Bei ya vifaa vya ujenzi ni pasua kichwa, Gharama zimepanda kwa zaidi ya 30% ndani ya miezi 3

Leo hii kujenga nyumba kwa ajili ya makazi ni anasa" kwasababu ya ughari wa materials. Nyumba ya kawaida vyumba vitatu tu inakugharimu zaidi ya 25-30m ikiwa na finishing standard sasa hesabu tu kwa mtumishi wa kawaida wa serikali wa ngazi ya batchelor anayelipwa mshahara wa Tshs. 700,000/- kabla hajakatwa unadhani ataweza kujenga nyumba hii kwa muda gani kama sio mpaka astaafu hajamaliza nyumba hii. Achilia mbali wengi wa watanzania ambao vipato vyao ni unga unga mwana.
 
Kama uchumi wa kati unaombwa na hawa jamaa ndo gharama zake basi bora tungeendelea uchumi wa chini tu, labda kama wametengeneza data ili kuwadanganya mabeberu yao ili yawakopeshe kwa fujo.
 
Materials za kutengeneza hizo nondo, bati na steel materials kwa ujumla zinatoka abroad. That's number one mistake, huwezi kuwa na chuma inazalishwa Tanzania then raw material ya kutengeneza bidhaa za chuma na bati tutegemee kutoka nje.

Kiwanda kama Sitta Steel au Alaf wanategemea kwa % kubwa raw materials kutoka China na Korea huko, kwa usawa huu wa Corona worldwide mzigo unaweza kuchukua hadi 4months haujafika nchini, unategema wao wauzeje baada ya kutengeneza hizo bati, but again hizo structure za kodi kwa sasa sio rafiki hata kidogo.

We still have a mountain to climb!
 
Mkuu hivi Bei ya bati la geti geji 20 na geji 18 zimefika Bei gani sahv
 
Hali ya maisha kwa mtanzania wa kawaida imeendelea kukazwa na kuwa ngumu zaidi kiasi watu kutoona thamani ya uhai na kupuuzia vifo na vitisho vya magonjwa ya mlipuko kama Corona.

Leo nizungumzie gharama za vifaa vya ujenzi ndani ya miezi mitatu iliyopita, mfano bei ya Nondo 12mm kwa hapa Dar kwa mwezi wa 8 ulikua unaweza kupata kwa sh 17,500 - 18,000 lakini kwa sasa bei yake ni kati ya 21,000-22,000.

Bei ya bati la kampuni maarufu ya Alaf 30G zile nyeupe migongo midogo kwa mwezi wa 8 ulikua unaweza kupata kwa Sh 16,000 - 17,000 kwa kila bati kwenye bundle la bati 16 lakini kwa sasa unaweza kupata kwa Sh 21,000-22,000 kwa aina hiyo ya bati.

Kiujumla hali ni mbaya sana katika sekta hii hasa kwa sisi tuliowekeza kwenye hii sekta muda mrefu kwani kila kitu kimepanda bei kwa zaidi ya 30% ndani ya miezi 3.Bei za pipes na chuma kwa madirisha, milango balcony, zote ziko juu. Ni wazi kuna watu wameshindwa kuwajibika katika majukumu yao na watumie busara watupishe.
Hapa umeweka na ushahidi kabisa safi sana
 
Jengeni mnaoweza kujenga mkimaliza tu Jaffo nae anazitaka hizo nyumba na kodi zake kwa TRA ukishindwa nyumba inapigwa mnada na private corporation zitanunua hizo nyumba na kukupangisha usipo conform na wanachokitaka unafukuzwa fasta
 
tunakumbushana.

ujenzi haujawahi kuwa rahisi.
kama unadhani ni hivyo subiri bei ishuke,utajua hujui.
 
Mkuu hivi Bei ya bati la geti geji 20 na geji 18 zimefika Bei gani sahv
Plate 20G kwa sasa ni 60,000-65000, 18G ni 70,000-75,000. Kumbuka mwezi Oct kabla ya uchaguzi zilikuwa zinauzwa 45,000-50,000 kwa 55,000-60,000.
 
Comrade sidhani kama kutakuwa na bei elekezi kama kodi ya bidhaa imeongezwa na hao wenyewe wenye mamlaka, hapo hakuna msaada kwa maana wakitaka bei elekezi baadhi ya wafanyabiashara wataacha kuuza, sasa matokeo yake bidhaa itakuwa adimu sokoni kwa hiyo bado tutarejea kulekule tulipotoka.
Nimefika kuandika mbinu chafu za wafanyabiashara wa viwanda. Bora tuanze kuagiza Tena maana ukitaka kulinda viwanda vya ndani wao wanatengeneza mtandao wakuzalisha kidogo Kwa kupeana zamu. Hivyo kufanya awepo upungufu wa vitu makusudi
 
Nimefika kuandika mbinu chafu za wafanyabiashara wa viwanda. Bora tuanze kuagiza Tena maana ukitaka kulinda viwanda vya ndani wao wanatengeneza mtandao wakuzalisha kidogo Kwa kupeana zamu. Hivyo kufanya awepo upungufu wa vitu makusudi
Hili nalo linawezekana.
 
January nimenunua 100m roll ya electric cable 1.5 kwa around 90k. Leo ni 140k.

Mitano tena
 
Back
Top Bottom