Beijing, China: Bunge laanza rasmi, Makadirio ya Uchumi yaonekana ngumu kutabiriwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,981
Kwa mara ya kwanza katika kupindi cha miaka 22, mkutano unafanyika mwezi Mei badala ya mwezi Machi. Hii ni kutokana na serikali kujikitiza kwenye juhudi za kupambana na virusi vya Corona, na kuhakikisha usalama wa afya ya wabunge. Mkutano umefanyika sasa kwa kuwa kuna uhakika wabunge wote watakuwa salama.

Kwa mara ya kwanza Serikali ya China haijaweka makadirio ya ongezeko la uchumi (GDP) kwa mwaka huu kutokana na sintofahamu ya mwelekeo wa hali ya uchumi wa dunia.Kutokana na hali ya isiyokadiriwa ya maambukizi ya COVID-19 na hali ya kiuchumi na kibiashara duniani, maendeleo ya China yanakabiliwa na sintofahamu nyingi.

Kutokana na hali hii serikali ya China haijaweka malengo maalum la ongezeko la uchumi kwa mwaka huu.Ripoti pia imesisitiza kuwa China itaendelea nahatua ya kuzuia na kudhibiti virusi vya Corona katika kipindi kijacho, na kushughulikia vizurimaendeleo ya kiuchumi na kijamii.

======

BB675FEE-7ADC-48BB-A8D5-FF45896C27BE.jpeg

F79B6413-8816-48CA-8258-0DE3A627799A.jpeg

3E0E9BF2-6818-46B2-8E4A-9BE256C9A04C.jpeg

EFF06D44-280B-4EAF-9245-E6E3D01EBDFF.jpeg

C535577F-166A-4515-B477-52D6D1010FCD.jpeg


Mkutano wa Bunge la Umma la China umefunguliwa leo mjini Beijing, baada ya kuahirishwa kwa miezi miwili kutokana a virusi vya Corona. Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama cha Kikomunisti cha China na wa serikali, pamoja na wajumbe 2,897 wa Bunge la Umma la China wamehudhuria ufunguzi wa mkutano huo. Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 22 kwa mkutano huu kuahirishwa kutoka mwezi Machi hadi mwezi Mei kutokana na COVID-19.

Kubwa lililofanyika kwenye ufunguzi wa mkutano, ni Waziri Mkuu wa China Bw. Li Keqiang kutoa ripoti ya utendaji wa serikali katika mwaka uliopita, na ripoti ya mpango ya kazi za serikali kwa mwaka unaokuja.

Alitaja baadhi ya mambo yak

1. Mwaka jana pato la taifa la China liliongezeka kwa asilimia 6.1 na kufikia dola trilioni 13.9 za kimarekani, nafasi milioni 13.52 za ajira ziliongezeka, na idadi ya watu wenye hali duni sana kiuchumi vijijini ikipungua kwa watu milioni 11.09.

2. Mwaka huu serikali itahakikisha inawaondoa watu wote kutoka kwenye umasikini na kutokomeza umaskini, kuongeza juhudi za kusaidia vijiji maskini vilivyobaki.

3. China mwaka huu itaendelea kutekeleza sera chochezi za kifedha na sera tulivu za sarafu. China itadumisha kiwango chake cha ubadilishanaji wa fedha kuwa tulivu.

4. Serikali inapanga kuendeleza kupunguza mzigo wa kodi na gharama za uzalishaji, na kuzisaidia kampuni ndogondogo na wafanyabiashara binafsi kukabiliana na matatizo kwenye shughuli zao.

5. Serikali itahimiza uzalishaji viwandani na maendeleo ya shughuli mpya zinazojitokeza. Na itaendeleza zaidi mtandao wa Internet na kuhimiza teknolojia ya akili bandia, kwa kimombo “Artificial Intelligence (AI)”.

6. Serikali itaweka mkazo katika kuunga mkono ujenzi wa miundo mbinu ya aina mpya, kupanua matumizi ya teknolojia ya 5G.

7. Serikali itaweka kipaumbele kuleta utulivu wasoko la ajira na kulinda maisha ya watu, kushinda vita dhidi ya umasikini na kujitahidi kufikia lengo la kukamilisha kazi ya ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote mwaka huu.

8. Serikali itapunguza ukiritimba kwenye sekta zilizozuiliwa kwa uwekezaji kutoka nje kuingia kwenye soko la China, kuweka orodha ya sekta zinazozuiliwa kwa huduma na biashara nje ya nchi, na kuyapatia maeneo ya majaribio ya biashara huria haki zaidi ya kujiamulia juu ya mageuzi na kufungua mlango.

9. Serikali itaimarisha utaratibu wa afya ya umma, kwa kutoa msisitizo kwenye kujali maisha, kufanya mageuzi ya mfumo wa kukinga na kudhibiti magonjwa, kuboresha mfumo wa utoaji wa tahadhari na taarifa kuhusu magonjwa ya kuambukiza, kuendelea kutoa habari kwa uwazi kuhusu maambukizi.

10. Serikali itaunga mkono maendeleo ya uchumi wa Hong Kong na Macau, kuboresha maisha ya umma, kuunganisha maendeleo ya maeneo hayo katika mpango wa ujumla wa maendeleo ya taifa.
 
Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang amesema nchi hiyo haitajiwekea lengo la ukuaji wa uchumi mwaka huu kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID19

Amesema wamefikia uamuzi huo kwasababu China itakabiliwa na mambo kadhaa ambayo ni ngumu kutabiri kutokana na kutokuwa na uhakika kuhusu janga la Corona na mazingira ya kiuchumi na biashara duniani

Amesema nchi hiyo inatarajia kukabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi na kutoweka lengo la ukuaji uchumi kutaiwezesha Serikali kuelekeza nguvu zaidi katika kufikia uiamara na usalama

Waziri Mkuu amesema CoronaVirus ni changamoto kubwa zaidi ya afya ya umma ambayo China imewahi kukutana nayo

======

China will not set a specific target for economic growth this year, said Chinese Premier Li Keqiang at the 13th National People's Congress in Beijing.

The NPC, China's top legislature, opened its third session on Friday morning.
The decision not to set a target is "because our country will face some factors that are difficult to predict in its development due to the great uncertainty regarding the Covid-19 pandemic and the world economic and trade environment," said Li, the country's second-in-command.
Not setting a specific target for economic growth would enable the government to focus more on achieving stability and security, he said.

Li added that China is expected to face great uncertain economic challenges following the pandemic, and that coronavirus was "the fastest spreading, most extensive, and most challenging public health emergency China has encountered since the founding of the People's Republic."

Some context: The world's second largest economy has taken a huge hit from the virus, as lockdown measures brought much of the country to a halt from late January to March.

China's gross domestic product shrunk 6.8% in the first quarter this year -- the worst plunge since quarterly records began in 1992.

The Chinese Communist Party has pledged to double the size of the economy from 2010 by the end of 2020 -- a goal that could be difficult to reach in the fallout of the pandemic, as growth had already slowed due to a prolonged trade war with the United States.

CNN
 
Back
Top Bottom