Greenwhich
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 1,337
- 968
Ni takribani miezi miwili tangu mwanachama wa Chadema Ben Saanane aibuke katika vyombo vya habari hususan mitandao mbalimbali ya kijamii na kile kinachoitwa kundi la Masalia ndani ya Chadema ambalo lilikuwa linatumiwa na CCM kuhujumu chama na ambalo lilikuwa pia na malengo ya kutukana na kukashifu viongozi wakuu wa chama kupitia mitandao ya kijamii.
Kati ya waliotajwa kuasisi na kuunda kundi hilo ni Mtela Mwampamba aliyegombea ubunge jimbo la Mbozi na Juliana Shonza
aliyekuwa Makamu Mwenyekiti BAVICHA.Ben alitoa ushahidi mbalimbali ambao kwa kiasi kikubwa ulisaidia BAVICHA kuwafukuza uanachama Mtela Mwampamba na Juliana Shonza.
Hata hivyo wako watu wachache waliolaumu na kupinga uamuzi huo na kusema vijana hao wameonewa.Hata hivyo leo yametimia baada ya vijana hao kurudi CCM na kuporomosha kila aina ya kashfa kwa chama cha Chadema na viongozi wake.
Ni ukweli ulio wazi kwamba aliyosema Ben Saanane leo yametimia pale aliposema vijana hao walikuwa wamepanga kuleta madhara makubwa ndani ya chama na hatimaye kutimkia CCM.Kutokana na ushirikiano wa Ben Saanane hatimaye vijana hawa walifukuzwa kwa hiyo hawakukamilisha mpango waliopanga kuhujumu chama.
Kuna wengine walipinga kitendo cha Ben Saanane kumhusisha Zitto Kabwe na vijana hawa mapandikizi hata hivyo vyovyote iwavyo Zitto Kabwe amebadilika sana tokea tuhuma dhidi yake zitolewe na yuko pamoja na chama katika shughuli za kukijenga tofauti na siku za nyuma.Ilikuwa ni nadra sana Zitto kushiriki maandamano ya Chadema kama alivyoungana na viongozi wenzie Jumapili ya kumlaani Spika wa bunge Zitto alishangiliwa sana Temeke Mwisho Jumapili pale alipomkaribisha Dr Slaa na kusema huyu ni Rais wa watu ambaye hakutangazwa mshindi Ni wazi mwenendo wa Zitto umebadilishwa na ujasiri wa Ben Saanane.
Bila unafiki wala upendeleo Chadema wanapaswa kumpongeza Ben Saanane kwa kazi kubwa aliyofanya kuwatifua Mapandikizi ya CCM na kuleta umoja na mshikamano ndani ya Chadema.

Last edited by a moderator: