MTZ 255Dar
JF-Expert Member
- Sep 25, 2018
- 1,152
- 3,967
Makampuni ya China yameanza kulikimbia soko la Urusi kutokana na Vikwazo vya Kiuchumi ambavyo Urusi imewekewa na nchi za Magharibi.
Makampuni hayo Ni Pamoja na Lenovo, Xiaomi, Alibaba, Exim Bank, Huawei na Oppo. Baada ya Makampuni mengi ya Magharibi kufunga biashara zake Nchini Urusi baada ya Nchi hiyo kuivamia Ukraine, Makampuni ya China yaliendelea kubaki kwenye Soko la Urusi.
Wataalamu wa Kiuchumi wanadai kwamba, Makampuni hayo Binafsi yanaweza kuwa hayajaogopa vikwazo vya Magharibi Kama wengi wanavyofikilia, Bali Uchumi wa Urusi unaelekea kuwa Closed economy ambapo Biashara Nyingi Nchini Urusi hazitaweza kupata fedha za kigeni kuyalipa Makampuni ya Nje hasa China.
Pia wengi wanadadisi na kusema,Kwa kuwa Makampuni mengi ya China hasa ya Simu na Computer yanategemea Chip sets kutoka Marekani, Ulaya, Korea, Japan na Taiwan ambazo nchi zote Hizo zimeiwekea Urusi vikwazo vya Kiuchumi, Basi Makampuni hayo huenda yanaogopa Kupigwa mafuruku kupata vifaa hivyo muhimu kutoka kwenye Nchi za Magharibi kwa kuendelea kwao kukaa Nchini Urusi.