Bendera kwenye mahoteli zina maana gani?

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,683
8,829
Mahoteli hupeperusha bendera za mataifa mbalimbali. Je bendera hizi zinamaanisha nini?
 
Mahoteli hupeperusha bendera za mataifa mbalimbali. Je bendera hizi zinamaanisha nini?
hata mie mway hua zinanitia hamu ya kutaka kujua umuhimu wa Bendera kiujumla na zilianza wakati gani? katika vita miaka ya kupigana na pinde, mikuki na panga kuna wabeba bendera ambao walikua bize kubebe wakati wote wa mapigano !
 
Mahoteli kupeperusha bendera za mataifa mbalimbali maana yake nikukujulisha kuwa raia kutoka nchi husika ambazo unaona bendera zao zinapeperushwa kwenye hiyo hoteli wamefikia hapo au kwa maana nyingine hoteli husika wana wageni kutoka nchi ambazo unaona bendera ziko nje ya hoteli
 
Sina hakika na hili...kwa maana ito pakiwa na wageni 500 wanaotoka nchi tofauti tofauti tutakuta bendera 500 pale nje....au ww ukienda hotel ya nje ya nchi let's say labla ni uchina au marekan...hoteli utakayo fikia itasimamisha bendera ya tanzanzia...na shaka juu ya hili
 
Hiyo assumption yako uliyoitoa haiwezi kufanya kazi, wao wanaangalia idadi ya wageni walionao toka nchi husika
 
Bendera hizo ni alama kwamba hiyo hoteli ni ya kimataifa. Inakaribisha watu wa mataifa mbalimbali. Bendera chache zinazokuwa zinapeperushwa ni kiwakilishi tu cha mataifa yote hata yale ambayo bendera zake hazipepei hotelini hapo.
 
Kiutaratibu, bendera inawakilisha wageni waliofikia hotel hiyo ni wa kutoka maeneo gani kwa maana ya nchi, ukienda hotel yoyote ile ya kimataifa lazima utaona bendera za namna hiyo zinapeperushwa nje, mifano hai nenda pale kenmpisnki(sina hakika kama jina liko sahihi), Holiday Inn, Roayal palm na mengineyo!
 
Hamna hata mmoja ambye amejibu kwa usahihi........... hebu jaribuni tena!
 
Hamna hata mmoja ambye amejibu kwa usahihi........... hebu jaribuni tena!

Kama wewe ni Mkenya, ukifika hotelini nchini Tanzania let say Holiday Inn, watu hotel ndo watakuuliza umetokea wapi, ukisema umetokea Kenya, bendera ya nchi yako itapandishwa juu kwenye mlingoti kuashiria kwamba katika Hotel hiyo kuna mgeni kutoka Kenya, so mtu akipita tu akiona atajua ahaa hapa kuna Mkenya!

Sasa tumejibu tofauti, tusaidie mkuu!
 
Nope! That is business strategies mkuu............ hizi Hotel especially za nyota tano hulenga zaidi mataifa ambayo wananchi wake huingia nchini mara kwa mara ili kuweza kuwavutia wafikie hapo, lakini pia inapotokea official visit ya kiongozi au hata kundi la wafanyabiashara kutoka taifa fulani kuja nchini, na kufikia katika hoteli hiyo, kama haina bendera ya nchi hiyo katika milingoti yake, basi wataenda kuazima katika ubalozi wa nchi hiyo ili kuweka utambulisho wa ugeni wa taifa hilo, lakini hapo lazima bendera mojawapo itashushwa ili kupisha kupandishwa kwa brndera ya nchi hiyo japo kwa muda........ na ndio maana si rahisi kukuta bendera ya nchi kama Chad!
 
BENDERA ZINAZOWEKWA KWENYE HOTEL NA HASA ZILE ZA NYOTA ZA JUU KABISA, ZILE BENDERA ZINAONESHA KUWA HIYO HOTEL INAPATIKANA HATA KWENYE NCHI YA BENDERA HUSIKA. KWA MFANO UKIONA NJE YA HOTEL KUNA BENDERA YA S.A, USA, KENYA,UK,FRANCE,GERMAN INAMAANA HIYO HOTEL INAPATIKANA HATA KWENYE HIZO NCHI ZINAZOPEPERUSHA BENDERA ZAO NJE YA HIYO HOTEL. HIYO INARAHISISHA HATA KWA WATEJA KUFAHAMU KIRAHISI MATAWI YA HIYO HOTEL NJE YA NCHI. UKIONA NJE KUNA BENDERA 3 INAMAANA HIYO HOTEL INA MATAWI MA3 AU NAYO NI MOJA YA TAWI NA MAKAO MAKUU YANAPATIKANA MOJA KTK NCHI YA BENDERA. ZINAZOPEPERUSHA.
Hata makanisa ni hivyo inamaana hilo kanisa linauhusiano na nchi inayopeperusha hiyo bendera.
NIJUAVYO MIMI HAKUNA KITU AU JAMBO LINALOWEKWA MAHALI PASIPO KUWA NA MAANA YAKE,JAPO HAIJALISHI KAMA HIYO MAANA NI YA MUHIMU AU LA.
 
nnunu!! exellent! namaanisha umeongea exactly maana ya hizo bendera! Mtambuzi tambo zooote!
 
Kiutaratibu, bendera inawakilisha wageni waliofikia hotel hiyo ni wa kutoka maeneo gani kwa maana ya nchi, ukienda hotel yoyote ile ya kimataifa lazima utaona bendera za namna hiyo zinapeperushwa nje, mifano hai nenda pale kenmpisnki(sina hakika kama jina liko sahihi), Holiday Inn, Roayal palm na mengineyo!

Hakuna hizo Hoteli hapa Tanzania.
 
nnunu!! exellent! namaanisha umeongea exactly maana ya hizo bendera! Mtambuzi tambo zooote!

Mmmnh kama hivyo ndivyo basi hotel zingine wanaweka hizo bendera bila kujua maana yake; siamini Kama Lake Tanganyika beach hotel ipo na USA na SA!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom