Beefs/ugomvi na hatma ya mziki

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,908
1,951
Habari za wakati huu ndugu, jamaa na wanabodi wengineo?? Ni imani yangu kuwa sote tu wazima wa afya na tunaendelea vyema na majukumu ya ujenzi wa taifa. Kwa wale ambao hawapo sawa kwa sababu za kibinadamu nawatakieni pole na kuwaombea hali zenu za kiafya, kiakili, kijamii na kiuchumi zikae sawa kama mnavyozitaka ziwe. Amen!

Najua ni usiku sana ila imenipasa niandike na kuuweka uzi huu kwa muda na wakati huu. Kwa wale ambao mtabahatika kuuona mapema ukiwa bado mbichi bahati kwenu. Kwa wale ambao mtachelewa bahati kwenu pia. Na wale ambao hawatauona niwape tu pole zangu!

Nirudi kwenye mada kwa sababu salamu huwa hazina mwisho!
Haina ubishi kuwa sanaa, kwa miaka ya hivi karibuni, nchini Tanzania imethibitisha kukuwa kwa kasi ya ajabu sana haswa sekta ya muziki ukilinganisha na viunga vyote vilivyomo ndani ya sanaa – Naongelea uchoraji, Maigizo ikiwa ni miongoni mwa viunga vingi sana visivyokuwa na kikomo vya sanaa.

Hivyo basi, Muziki umetoa fursa na nafasi za ajira kwa vijana wengi ambao wamejiingiza kwenye muziki kama upenyo wa, kwa lugha ya mtaani, kutoboa. Yaani kila uchao masikio yetu huwa yanakutana na ladha na sauti mpya – baadhi zikiwa mbaya na baadhi zikiwa za kuridhisha tu na zingine zikiwa nzuri na bora - za vipaji na wasanii wapya hadi ikapelekea kuwepo kwa msemo kama Siku hizi kila nyumba ina msanii. Hehe Heeee hatari tupu!

Maajabu ya mziki hayajaishia hapo tu, Mziki huo huo pia umejichotea mashabiki bila kujali umri, rika, jinsia au uewezo wa kiuchumi wa mtu: Utathibitisha hilo kwa instagram post ya hivi karibuni kutoka kwa Mo Dewji alipogusia ishu ya Wasafi Festival. Jambo lililoamsha hisia za wengi kwa sababu kati ya watu kumi ni mmoja tu ndiyo angeweza kukubali kuwa Mo Dewji anafuatilia uwanja wa muziki na
burudani kwa ukaribu kiasi hicho.

Hiyo ndiyo nguvu ya muziki kwa sasa. Zamani ingekuwa kitu cha ajabu sana kwa mtu kama Mo kuongelea muziki na kwa sababu hiyo basi angeitwa mhuni tu. Ukweli ni kwamba nikisema nitaje sifa na faida zote ambazo muziki umezileta na zinaoneka itanichukua nusu ya uhai wangu uliobakia kuzimaliza zote hivyo naomba niende kwenye sifa moja kuu: Mziki umegeuka ukawa biashara.

Ndiyo! Muziki umegeuka ukawa biashara, Sio wa kujifurahisha kama zamani ndiyo maana hata wazee waliokuwa wanapinga hao hao ndiyo mabosi walio nyuma ya matamasha na ishu mbali mbali za wasanii. Watu wanawekeza mamilioni ya pesa kwenye muziki ili wapate mabilioni na inakubali. Hiyo ni lazima ikuambie muziki ni nini kwa sasa! Muziki kwa sasa sio kama ulivyokuwa zamani na hapo ndipo zinapokuja mbinu za kibiashara.

Kama ilivyo kawaida ya biashara yoyote ile, kwenye muziki pia watu wanatumia mbinu za kibiashara ili kutawala soko.! Na hapa zipo mbinu nyingi sana, halali na zisizo halali, ambazo hutumiwa lakini leo nitagusia moja tu ambayo ni BIFU.

BIFU kwa lugha rahisi tutasema ni ugomvi kati ya wasanii. Ugomvi unaweza ukawa ama wa kusukwa ambao kwa jina maarufu maarufu ni KIKI au ni ugomvi wa kweli. Wakati mwingine bifu hutokea kwa sababu ya mashabiki. Kwa upande mmoja ni jambo ambalo linachangamsha gemu wanasema ila kwa upande mwingine wa shilingi ni wazi kuwa bifu zinaweza zikasababisha matokeo mabaya kama kudhalilishana na hata kuwindana na kutoleana uhai.

Kimahusiano pia bifu ni mbaya kwa sababu zinaweka ukomo (boundary) nani afanye kazi na nani na nani asifanye kazi na nani?? Na ukishatenga matabaka ni wazi kuwa umepoteza uhuru wa ubunifu na ushirikiano kati ya wasanii. Wengi wetu ni mashaidi wa madhara ya hizi ugomvi, ambazo huwa baina ya msanii na msanii au msanii na chombo cha habari/wafanyakazi wa kituo husika cha redio na Tv.

Mtazamo wangu mdogo ni kuwa pamoja na hizi gomvi kuwa na faida, ambapo mara nyingi faida hizi huwa ni za muda mfupi tu, bado hasara zilizopo ni kubwa sana na hata mzani unaonesha faida zimezidiwa uzito na hasara na wala haihitaji uwe na degree ya menenjimenti ya msanii ndiyo ugundue hilo.

Kwa lugha nyingine rahisi na inayoeleweka, Bifu zinaua muziki. Si jambo la kuonekana ghafla lakini ukweli ndiyo huo! Taratibu tu madhara ya hizi gomvi yataanza kudhihirika. Kutakuwa na mgawanyiko wa watu na hali itakuwa mbaya na muda utakuwa umekwishaenda ili kurekebisha.

Sisemi kuwa mikwaruzano haitokei. Hapana ila bado nina uhakika wasanii, pamoja na umaarufu wao, bado wanateleza na kukoseana ila si jambo jema kung’ang’ania hisia za kuumizwa na kukosewa moyoni. Ni muda sasa watu wasameheane, na kama bifu ndizo zinasukuma mziki mbele basi ziwe ni mbele ya macho ya mashabiki. Watu wakienda nyuma ya kamera tofauti zao wanaziweka pembeni wanafanya mambo ya msingi!

Ciao adios.
 
Huna uwezo wa kuchambua mziki bwana mdogo

Nenda kaendelee na kazi yako ya kukeketa wanawake

Huu mziki tuachie wenye nao

Shwain
Mziki sio karanga mpaka uchambuliwe, chief. Nina wasi wasi na uwezo wako wa kuelewa mambo! Wakati mwingine ni bora kukaa kimya ili usionekane mjinga.
 
Back
Top Bottom