Bei elekezi ya sukari ni kwa ajili ya watu, walaji au Wasambazaji?

Komba the Great

JF-Expert Member
Apr 25, 2016
338
653
Habari wana jukwaa!!

Leo katika kipindi cha mada moto kinacho rushwa na kituo cha Channel 10, Kulikua na mada isemayo " Sakata la Sukari na uchumi wa Tanzania" Moja ya wachangia mada walio alikwa studio alikua ni mfanyabiashara na msambazaji mkubwa wa sukari hususani katika mkoa wa Dododma Bwana Hidary Hussein Gulamali.

Bwana Gulamali alieleza mengi kuhusiana na upungufu wa sukari nchini, ila kubwa ambalo naomba kueleweshwa kidogo ni suala la Bei elekezi ya sukari. Kwa maelezo ya Gulamali ni kwamba bei elekezi ya sh 1,800/= kwa kilo moja ya sukari ni kwa ajili ya wasambazaji, na akatoa mfano kuwa yeye sukari yake anayo uza Mkoani Dodoma ni shilingi 2,000/= kwa kilo moja. Gulamali alidai kuwa yeye kama mfanya biashara hawezi akanunua sukari kwa bei ya 1,800/= na kisha kuiuza kwa bei hiyo hiyo. Yaani bei ya jumla ikafanana na ya reja reja.

Kwa uelewa wangu nilikua nafahamu kwamba bei elekezi ya sukari ni kwa ajili ya watumiaji wa mwisho, sasa maelezo ya huyu Bwana Gulamali yamenipa Mkanganyiko.
 
Back
Top Bottom