Beki 3 na mama mwenye Nyumba

Beki 3 na mama mwenye Nyumba

mzanzibara-

Senior Member
Joined
Feb 3, 2014
Posts
179
Reaction score
59
Msichana wa kazi alitaka mama mwenye nyumba ampandishie mshahara..... Mama mwenye nyumba akamwambia msichana ampe sababu tatu za kutaka kupandishiwa mshahara.

Msichana: Napika vizuri kuliko wewe.

Mama: Nani kakuambia?
Msichana: Baba kaniambia.

Mama: ok. Sababu ya pili?
Msichana: Napasi nguo vizuri kuliko wewe

Mama: Nani kakuambia na hili?

Msichana: Baba pia kaniambia

Mama: ok, na sababu ya tatu?

Msichana: Najitahidi kitandani kuliko wewe.

(Hapa mama kaonekana kutaka kujua zaidi na akawa tayari kujiandaa kumrukia akate kichwa cha binti mara moja)

Mama: Mume wangu kakuambia na hili pia?

Msichana: Hapana ni Shamba boy kaniambia mimi najitahidi kitandani kuliko wewe.

Mama: Tafadhali punguza sauti baba yako asisikie. Nitakupandishia mshahara wako mara tatu.......

*****************************************************************************
 
Mtoto mdogo alimfuata baba yake na kumuliza, " Nini maana ya SIASA?"Baba akajibu, " Mwanangu ngoja nijaribu kujibu kwa mfano huu: mimi natafuta fedha ya matumizi, hivyo niite mimi BEPARI
Mama yako yeye anasimamia matumizi ya fedha, hivyo mwite SERIKALI.-
Mimi na mama yako tuko kwa ajili ya kuwapa nyie mahitaji yenu hivyo nyinyi twawaita WATU.
Dada wa kazi yeye anatusaidia kazi za hapa ndani hivyo tunamwita MFANYAKAZI.
Na mdogo wako ambaye ni mdogo tunamwita FURSA ZA BAADAYE"

Haya sasa mwanangu hebu fikiri na uone kama ina kupa jibu la kuridhisha....-Kijana akaondoka na kwenda kulala huku akifikiri na kuyatafakari maneno aliyoyasema baba.Baadae usiku ule, akasikia mtoto ambaye ni mdogo wake akiwa analia hivyo akaamua kuamka na kwenda kumcheki.Akaona mtoto kajinyea na kajipaka uchafu huo huku akilia kuashiria anahitaji msaada.

Akaamua aende chumbani kwa baba na mama, akamshuhudia mama akiwa peke yake kalala usingizi mzito na hana habari yoyote.
Hakutaka kumwamsha akaona angemsumbua mama, akarudi na kwenda shumba cha dada wa kazi na kuona mlango umefungwa.-Akachungulia kupitia tundu la ufunguo na kuona dada wa kazi akiwa na baba wanafanya yao.-Akakata tamaa na kurudi kulala bila ya kuwa na msaada wowote kwa mdogo wake.

Siku ya pili mtoto akamwambia baba, "sasa nafikiri naelewa maana halisi ya SIASA."Baba akasema, " safi sana mtoto mzuri, haya sasa niambie kwa maneno yako maana halisi ya siasa kwa jinsi ulivyoitafakari"

Mtoto akajibu, "Ni hivi, wakati BEPARI anamyanyasa na kumtumia vibaya MFANYAKAZI, SERIKALI imelala usingizi mzito, Na WATU hawasikilizwi shida zao huku FURSA ZA BAADAYE zikiwa zimesusiwa kwenye uchafu bila msaada.
Baba kidogo azimie.
wewe ungejibu vipi?
 
haaaaaahaaaaaa...umenikumbusha mdau,kuna hii mashosti wawili mama papito na mama usipitwe hawa kila wakikutana huwa nikupeana visa,mikasa na umbea..lakini siku hiyo mama papito uzalendo umemshinda yamemfika shingoni baada ya kumfumania mumewe na kimada,mambo yalikuwa hivi

mama papito:shoga moja haikai mbili haikai
mama usipitwe:kulikoni shogaangu..??
mama papito:sijui hata nikwambia je mwenzangu,ni metendwa nataka unishauri
mama usipitwe:we nambie hivohivo shogaangu,hebu kwanza kaa utilie unieleze kwa kirefu
mama papito:mwenzio sinimemfuma baba papito na kimada gesti hausi ya pale jirani yuko na shoga yetu huyu jeni
yaaan nimechoka mimi ,nimechokaaa nakwambia staki tena..!!!
mama usipitwe:mwenzangu,kama nihayo nakushauri omba taraka yako shogaa mapemaaaaa...!
mama papito:weeeee..ya nini hiyo taraka..!!wakati nilivo mfuma na hausigeli alininunulia samsung note3
kwataarifa yako fumanizi hili lazima aninunulie verosa
mama usipitwe:mweeeeeeeeehhh...hayaaa
 
Mtoto mdogo alimfuata baba yake na kumuliza, " Nini maana ya SIASA?"Baba akajibu, " Mwanangu ngoja nijaribu kujibu kwa mfano huu: mimi natafuta fedha ya matumizi, hivyo niite mimi BEPARI
Mama yako yeye anasimamia matumizi ya fedha, hivyo mwite SERIKALI.-
Mimi na mama yako tuko kwa ajili ya kuwapa nyie mahitaji yenu hivyo nyinyi twawaita WATU.
Dada wa kazi yeye anatusaidia kazi za hapa ndani hivyo tunamwita MFANYAKAZI.
Na mdogo wako ambaye ni mdogo tunamwita FURSA ZA BAADAYE"

Haya sasa mwanangu hebu fikiri na uone kama ina kupa jibu la kuridhisha....-Kijana akaondoka na kwenda kulala huku akifikiri na kuyatafakari maneno aliyoyasema baba.Baadae usiku ule, akasikia mtoto ambaye ni mdogo wake akiwa analia hivyo akaamua kuamka na kwenda kumcheki.Akaona mtoto kajinyea na kajipaka uchafu huo huku akilia kuashiria anahitaji msaada.

Akaamua aende chumbani kwa baba na mama, akamshuhudia mama akiwa peke yake kalala usingizi mzito na hana habari yoyote.
Hakutaka kumwamsha akaona angemsumbua mama, akarudi na kwenda shumba cha dada wa kazi na kuona mlango umefungwa.-Akachungulia kupitia tundu la ufunguo na kuona dada wa kazi akiwa na baba wanafanya yao.-Akakata tamaa na kurudi kulala bila ya kuwa na msaada wowote kwa mdogo wake.

Siku ya pili mtoto akamwambia baba, "sasa nafikiri naelewa maana halisi ya SIASA."Baba akasema, " safi sana mtoto mzuri, haya sasa niambie kwa maneno yako maana halisi ya siasa kwa jinsi ulivyoitafakari"

Mtoto akajibu, "Ni hivi, wakati BEPARI anamyanyasa na kumtumia vibaya MFANYAKAZI, SERIKALI imelala usingizi mzito, Na WATU hawasikilizwi shida zao huku FURSA ZA BAADAYE zikiwa zimesusiwa kwenye uchafu bila msaada.
Baba kidogo azimie.
wewe ungejibu vipi?

Iko vizuri sana, its creative.
 
Back
Top Bottom