MAHANJU,
...Tatizo si bei ya sukari. Kipato cha wengi ni kidogo kumudu mahitaji ya muhimu ya kila siku. Challenge kubwa tuliyonayo kama Taifa ni kuinua kipato cha wengi. Ndio maana inaonekana bei ni kubwa. Si kubwa, kama unazingatia gharama za uzalishaji, kodi, usafirishaji, n.k.
...Bei elekezi zina manufaa zaidi kwa bidhaa ambazo ni muhimu katika shughuli za kiuchumi, kama mafuta. Lengo ni kutoathiri shughuli za kiuchumi na maendeleo, kwa kusababisha ongezeko lisilo la lazima, kwenye bei ya bidhaa na huduma -pengine kupelekea mfumuko wa bei- kwa ujumla kwenye uchumi.
...Kwenye bidhaa hizi za mlaji, ukiweka bei elekezi ukakosea kidogo tu, utaharibu soko lote la bidhaa hiyo. Mzalishaji anaweza akaanza kupoteza faida, mfanyabiashara akakosa faida, na hatimae kukaanza kuwapo uhaba kutokana na uzalishaji na biashara kushuka. Tukumbuke enzi ya Ugawaji, na tujifunze.
...Bei za vitu mbalimbali zinalalamikiwa na wananchi, na hasa vipindi vya sikukuu. Ukweli ni kuwa, vipato vya wengi ni vidogo, na hilo ndio tatizo. Sio bei ya bidhaa. Bei nyingi hufuata hali ya soko -demand and supply- na kuna namna ya kuzishusha -in this case, sugar- bila kuweka bei elekezi.