasani ila ni matumizi yake ktk fani mbalimbali. Tunapata elimu ili kuweza kuitumia na sio elimu kwa sababu ya kujua kusoma na kuandika. Maamuzi kama haya ni dhahiri yanaonyesha upeo mdogo wa kielimu kifahamu chanzo na tiba ya gonjwa hili la viongozi wetu kutoa kutoa hadi za Uongo.
Maandamano hado ofisi za manispaa na kutinga ktk geti lao, kuwazomea na hata kusababisha wao wasiweze kufanya kazi siku hiyo ni somo kubwa sana kwa viongozi hao.
Mjomba Madilu dawa ya mke anayezini nje ni kumtafutia mkeo mwingne. CUF wapo Chadema wapo na wote hawa wanasubiri kura zenu kuwafanya wake zenu. Ama kama mapenzi yamezidi sana basi fumanizi linaweza kusaidia.. vishindo, mikwara na pengine hata makofi ya haraka haraka...(hilo kuvamia ofisi zao) pamoja na kwamba sio ustaarabu. Kama mkeo hataogopa basi jamaa mme mwenzako anaweza kuogopa na pengine kukomesha mawasiliano.