Ben Vs Kikwete

Mafisadi hawakuanza leo,ni kuanzia wakati wa mwalimu mwenyewe.mashirika ya umma yalitafunwa na mafisadi wakati wa Nyerere.Mkapa yeye akaona mradi ayauze akafanya biashara yake.Jk amerithi mambo machafu lakini anajaribu kusafisha nchi.juhudi zake zinaonekana.
 
NATOFAUTIANA KABISA NA WEWE

Mkapa juu ya ubaya wake na wizi wake, na roho mbaya yake lakini amefanya mengi ambayo mazuri. Hii ni nature kwani sisi binaadam hatuna sifa za umalaika. Lazma mtu awe na kitu kibaya watu wapate kumtoa kasoro. Hii ndio Mungu ameumba iwe hivyo!

Mkapa ndie alieanzisha TASAF mafanikio ya TASAF nyote mnayajua na sasa TASAF imeingia awamu ya pili.Kipindi cha Mkapa watu hawakuwa na hali ngumu ya maisha kama sasa. Usalama ulikuwepo japo kwa kiasi ila waliomzunguka walikuwa wanajua "mzee" hatabiriki. Mkapa aliogopwa! Mkapa hakuwa akichekacheka alionyesha kuwa yeye ni kiongozi.

Kikwete.

Kikwete ni kweli ana bahati ya kupendwa sana hilo halipingiki ila ni lazma achukue tahadhari maana graph yake ya kupendwa inashuka kwa kasi sana. Ni mtu wa mzaha mzaha tu wengi waliomzunguka wanaujua udhaifu wake na ndio wanatake advantage hiyo. Mtaona jinsi alivyoshindwa kushughulikia ufisadi kwakuwa ni mtu dhaifu!

Mkapa na Kikwete wana kitu ambacho wana "share"

Wakati Mkapa ni Rais Kikwete alikuwa Waziri mwenye dhamana ya ushirikiano wa kimataifa. Kama waziri Kikwete alikuwa ndanii ya baraza la mawaziri lililoamua mambo yote yaliyofanywa kipindi cha miaka kumi ya mkapa kama mikataba iliyonyonga uchumi wetu. Kumbukeni kwenye kikao cha bunge wiki iliyomalizika Nazir Karamagi alisema uamuzi wa kuongezewa TICTS mkataba ulitokana na baraza la mawaziri na ana barua aliyoandikiwa kuwa (wao) serikali kupitia baraza la mawaziri na JK akiwamo wameridhia kuongeza muda kwa kampuni hiyo wa miaka 15.

Sasa hapa kama Kikwete angekuwa anaona wanayoyafanya ni madudu angewashauri wenziwe akajenga hoja wakakubaliana na wakaacha kufanya waliyoyafanya!

Kikwete ameshiriki kila lililofanywa na Serikali ya awamu ya tatu kwani yeye pia alikuwa mmoja wa watendaji wakuu wa Serikali!

Kikwete ameshiriki kuuza nyumba za serikali na yeye amenunua yake mtaa wa ursno regent estate. JK ameshiriki kuuza mashirika ya umma kwa bei chee. Ameshiriki mikataba ya TICTS,AGREKO,SONGAS,IPTL na mingine mibaya!

JK anajua kila baya lililofanyika na Serikali hii.

Sioni mantiki kwa wale wanaomtetea maana hata hoja hii ilivyo letwa imeletwa kiujanja janja hivi especia mchangiaji niliye m-coute. Anataka tumtukuze Kikwete kutupa uhuru wa kutoa maoni!

Kama nyie mtampa Kikwete ahsante kwa kuwapa uhuru wa kutoa maoni mie siwezi kufanya hivyo. Siwezi kufanya hivyo kwasababu najua ni haki yangu kikatiba. Hutakiwi umshukuru mtu kwa kukupa haki yako hata siku moja kwani huo ni utumwa na ukoloni ndani ya nchi iliyo huru.

Mkapa kachukua Kiwira coal mining na Kikwete na rafiki zake wamechukua pesa BoT na Tanesco kupitia Richmond.

Mkapa na Kikwete ni alpha na omega.

Wasalaam,


Hata kama binadaamusio malaika lakini lazima binadamu dhamiri yako ikusute japo kidogo unapofanya madhambi ya kutisha. Wanyama tu wana-conscience. kimsingi nilikuwa namwona Mkapa kama mkombozi wa Tanzania baada ya kuipokea nchi ikiwa katika hali mbaya toka mikononi mwa Mohamed Ally, oh sorry Ally Hassan Mwinyi. Lakini kwa kuangalia tu yeye na wafuasi wake walivyojichotea mafedha namwona hana maana kabisa. Mzee Mwinyi amewahi kutamka kuwa anachofanya Mkapa, kubinafsisha na kuuza mashirika ya umma, mtu yeyote angeweza kufanya (hata ambaye elimu yake kuhusu uchumi ni ile aliyoipata kutoka elimu ya msingi). Alikuwa sahihi kitu kimoja tu, kwamba kuuza ni rahisi kuliko kununua/ku-create. Lakini kumbe ndani yake Ben alikuwa anajiwekea hazina duniani. Oh huyu mtu mbinafsi!!!!! Namwombea hayo mahela yote aweze kuwahonga watakaokuwa geti lu kuingilia mbinguni kama ataweza!! za nini sasa hela zote hizo hapa duniani wakati ataishi miaka isiyozidi sabini???
 
Kwani kuzima nyota ya mwenzako ndo kunafanya nyota ing'ae?

Woote walishiriki kuiangamiza nchi. Kama serikali ya sasa itajifanya kuwashughulikia mafisadi basi ni sawa na mbwa kula matapishi yake mwenyewe.

Kuna ndugu mmoja maetoa mchango wake kuhusu ufisadi kuanza huko nyuma na alizungumzia kuwa kilichomtoa Mrema katika system ni kusema ukweli. Kama alisema ukweli basi ilikuwa kweli dhidi ya Mwinyi. Na je, ni nini kilifanyika kumuwajibisha mzee huyu?

Ama ni kwa kuwa yeye alitoa ruhusa kila mwenye jino atafune chake? Hiyo biashara aliyofanya akiwa ikulu nani amefaidika nayo? Nchi aliiacha ikiwa utupu na hapakuwa na pa kuanzia ili angalau kutengeneza mitaji na ama kuendesha serikali. Zaidi kilichofanyika ni namna ya kupata pesa na kuendesha nchi. Je, serikali ya Bwana Ben ilikuwa na sababu gani kuingia mikataba mibovu ambayo inalipunguzia taifa mapato?

Lakini na Bwana Kikwete alikuwa wapi kipindi hicho cha mauzo ya mali za wananchi? Kinachinifurahisha ni kuruhusu kesi dhidi ya aliyekuwa balozi wa Italia kwa manunuzi mabaya ya nyumba ama ofisi ya balozi huko ughaibuni. Suala lenyewe limefanyika chini ya wizara yake, yeye hakuona inakwaje ashughulikiwe ndugu huyo mmoja na fimbo isimkumbe na waziri wake?
 
Kuna JK aliyofanya Mazuri siwezi kubisha lakini katurudisha 10000miles nyuma wakati mkapa pamoja na kutafuna nchi alikuwa anatupeleka next level


And where is this Dude!

Hommmieeeeeeeeeeee !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Next level!!!!!!!!!!!!!!! ulikwiya?
 
Mafisadi hawakuanza leo,ni kuanzia wakati wa mwalimu mwenyewe.mashirika ya umma yalitafunwa na mafisadi wakati wa Nyerere.Mkapa yeye akaona mradi ayauze akafanya biashara yake.Jk amerithi mambo machafu lakini anajaribu kusafisha nchi.juhudi zake zinaonekana.

hapo kwenye red, unaweza kueleza japo vitu vitano tu alivyofanya ambavyo havikuwa planned and artectured na mkapa?
 
Back
Top Bottom