Beijing yaipita New York kwa mabilionea

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
739
484
Beijing yaipita New York kwa mabilionea
160124104404_cn_china_chunyun_beijing_high_speed_640x360_epa_nocredit.jpg
Image copyright EPA
Image caption: Jiji la Beijing lina mabilionea 100
Jiji la Beijing limelipita jiji la New York katika kuwa na idadi kubwa ya mabilionea, ripoti mpya ya shirika la Hurun kutoka Uchina inasema.

Mabilionea 100 kwa sasa wanaishi katika jiji hilo kuu la Uchina, wakilinganishwa na mabilionea 95 wanaoishi New York, ripoti hiyo inasema.

Jiji la Shanghai, kitovu cha kiuchumi nchini Uchina, limo nambari tano.

Hurun, shirika ambalo hufuatilia utajiri na huduma za kifahari nchini Uchina, limekuwa likitoa orodha ya matajiri wa kupindukia duniani kwa miaka mitano iliyopita, wakihesabu mabilionea kwa dola za Kimarekani.

151030092008_wang_jianlin_624x351_getty.jpg
Image copyright Getty
Image caption: Wang Jianlin ndiye mtu tajiri zaidi Uchina, kwa mujibu wa Burun
Waligundua kwamba Beijing imepata mabilionea 32 wapya tangu mwaka jana, na kuiwezesha kupita New York ambayo ilipokea mabilionea wanne wapya pekee.

Kwa ujumla, Uchina pia imeipita Marekani kwa kuwa na mabilionea wengi zaidi duniani.

Hata hivyo Wamarekani bado wanatawala katika orodha ya mabilionea 10 wakuu zaidi katika orodha hiyo ya Hurun.

Uchina ina mabilionea 568 baada ya kuongeza mabilionea 90 nayo Marekani ina mabilionea 535.

150203041137_cn_hurun_logo_640x360_afp.jpg
Image copyrightAFP
Image caption: Uchina sasa ina mabilionea wengi kuliko Marekani
Mabilionea wa Uchina kwa pamoja wana utajiri wa $1.4 trilioni (£1.01 trilioni), ambao ni sawa na mapato ya jumla ya Australia.

Mtu tajiri zaidi Uchina bado ni Wang Jianlin, ambaye utajiri wake unakadiriwa kuwa $26bn (£18.8bn).

Mmarekani tajiri zaidi ni Bill Gates aliye na $80bn, akifuatwa na Warren Buffett mwenye utajiri wa $68bn.

Nambari tatu inakaliwa na tajiri wa mavazi kutoka Uhispania Amancio Ortega aliye na utajiri wa $64bn. Ripoti hiyo ya Hurun inasema kwa sasa kuna mabilionea 2,188 duniani, ambayo ni rekodi mpya.
 
Hivi kwanini China yenye watu 1.35bilion inapenda jilinganisha na watu 330mil? Karibia robo
 
Hivi kwanini China yenye watu 1.35bilion inapenda jilinganisha na watu 330mil? Karibia robo
Kuwa na wingi wa mabilionea sio hoja sana...hoja ni kwamba hao 100 wanamiliki net worth kiasi gan mmoja mmoja?..saban unaeza kuta kat ya hao may be 50 wan miliki $1bil kila mmoja wakat wenzao wa NY mau be mmoja anamiliki 10 bil na kuendelea...sasa apo huwez jisifia kivile
 
Hivi kwanini China yenye watu 1.35bilion inapenda jilinganisha na watu 330mil? Karibia robo
Wanalinganisha watu wachache wenye hela! Hata wewe ungekuwa na hela kufikia us1b wagekuweka kwenye list mabilionea zaid ya 2000
 
Kuwa na wingi wa mabilionea sio hoja sana...hoja ni kwamba hao 100 wanamiliki net worth kiasi gan mmoja mmoja?..saban unaeza kuta kat ya hao may be 50 wan miliki $1bil kila mmoja wakat wenzao wa NY mau be mmoja anamiliki 10 bil na kuendelea...sasa apo huwez jisifia kivile

Yani unapenda kuishobokea marekani weye!sijui umelishwa nini tu! Dah angalia watakuoa
 
Back
Top Bottom