Bei ya flame za maduka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bei ya flame za maduka

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by marandu2010, Aug 23, 2010.

 1. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  Najua inategemea frame yenyewe ilivyo,,mahari ilipo na vitu vinginevyo,,kwa kuzingatia hayo naomba kwa wale wenye kujua hili tushirikiane,,maana hivi ndivyo tunavyoendelea kupanua uwanda wa habari(utandawazi) ili ifikie hatua watu tufanye maamuzi mazuri zaidi yalijengwa kwenye msingi wa wingi wa habari..

  Kwa hiyo yeyote mahali hapa mwenye kujua bei za kukodi frame za biashara(maduka) za sehemu mbalimbali nikilenga zaidi sehemu za jijini dar,,namuomba atupashe..

  Natanguliza shukurani zangu wakuu.
   
 2. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwanini unataka kuchoma hayo maduka kwa hiyo 'flame'?

  Au ulimaanisha frame? Rekebisha basi
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu rekebisha kidogo hapo basi.............. I always remember my granny who would never pronounce "z" to him that was always "s" lakini katika maandishi yake sikuwahi kuona hata siku moja ameandika "Kisuisi" badala ya kizuizi au "soo" badala ya zoo.

  Hi nadhani ni madhara ya kufuta fimbo shule ya msingi.

  Sorry mkuu I do not mean to offend.
   
 4. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  nashukuru kwa kunisahihisha wakuu.kwa kuwa mmenielewa naomba mawazo yenu wasomi....
   
 5. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ....sasa wewe unataka nini? mara unataka Mashamba morogoro, mara ufugaji kuku, mara mtaji wa duka la jumla....mzee ndo umepata ngawira ''Kiinua mgongo'' unataka kukizika nini......?
   
 6. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  helo next level,
  zote zipo kwenye category moja ya biashara....sasa hivi niko kwenye hatua ya kukusanya mawazo..siwezi kufanya jambo lolote bila kuwa na idea,,,,wingi wa mawazo siku zote ni kitu kizuri,,,maana unakufanya kuwa selective,,,pia kuwa na mawazo kuhusu biashara mbalimbali kunakusaidia kupunguza risk...(diversification of risk) ,,,isitoshe nia yangu pia habari hizi zijulikane kwa wengine maana naamini si mimi tu ninazohitaji habari hizi bali ni wengi...kwa hiyo kwa kuzianika hapa kwenye public area zitawafaidisha wengi...

  hayo ndiyo malengo yangu mkuu..hata wewe ukitaka kufanya hivyo JAMII FORUMS HAIKUZUII,,unajisaidia wewe mwenyewe kwa upande mmoja lakini kwa upande mwingine unaisaidia jamii..naomba uwe na mtazamo chanya katika hili...

  nadhani tumeelewana katika hilo,,

  asante sana mkuu,,
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hahaha haha ahahah, oooh man! i love JF!!!!!!!!!!!!!
   
 8. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  R na L ni tatizo kubwa sana blaza especial kwenye kiingereza ukiweka R kwenye L and vise versa ndio umeshakoroga kila kitu....
   
 9. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kumbuka:

  Minja/miruzi mingi humpoteza mbwa......
   
 10. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  ni kweli ulivyosema,,,lakini mfanyabiashara yeyote hukumbana na RISK,,na njia muhimu sana ya kupunguza RISK hii ni kuwekeza katika biashara mbalimbali tofautitofauti,,ili mambo yakiharibika kwenye ile,,unakuwa na usalama kwenye biashara nyingine...hatutakiwi kuweka mayai yote katika kapu moja,,,maana likukumbwa na ajali,,tutapoteza mayai yote,,,ila tunatakiwa kuweka mayai katika makapu mengi...hivyo ndivyo ninavyo maanisha mkuu..

  lakini pia ninataka utajili wa habari hizi kwa watu,,,sisi watanzania ama niseme wa africa tuna uhaba wa habari sana,,kwa njia hii ya kuziweka wazi taarifa hizi muhimu kwa wafanyabiashara,,tutakuwa tumeiinua kwa kiasi fulani wafanyabiashara wenye kuzihitaji hizi information ambao ninaamini wapo wengi sana hawayajui haya..ninataka watu watoe mawazo hata kama hazitanisaidia mimi zitamsaidia hamisi,john au mwajuma,,ndivyo maisha yalivyo,,waache watu watoe mawazo yao jamii ielimike..hata wewe pia utapata elimu hapa..au kama unayo katika hili basi itoe kwa uma,,utabarikiwa zaidi.

  namalizia kwa kusema ukitoa mchango wowote,,uwe wa kitu kinachoonekana au hata mawazo,,,ndivyo wewe pia utakavyopewa hata kwa kuzidishiwa,,,nadhani nimeeleweka mkuu..kama bado tutazidi kuwasiliana..

  asante mkuu.
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,483
  Likes Received: 5,867
  Trophy Points: 280
  Huo mtaji weka benki kwanza.....tuonane baada ya November 5....otherwise utapata majibu ya ajabu sana hapa
   
 12. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  kwa nini unasema hivyo mkuu??? anyway nakushukuru
   
 13. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tunaenda nje ya mada unnecessarily!
  Kama unajua bei za frame za maduka popote ulipo ndani ya jiji respond to marandu's need!

  Kama hujui, si lazima uchangie...
  (Refer Invicible's signature)

  Kwa nnavyofahamu bei za frame hupangwa kutokana na location, traffic flow, ukubwa wa eneo, uimara wa chumba chenyewe, etc.
  Kwa hiyo unaweza kuwa specific ni chumba cha ukubwa gani unahitaji ili wadau waweze kuchangia. Vile vile unaweza kutoa vidokezo vya maeneo unayodhani unaweza kufungua hiyo biashara, mfano g/mboto, msasani, sinza, kimara, ubungo etc. Aidha unaweza kusema kama unataka cha barabarani (kwenye Highway) au mitaani [Hapo nna refer traffic flow].

  So Marandu2010, you can rephrase you question ili uwe specific a bit, wadau waweze kukusaidia.
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,483
  Likes Received: 5,867
  Trophy Points: 280
  Kwa sasa wanaFJ wako busy na siasa...just angalia idadi ya threads za siasa
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kuna mzee wangu huwa anasema muda wa kutafuta pesa ni kipindi cha ujanani ukistaafu usitegemee kama unaweza tafuta pesa zaidi zaidi unazipoteza, huyu hakujiwekea msingi mzuri kipindi cha ujana sasa hivi arudi kijijini tu awe analima huku akipumnzika lasivyo mmmh! hawezi ligi na vijana huko k.koo au sinza au migomigo n.k
   
 16. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  kaka mimi ni kijana tu,nina miaka 25 tu..ninatafuta habari ambazo ninaamini zitanisaidia,,kama alivyo sema mkuu hapo juu,,kama hauna kitu kizuri cha kuchangia,,unasoma tu,sio lazima uandike labda uwe na jambo la msingi,,hebu pitia forums za kizungu halafu uone kama kuna mambo unayofanya..

  any way ninajua,kwa kusema hayo utakuwa umejifunza kitu.

  asante kaka.
   
 17. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  okey,nimekupata kaka,,lakini tusisahau haya mambo,,tusije tukalala njaa.
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kitu nilikuwa nacho ndo maana nikachangia ungeweka wazi hapo juu kuwa wewe nikijana unataka labda kufanya biashara watu tungekusaidia lakini huweki wazi lakini kama unataka fremu k.koo bei yake inalala kuanzia laki 4-6,7 inategemea na mtaa ukizunguka maeneo ya sinza unakamuliwa kuanzia laki 2-4 na kwendelea inategemea position ya fremu pamoja na biashara unayo taka kuifanya. Bei hizo ni kwa mwezi malipo unalipa kuanzia miezi kumi na kwendelea wachache wanapokea miezi 6 lakini wengi wanakwepa usumbufu wa kusumbuana kodi wanakukamua kodi ya mwaka mzima.
   
 19. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #19
  Aug 25, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ningekushauri kwanza uchague biashara kama tatu unazozipenda kisha ukusanya details zinazohusiana na hizo biz (including soko, costing etc). Baada ya hapo ni vema uinvest katika biz kama 2 utakazoziona zimekukuna zaini. I believe in having more that biz opportunities maana hii inakupa nafasi ya kuona ipi inafanya vizuri zaidi na kuiongezea na kukulinda in case biz uliyochagua ukatumbukiza pesa zako zote haifanyi vizuri.
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Aug 25, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,626
  Likes Received: 5,788
  Trophy Points: 280
  SMS
  MKOKO KWENDA 15544 watakusaiidia zaidi hapa wengi wanasikiliza nani anaingia mjengoni DOM
   
Loading...