Bei ya maziwa ya unga kupanda

Bei ya maziwa ya unga kupanda

Tatizo lako huoni picha kubwa, look at the big picture, tunachofanya kwa sasa ni kuvunja ile ' vicious cycle'. Tutakapoweka hivi vikwazo ni kwamba watu wengi sasa watahamasika kufuga kisasa (Zero grazing) ili kuweza kuziba pengo kubwa litakalojitokeza (demand ndio asset kubwa iliyopo),kweli mwanzoni tutaumia kwani kutatokea upungufu mkubwa wa maziwa na yalipo yatauza bei kubwa sana ( demand vs supply) na bila shaka kila mti mwenye mtaji atavutiwa sasa kujitosa katika ufugaji bora wa kisasa ( sio wa kienyeji) ambao utazalisha maziwa bora na kwa wingi ili kuzina pengo kwenye soko, kiwango cha supply na demand kikisha stabilize basi bei itashuka na tutakuwa 1.) tumeongeza ajira kwa kiasi kikubwa 2.) Tutakuwa tumeokoa hizo bilionj 160 pesa ya kigeni kuagiza maziwa 3.) Tutaongeza ukusanyaji wa kodi 4.) Tutapunguza utapiamlo kwa watoto 5.) Uchumi kwa ujumla wake utakuwa. Hivi mnawekaga konokono humo vichwani au huwa mnajitoa akili kwa makusudi?
Umeandika kwa mikogo na matusi as if TZ government as shown a road map or atleast succeed revamp one sector which can be taken as example. Hayo makelele na matamko yote ysnayofanywa na hao wanaojinasibu kuwa ni vichaa si mkakati thabiti wa kuijenga na kuinua sector ya ufugaji bali ni virungu tu ili ionekane watu wako shughulini.
Serikali lazima kwanza ihakikishe upatikanaji wa maziwa as raw material kwa kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi/ushirika wa wafugaji kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na kuwapatia mikopo na pembejeo ili kuwavutia hata mtu mmoja mmoja kufuga at a family level. Tunakaa na kujidanganya kwamba maziwa raw ni mengi ilhali processors wanaangaika kupata maziwa. Mashine ndogo tu ya kuproccess UHT inahitaji lita 500,000 kwa siku ili upate faida. We usione akina Azam wanakoroga powder ukafikiri wanapenda, kodi ya kuingiza powder milk sio mchezo.
 
Ndiyo mana bei imepanda
Nilikuwa nanunua 1kg kwa shilingi 12000/=
Sasa nanunua kwa shilingi 14000/=
 
Hivi hii tozo inagusa na maziwa ya watoto (formula)?
 
Hii tozo wala halimnufaishi mfugaji zaidi zaidi wataonufaika na wanaopigia chapuo tozo hii ni Tangafresh, Asas, darfresh labda na azam ambao asilimia kubwa ya malighafi yao ni maziwa ya unga. Na wanaitumia serikali ili kuzuia competition toka nje na kufanya lobbying ili maziwa ya unga wanayoagiza kama raw materials yaondolewe ushuru na yanayokuja ready for consumption ndio yatozwe ushuru na tozo zingiine. So ukweli hapa si kuinua wafugaji bali restrictions kwa importers kwa manufaa ya wachache.
 
Kwanini uagize maziwa toka nje ya nchi ilihali Tz inaongoza kwa kuwa na ng'ombe Afrika? Huoni kama kwa kuagiza maziwa unaua viwanda vya ndani kama vya Azam, Tanga fresh, Dar fresh na wengine? Napendekeza kodi ipandishwe mara 100 zaidi ili kuinua viwanda vya ndani. Ukiimport maziwa pia una export ajira
Tanzania kwa sasa hatuna dairy farms, hivyo uzalishaji unategemea watu binafsi ambao wanazalisha Kiwango ambacho si kikubwa ku sustain kiwanda kwa mwaka mzima, Kwa miezi ya March hadi june maziwa ni mengi sana na yanaharibika kwa sababu hatuna storage facilities na reliable transport kuyatoa yanakozalishwa hadi kiwanda kilipo.Hivyo spoilage ni kubwa sana msimu huo
Lakini baada ya hapo , malisho yanapungua na maziwa yanakosekana kwa kiasi kikubwa
 
Serikali ya Tanzania imeongeza tozo ya kwa zaidi ya asilimia 1,200 na kuzua mjadala kuhusu hatima ya sekta ya maziwa nchini.

> Tozo hiyo ipo katika kanuni zilizotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilipitishwa mwezi Agosti na kuanza kutekelezwa tarehe 1 mwezi huu.

> Awali, waagizaji wa maziwa na bidhaa zake walikuwa wakilipa Shilingi 150 kwa kilo 1 ya maziwa

Lakini sasa tozo hiyo imepanda hadi Shilingi 2,000 ni sawa na ongezeko la asilimia 1,233.
 
ni muhimu kulinda viwanda vya ndani, by the way tuna bidhaa bora za maziwa za ndani kuanzia asas, Iringa na zile toka musoma. they beat us on the package and added flavour
 
Back
Top Bottom