Haya ni maelezo kutoka ukurasa wa Facebook wa fans wake.
Furahia Valentine’s Day ukiwa na umpendaye kwa burudani nzuri ya muziki toka kwa mkali wa R&B Belle 9 atakaekuimbia nyimbo zake zote kali zitakazopigwa na live band huku ukipata chakula na vinywaji vilivyoandaliwa kuendana na mahadhi ya siku hii ambayo
itaongozwa na mshindi wa Big Brother Africa Idris Sultan pia ukisindikizwa na Millian, Bella & The Band.
Utapata wasaa maalum wa wewe kumchagulia au kumuimbia wimbo yule umpendaye.
Yote haya ni siku ya Jumamosi 13.02.2016 kuanzia saa mbili usiku katika ukumbi wa Sky Nightlife kwa kiingilio cha Sh 20,000 kawaida na Sh 50,000 VIP ambapo wapendanao 20 wa kwanza kuwasili watapata chupa ya champagne bure. Wahi tiketi yako sasa.