Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,150
Bei ya mafuta yashuka
na Betty Kangonga
BEI ya mafuta ya petroli na dizeli nchini imeshuka baada ya kutokea mabadiliko katika soko la dunia na kupanda kwa thamani ya shilingi ikilinganishwa na dola ya Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu, inaeleza kwamba bei za rejareja kwa aina zote za mafuta imeshuka ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita.
Taarifa hiyo inaeleza kwamba petroli imeshuka kwa asilimia 3.7), dizel asilimia 4.92 na mafuta ya taa asilimia 6.86; na wafanyabiashara wanatakiwa kuelewa kwamba ni kosa kwa kituo kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja, ilieleza taarifa hiyo.
Aidha, kwa mujibu wa sheria ya mafuta ya mwaka 2008, bei ya bidhaa hizo itaendelea kupangwa na soko. Hivyo mamlaka husika itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei elekezi pamoja na bei ya kikomo. Taarifa hiyo inaeleza zaidi kuwa kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya ushindani ili mradi ziwe chini ya bei ya kikomo ambayo ni asilimia 7.5 ya bei elekezi. Pia inaelekeza mnunuzi kuhakikisha anapata stakabadhi ya malipo inayoonyesha jina la kituo, tarehe na aina ya mafuta aliyonunua na bei kwa lita kwani ndiyo kidhibiti endapo yanajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa kwa bei ya juu kuliko ya kikomo au kuuziwa mafuta yasiyokuwa na kiwango.