Beka Ibrozama afunika kwenye cover wimbo wa Adele "Hello"

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Nimeangalia na kusikiliza cover kibao za wimbo wa Hello wa Msanii nguli wa Uingereza 'Adele'. Leo nimeangalia na kusikiliza cover ya msanii wa kibongo Beka nimegundua dogo ana kipaji si haba.

Amedai kuwa hajui lugha ya kiingereza ila maajabu aliyofanya makubwa sana, ameweza kutamka maneno vizuri kwa asilimia 90.

Beka ameingia kwenye Top 10 yangu ya walioimba cover ya wimbo huu maarufu kwa sasa.

Hongera sana msanii Beka.

Since it was released last year, Hello by Adele has become one of the most successful songs of our times. Hello which was the first single from the British singer's 25 album which has so far sold more than eight million copies in the US alone, has attracted a thousands of covers from singers all over the world including Africa.
Famous singers including Joe Thomas, Celine Dion and Demi Lovato have also sung their own rendition of this song. But could this be the best cover sang by an African singer yet?

Beka Ibrozama is one of the most talented singers in Tanzania. He is nicknamed ‘Fundi’ which means Expert because of his powerhouse voice and ability to hit the higher notes of the most difficult songs ever sung. The most interesting fact about this kid is that he cannot speak English, but able to sing this beautiful song in a way that no one can even imagine that fact. “That’s the truth that I don’t know English but I have sung an English song with my capacity and I believe I have shown a great level of competence considering that I didn’t even know what I was singing. I believe this is an amazing talent that God has given me,” he says. “I love Adele, and it’s a fact that Hello is one of the best song of this decade, I believe you will love my rendition, enjoy.”

Muimbaji mahiri wa nchini Tanzania, Beka Ibrozama ameachia video ya cover ya wimbo maarufu wa msanii wa Uingereza, Adele ‘Hello’ uliopo kwenye albamu yake 25 iliyotoka November 20 mwaka jana. Hello umekuwa wimbo maarufu zaidi kutoka mwaka 2015 huku hadi sasa video yake ikiwa imeangaliwa kwa zaidi ya mara milioni 940 kwenye mtandao wa Youtube huku albamu yake ‘25’ ikiuza nakala milioni 7.4 ndani ya sita tu nchini Marekani.

Hello umekuwa wimbo uliofanyiwa cover nyingi zaidi hadi sasa na wasanii kutoka mataifa mbalimbali wakiwemo wakongwe kama vile Joe Thomas, Celine Dion, Demi Lovato na wengine. Beka anadai aliamua kuwa mmoja wa waimbaji waliofanya cover za wimbo huo ili kuwaonesha wapenzi wa muziki duniani uwezo mkubwa alionao kiuimbaji.

“Ni wimbo fulani mgumu sana, ni wimbo wenye sauti za juu, una melody nzuri na ili uweze kupita kwenye hizo njia ni lazima kidogo uwe unajua muziki,” anasema Beka. Anasema pamoja Hello kuwa na sauti ngumu kuweza kuzimudu, alipata tabu katika kuweza kutamka vizuri matamshi ya Kiingereza kutokana na kuwa lugha asiyoijua kabisa.

“Ukweli uko hivyo kwamba sijui Kiingereza lakini nimeimba wimbo wa Kiingereza kwa uwezo wangu naamini nimefanya kwa uwezo mkubwa ukizingatia kuwa sijui hata nilichokuwa nakiimba, naamini ni kipaji cha ajabu sana Mungu amenipa,” anasisitiza. “Kwahiyo watu hata wakisikia baadhi ya maneno sijayatamka kama Muingereza mwenyewe anavyoyatamka, wajue kuwe sijui hicho kitu ila nimejitahidi kwa uwezo wangu.”

Msanii huyo ambaye kwa sasa hupenda kujiita Fundi, anadai kuwa jina hilo amepewa kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kuchezea sauti kama anavyotaka na uwezo wa kuimba aina zote za muziki kwa umahiri mkubwa.

“Nina vitu vingi sana vikubwa watu hawajavigundua kutoka kwangu.”

Amesema mwaka 2016 utakuwa mwaka muhimu kwake sababu amedhamiria kuuthibitishia ulimwengu kuwa yeye ni dhahabu iliyoanguka kwenye tope na inahitaji sikio la mtu anayejua muziki kuiona, kuikota na kuiutumia vyema ili kuitangaza Tanzania kwa kipaji kikubwa alichobarikiwa na mwenyezi Mungu.

Beka alijipatia umaarufu mkubwa kwa wimbo wake ‘Natumaini Remix’ aliouandika kwa ufundi mkubwa huku akitumia kuunganisha mantiki wa wimbo huo kwa kutumia majina na nyimbo za wasanii mbalimbali.

ITAZAME VIDEO HIYO HAPO CHINI

...mkuu bado sana, this does not even come closer to the best from Tanzania let alone Africa [Hint: Huyu fundi amecheza na sauti i.e., sio ya kwake].
Sikiliza hii kutoka kwa majirani zetu hapo, by Dela [Hint: Kaifanya kwa kiswahili, na jaribu sikiliza sauti mkuu..noma]
 
Huyu Adele nyimbo zake zote za kulialia kuhusu x-boyfriend tu. Sijui hana other subjects kwenye maisha yake.
 
Nimeangalia na kusikiliza cover kibao za wimbo wa Hello wa Msanii nguli wa Uingereza 'Adele'. Leo nimeangalia na kusikiliza cover ya msanii wa kibongo Beka nimegundua dogo ana kipaji si haba.

Amedai kuwa hajui lugha ya kiingereza ila maajabu aliyofanya makubwa sana, ameweza kutamka maneno vizuri kwa asilimia 90.

Beka ameingia kwenye Top 10 yangu ya walioimba cover ya wimbo huu maarufu kwa sasa.

Hongera sana msanii Beka.

we hujui mziki, unaongea kwa hurka. cover hiyo imejaa Echo, imejaa "Dry Auto-tune"
 
...mkuu bado sana, this does not even come closer to the best from Tanzania let alone Africa [Hint: Huyu fundi amecheza na sauti i.e., sio ya kwake].
Sikiliza hii kutoka kwa majirani zetu hapo, by Dela [Hint: Kaifanya kwa kiswahili, na jaribu sikiliza sauti mkuu..noma]

Mkuu hata ww hujui mziki, huyu cover yake imejaa Echo na Dry Auto Tune. Isikilize tena sauti ya Adele...pale Producer hata haangaiki kuficha aibu nyingi.
 
Mkuu hata ww hujui mziki, huyu cover yake imejaa Echo na Dry Auto Tune. Isikilize tena sauti ya Adele...pale Producer hata haangaiki kuficha aibu nyingi.

...ni kweli sijui mziki kiivyo kwa maana ya technicalities, lakini kwa usikilizaji tu najua..na feeling yangu ni kuwa rendition ya Beka haina ubora huo kama tunavyotaka kuaminishwa, ni ten times better hata ya huyu Dela (with a twist kuwa kaifanya kwa kiswahili)
 
Katika cover zote za huu wimbo, cover ninayoikubali na ambayo huwa naisikiliza na kuitazama kuliko original version ni ya Joe Thomas. Cover ya huyu dogo inapwaya sana sijaikubali kiivo bora hata ya yule mkenya alieimba kwa kiswahili.

ila jamaa ana sura ngumu...anyway
 
Huyu Adele nyimbo zake zote za kulialia kuhusu x-boyfriend tu. Sijui hana other subjects kwenye maisha yake.
Anakuambia anaimba kile kinachomtokea kwenye real life....ka hajawahi pendwa aimbe nini sasa???????
Skelewuuu Skelewuuu au
 
Katika cover zote za huu wimbo, cover ninayoikubali na ambayo huwa naisikiliza na kuitazama kuliko original version ni ya Joe Thomas. Cover ya huyu dogo inapwaya sana sijaikubali kiivo bora hata ya yule mkenya alieimba kwa kiswahili.

Adele akasome tena....hapa kafunikwa aise
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Binafsi, namkubali sana Beka kama msanii mwenye kipaji hata ukiweka kando huu wimbo.
 
Nimeangalia na kusikiliza cover kibao za wimbo wa Hello wa Msanii nguli wa Uingereza 'Adele'. Leo nimeangalia na kusikiliza cover ya msanii wa kibongo Beka nimegundua dogo ana kipaji si haba.

Amedai kuwa hajui lugha ya kiingereza ila maajabu aliyofanya makubwa sana, ameweza kutamka maneno vizuri kwa asilimia 90.

Beka ameingia kwenye Top 10 yangu ya walioimba cover ya wimbo huu maarufu kwa sasa.

Hongera sana msanii Beka.

beka amefanya kazi nzuri sana Ameonyesha kipaji mngu azidishide bonge la cover
 
Ni kwasababu Dela ni Mkenya Beka ni mtanzania thus anakuwa bado sana?, Autotune ulioiskia mi ipi hapo? Hiyo ni sauti ya original na hata reverb na echo unayoiskia haimodify sauti bali ni technique za sound engineering tu. JF muwe Great Thinkers na sio Great Discouragers

...mkuu bado sana, this does not even come closer to the best from Tanzania let alone Africa [Hint: Huyu fundi amecheza na sauti i.e., sio ya kwake].
Sikiliza hii kutoka kwa majirani zetu hapo, by Dela [Hint: Kaifanya kwa kiswahili, na jaribu sikiliza sauti mkuu..noma]
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Asante kwa kuuona ukweli. Muziki unaujua ww

Nimeangalia na kusikiliza cover kibao za wimbo wa Hello wa Msanii nguli wa Uingereza 'Adele'. Leo nimeangalia na kusikiliza cover ya msanii wa kibongo Beka nimegundua dogo ana kipaji si haba.

Amedai kuwa hajui lugha ya kiingereza ila maajabu aliyofanya makubwa sana, ameweza kutamka maneno vizuri kwa asilimia 90.

Beka ameingia kwenye Top 10 yangu ya walioimba cover ya wimbo huu maarufu kwa sasa.

Hongera sana msanii Beka.

Ni kwasababu Dela ni Mkenya Beka ni mtanzania thus anakuwa bado sana?, Autotune ulioiskia mi ipi hapo? Hiyo ni sauti ya original na hata reverb na echo unayoiskia haimodify sauti bali ni technique za sound engineering tu. JF muwe Great Thinkers na sio Great Discouragers

Mimi mwenyewe mtanzania, ila ukweli ndio kama huo niliokwambia hapo. Hii rendition ya Beka ni ya kawaida...haijafika kiwango hicho unachokisema wewe kuwa the "best from Africa".

Akichukulia kama ni kumdiscourage then atakuwa hafikirii vizuri, hii ni kumpa ukweli ambao unatakiwa ummotivate zaidi. Kuna swala la lugha pia ambalo sijalizungumza maana kama vipi si angeifanya kwa kiswahili ili tuone msanii haswa? Marehemu Ngwair alishawahi kuirudi nyimbo moja enzi hizo kwa kiswahili chake mwenyewe cha mtaani unakumbuka ilivyobamba?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom