Ukienda ofisini kwao, hakuna gharama zitakazoongezeka. Na chance ya kupunguziwa ni kubwa. Kuna watu niliwaelekeza wakaenda Jumatatu wiki iliyopita, walikuwa wanataka kuagiza Toyota Rush. Walipunguziwa dola 700 kwenye bei inayoonekana mtandaoni. Binafsi nilipunguziwa kutoka $5127 hadi $4660. Kama ni mtu usiyetaka usumbufu, lipia gharama za gari, inspection, hadi clearance. Wkt wa kulipa ushuru watakutafuta ulipie, baada ya hapo watakutafuta ukachukue gari lako.