Kiukweli sijawahi kutumia Kinu cha Mchina. Na hata ikitokea nikakinunua hua napeleka karakana za Kibongo nakifanyia modification kwa jinsi itakayonipa faida. Hizo model za Dustless na Noiseless sijaziona.
Note; Kinu kikiwa na muundo unaochelewesha feni kuhamisha unga uliosagwa kwenda kwenye pipa la Oulet ni hasara.
Kinu kikiwa na plate nyembaba/sahani zinazobeba meno/nyundo ni hasara.
Kinu kikiwa chembamba less than inch 6 ni hasara.
Ridges(mf. Kinywani mwako kwa juu kuna matuta pia yamo ndani ya kinu cha mashine) ndani ya kinu chako ndiyo silaha ya kutwanga nafaka hakikisha hizo ridges zinakua hai muda wote. Endapo zitaisha utachomea nondo ama flat bars.
Aidha, Quality ya Unga inategemea na NAMBA YA CHEKECHEO unalotumia. Endapo utatumia chekecheo lenye macho/matundu makubwa Utapata faida kubwa ila mteja atapata unga ambao unachenga nyingi. Endapo utatumia Chekecheo lenye macho madogo means Unga utakua laini sana bila chenga na mteja atafurahia huduma lkn badala ya kusaga debe 1 dkk 6 now kwa chekecheo dogo unaweza tumia dkk 2 zaid. Kikubwa ni kutafuta chekecheo la kati ambalo ni standard. Pia hakikisha kabla ya kuanza kusaga unachunguza Chekecheo ndani ya kinu, endapo lina pancha litoe uzibe kwa Kuchomelea na Gesi ama weka jingine. Pia wakati wa kuweka chekecheo hakikisha Umeikata kwa vipimo sahihi ambavyo haviachi nafasi ya kupitisha chenga, hakikisha umeifitisha kwenye Kinu bila kuachwa mwanya wowote. Zima mota mara moja endapo utasikia chuma ama kitu chochote kisicho nafaka kimeingia ndani ya kinu na kuleta mtafaruku na ufungue mfuniko wa kinu kuchunguza madhara kabla ya kuendelea na huduma.