Bei za magari

Zimeshuka au zimepanda?
Zimepanda boss kwa hiyo 300k na Kitu.

-Angalia hapo chini nimekuwekea sample ya gari ya Premio ya 2007 na 2008 kwa before kupanda na after.​

1.Kabla ya kupanda
- Gari ya 2008
IMG_2847.png


-Gari ya 2007
IMG_2846.png


2.Baada ya Kupanda
-Gari ya 2007
IMG_2845.png

-Gari ya 2008
IMG_2844.png
 
Japan Kuna makampuni mengi yanayouza used car, haya mnayoyafaham ni kwasababu yamejijengea umaarufu na kujikuta hata bei yanauza yanavyotaka lakini Kwa Yale yanayochipukia huitaji mzunguko was haraka wa pesa hivyo kuuza Kwa bei ndogo.
Pia sio kila muda ni mzuri Kwa kuagiza gari muda mzuri ni mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka huko minada ya magari Japan hushamiri magari
Pia kabla hujaagiza omba auction sheet
Gari ikianzia grade 3.5 sio mbaya na ikiwa grade R achana nayo
Grade3.5 na grade R mana yake nini hasa unapotaka nunua gari
 
M nmeagiza mwenyewe nmesave karibu 4M

Nakushauri tu,acha uoga mifumo iko very secured
Kama ukiamua kuagiza mwenyewe usiweke mtu kati

Lipa mwenyewe bank kila kitu
Ikifika wacheki clearing agent Trimex company
Wakutolew gari unawalipa laki 2 zao gharama zingine zote lipa mwenyewe wakutumie tu control number!

NOTE:mimi nliagiza SBT nlipokea gari in excellent condition hata mimi sikutarajia pia ilikuja na service card+mafuta nusu tank ya kuanzia🥹

Mpaka leo haijasumbua
KUAGIZA MWENYEWE INAWEZEKANA MAANA HAKIKA JAMAA WAKO SECURED SANA WANAKUTUMIA NA PRE FORMER INVOICE ILI UKALIPIE BANK NA MALIPO HASA YANAFANYIKA BANK
 
Mi nimeagiza mwenyewe...
Nikabagain mwenyewe....
Nikalipia kila kitu mwenyewe...
Natarajia kupokea ndinga mwenyewe...
Maana ni yangu mwenyewe....

Shida ya Watanzania wengi ni uoga na kutishana.
Mimi ni wewe labda tunatofautiana kwenye kampuni, mimi niliagiza kupitia autocom.

Watu waache kutishana hizi mambo zinawezekana .
 
Mi nimeagiza mwenyewe...
Nikabagain mwenyewe....
Nikalipia kila kitu mwenyewe...
Natarajia kupokea ndinga mwenyewe...
Maana ni yangu mwenyewe....

Shida ya Watanzania wengi ni uoga na kutishana.
Hongera mkuu mwenyewe kwa kufanya kila kitu mwenyewe
Naamini utauleta mrejesho mwenyewe kutuhamasisha na wengine kufanya kila kitu wenyewe.
Shukran🙏🙏🙏
 
then utamkabidhi agent unayemuamini atakutolea
"agent unayemuamini" utamjuaje na unampata wapi ?

Nishinde kwenye vijiwe vya ma agenti kuwasoma body language au inakuwaje ????

Nilidhani the whole point ni kufanya mchakato wa kitehama na kuondoa biashara za kiswahili za kuamini amini watu. Kama ndo hivyo tumkabidhi kazi dalali tunaemwanini! Might as well.
 
Back
Top Bottom