Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,371
- 14,481
- Thread starter
- #21
ningependa kujua lita moja ya diesel au lita 20 zaweza kusaga kilo ngapi!
swali zuri hili,ngoja nitege sikio nisikie jibu lake.
ningependa kujua lita moja ya diesel au lita 20 zaweza kusaga kilo ngapi!
swali zuri hili,ngoja nitege sikio nisikie jibu lake.
Nilifika Cambodia nikakuta wanatumia injini za magari madogo especially Corolla kuendeshea hizi mashine na hata boti za uvuvi.
Mkuu uko Sahihi kabisa, ila kuna kifaa fulan kinaitwa Changer kinahusika na aina hii ya Mota ili iweze kutumika kwa kazi hiyo. Trekta zinatumika sana hasa maeneo ya Wilaya za Magu na Bariadi. Ingawa kwa sasa utumiaji wa Engine ulizotaja haupo kabisa kutokana na Ujio wa Injin za Kichina yaan JD, DF nk ambazo ni rahisi kununua na kuziendesha pia. Kabla ya Ujio wa Injin hizi za kichina kulikuwa na Injini za Mjeruman kama LISTER PETER, DEUTZ nk ambazo zilikua zikiuzwa Mil.. 6 - 12 hivyo hali hii iliwasukuma watu wengi kutumia Injin za Colora, Isuzu, 110 matreketa nk. Lkn kwa sasa injin za mchina hata Lak 6 unapata na unaanzisha kazi ya kusaga.
Wadau kumbukeni kwamba, unapomiliki Mashine ya Kusaga ya Mafuta eneo ambalo halina Umeme fursa kubwa ni UFUAJI WA UMEME. Mota yako ya Kusaga yenye Ukubwa wa HP 20 Inaweza kuzalisha umeme wa kulisha zaidi ya Nyumba/familia 100 kwa matumizi ya kuwasha taa tu. Familia 1 itakulipa Tshs. 10,000 kwa mwezi na wenye Guest watakulipa Tshs 50,000 kwa mwezi. Endapo utakua eneo zuri aina hii ya biashara faida yake kwa mwezi ni zaidi ya Mil. 1 kwa mwezi. Hasa maeneo ya kambi za wachimba madini na Uvuvi ni sehemu sahihi kabisa kuvuna kipato hiki. Lkn pia mota yako inaweza kuvuta maji kutoka ziwani, Mtoni nk na kuyajaza kwenye matenki na kuyasambaza kwa walaji kwa bei mliyokubaliana. Haya yote yanawezekana kwa Mota yako ya Mchina ya Lak 9.5 ambayo utaifanya kadri utakavyo hata kutengeneza gari ya mizigo inakubali tu ni utaalam tu unatumika. Thats why ukienda site za Ujenzi za Wachina utasikia Vigari vyao vinatoa muungurumo, na kwa sasa METL ametumia Injin hizi kutengeneza Bajaj ambazo zinasambaza bidhaa jijin Dsm.
Ashajibu kasema 60 had 80 kulngana na bei yako
umetuelimisha vya kutosha Thank uWadau kwa Uzoefu wangu wa Kufanya biashara nimegundua Kuwa Biashara ambayo ni non mobile yaan iliyotulia sehemu maalum au isiyohamishika ina changamoto chache mno ukilinganisha na ile ya kuhamahama. Kwa biashara ya Mashine changamoto kubwa ni VIPURI FEKI, MGAO WA UMEME na Ubabaishaji wa Wafanyakazi. Zingatia unaponunua Vifaa vya Mashine yako ununue VIFAA GENUINE INGAWA VITAKUA BEI AGHALI LKN UTAFAIDI ZAIDI. mf. Switch ya kuwasha Mashine FEKI INAUZWA LAK 2 Kkoo, Lkn ukienda kwa Dealer wa Vifaa vya MEM ya Uingereza vifaa ambavyo utapewa Grantii ya Miaka 20 hiyo Starter wanauza Lak 4.5
ukijiloga ukanunua starter feki ya lak 2 kwa mwaka itaungua zaidi ya Mara 6 au zaidi so wewe utakua daily ni kwenda kununua spea. Tujitahidi kutafuta vifaa imara. Wenzetu wanasema CHEAP IS EXPENSIVE
Kaka MTEULE MUNGU AKIPE KILALAKHERI KATIKA MAISHA YAKO. samahani naomba unifanyie outline ya kila kitu na bei yake katika mradi huu, kuna jamaa anataka kuanzisha sasa naona kama anataka kunipiga za uso.Bei kwa Injini ya 20 HP ni Ths. 950,000 zinapatikana kwa Wingi mtaa wa India duka la KILIMO BORA.
Ni jambo gani la kuzingatia wakati wa kuchagua huo ukubwa wa hp mf kama ninunue hp 12 au hp 20.Mashine ya Kusaga ama kukoboa ina sehemu mbili. INJINI na KINU.
INJINI / MOTA zinapatikana kwa ukubwa tofauti yaan Horse Power mbalimbali. Eg. HP 12, 15, 20 na kuendelea. Injini nzuri kwa kupiga mzigo na Ulaji mzuri wa Mafuta ni HP 20 bei yake ni 950,000 aina ya Jiang Dong JD, ama DF ama AMEC zote za mchina. Usinunue Lister Peter.
Ukisha nunua Injini unanunua kinu cha Kusaga na kukoboa vinapatikana Sido ama kwa mafundi wa kuchomelea kwa bei ya 500,000-700,000 kutegemea na makubaliano.
Baada ya hapo utasimika mashine yako eneo ulilochagua. Note.... Injini moja inaweza kuvuta vinu viwili katika jengo lako kinachotakiwa ni kutafuta fundi mtaalamu. Ukiwa Dsm Injini zinapatikana Mtaa wa India duka la Jumla la Injini hizo linaitwa KILIMO BORA, AU AGRO METRO. Ukiwa Mwanza duka la Injini lipo Mtaa wa Rwagasore linaitwa SHYMOND.
Endapo utasimika mashine yako kwa usahihi kabisa Kila dumu la Lita ishirini la Diesel faida yake ni Tshs. 60,000 - 80,000 kulingana na bei ya Kusagiaa.
Karibu kwenye biashara isiyo na stress Mkuu.
Ok,nijibu swali hapo juu.Wadau naona kuna Maswali ya Tangu Nov. 2015 bado hayana majibu yaan nilikua sijapitia post za wadau. Huu uzi ni darasa tosha lkn nashangaa Mods wanauficha sana huu Uzi. Kuna maswali ya Mashine za Kukoboa Mpunga, Mashine za Kusaga kuorodhesha mahitaji yoote ntayatolea majibu. Tujikite sana hii biashara haiumiz Kichwa. Tulioko Mbarali, Mpanda, Sumbawanga, Ifakara wekezeni Kujenga Magodown yenye Mashine za kukoboa Mpunga nimefika huko pesa ziko nje nje sana.
Mkuu kama ulikuwa kwenye akili yangu vileMashine ya Kusaga ama kukoboa ina sehemu mbili. INJINI na KINU.