Benchika kama hataki kuondoka kwa fedheha pale Simba aachie ngazi kabla ya tarehe 20

Black poison The Factor

JF-Expert Member
May 31, 2020
864
1,264
Kiukweli kila nikiwaangalia viongozi wa Simba nyuso zao hazina Nuru tena, imebaki Bora liende tu na kwasasa mzigo mzito upo kwa kocha wao benchika,

Siku ya mechi na singida black star ilibidi abaki uwanjani kwa dakika kadhaa, ukiulizwa kwamba alikua anawaza nini utakua na majibu mengi ambayo hayatatoa jibu straight ni lipi.

Pengine alikua anawaza aachie ngazi, ama kibarua dhidi ya yanga ama hatima ya uwepo wake pale Simba.

Mimi ni yanga lialia ila kiukweli huruma ilinijia kwa hali aliyokua nayo siku ile, hapa ndo nikajua kwamba hakuna kazi ngumu kama kumfundisha mtu mzima ambaye nayeye anaamini kwamba ana akili timamu.

Ukimtazama ahmed ally amefikia hatua ya kusema shabiki wa Simba mwenye roho ngumu aende uwanjani, kweli hata wao wamechoka

Yote kwa yote kama benchika hataki kuondoka Simba kwa fedheha (kufukuzwa) basi aachie ngazi kabla ya mtanange wa tarehe 20.

Hata hivyo derby hua hazitabiriki
 
Kula chuma hiko. Utaikalia kwanza hio ndio mengine yaendelee.
JamiiForums406442391.jpg
 
Mimi nmeshakata tiketi yangu, taifa mapema tu Jmosi kushuhudia mtu akigongwa 5 zingine. Pona ya Simba ni Pacome na yao kutokuwepo ktk hiyo game.
Kupitia michezo yao mitatu iliyopita, sioni kama simba itakuwa na maajabu hata kama hao akina Pacome na Yao hawatakuwepo.

Maana wachezaji wengi wana fatique ya kucheza mechi mfululizo. Labda kama siku hiyo wwchezaji watachomwa sindano za kuiondoa hiyo fatique kwenye miili yao.
 
Kiukweli kila nikiwaangalia viongozi wa Simba nyuso zao hazina Nuru tena, imebaki Bora liende tu na kwasasa mzigo mzito upo kwa kocha wao benchika,

Siku ya mechi na singida black star ilibidi abaki uwanjani kwa dakika kadhaa, ukiulizwa kwamba alikua anawaza nini utakua na majibu mengi ambayo hayatatoa jibu straight ni lipi.

Pengine alikua anawaza aachie ngazi, ama kibarua dhidi ya yanga ama hatima ya uwepo wake pale Simba.

Mimi ni yanga lialia ila kiukweli huruma ilinijia kwa hali aliyokua nayo siku ile, hapa ndo nikajua kwamba hakuna kazi ngumu kama kumfundisha mtu mzima ambaye nayeye anaamini kwamba ana akili timamu.

Ukimtazama ahmed ally amefikia hatua ya kusema shabiki wa Simba mwenye roho ngumu aende uwanjani, kweli hata wao wamechoka

Yote kwa yote kama benchika hataki kuondoka Simba kwa fedheha (kufukuzwa) basi aachie ngazi kabla ya mtanange wa tarehe 20.

Hata hivyo derby hua hazitabiriki
Hawezi kuachia tonge lisifike mdomoni Tena tonge la pili ama la tatu baadae ya kuonja utamu wa mulo
 
Back
Top Bottom