Sharif,
Bwa bayana kama hii,
Mimi nadhani mtu wa kwanza kupanga FOLENI KUNAKO MALIWATO NI HUYU MSAMBAA Nguruvi3...
Teh teh teh
Hebu mpatie kata ya kujitawazia kabla hajachafua hali ya hewa
Hajat faiza Fox, al maarufu punjab Sing, Shariif Ritz ,Al akly THE BIG SHOW, na Al Alma Mohamed Said. Ahadi ni deni, na huwa sitoi kauli bila kuwa na msingi wa kauli hiyo.
Nipo tayari, nimekusanya makabrasha, panya wameyaparaza kidogo lakini sehemu za MS zipo intact. Ninakuja tuongee. Kabla sijamwaga kinachoitwa takwimu za Mohamed, napenda niwape kionjo kuwa mambo yamekaa uzuri, halafu jioni nawapa data zake. Zipo ili nina udhuru kidogo, nakwenda kuchukua madafu sehemu, jua kali
Niwaonyeshe kuwa Ms kafanya makosa mengi zaidi si ya logic bali ya upotoshaji. Nashangaa mnaposema Hirji ambaye amekiri kukosea mau mau na maji maji ametenda dhambi kuu. Hii ya Mohamed saidi si kuwa ni dhambi tu
- Nilimuuliza Mohamed Said mwaka 2011, kutokana na kauli yake kuwa EAMWS iliuawa na wakatoliki na Nyerere, je ana ushahidi wowote.
Mohamed Saidi akajibu hivi: Ukisoma ukursa huo hakuna mahali paliposema Wakatoliki walishirikiana na Nyerere kuua EAMWS. Hii maana yake ni kuwa Mohamed Said ametunga hadithi kama kawaida, kaiweka kwa lugha nzuri akijua anapotosha. Sikuwa alighafilikiwa kwa maneno, bali alisema maneno yasiyo na ukweli na ukurasa ni shahdi.
Nitaendelea maana niliwaonya kuwa mzee atakaa karibu na uani
Sikuweza kuupload ukurasa, ninao hapa
Niwia radhi Kakangu,
Narakabisha kiduchu...Professor Nguruvi3 ni Mbondei wa Kicheba!
Tafadhali kifurusika, basi watake radhi ndugu zetu wa Kisambaa kwa kuwanasibisha na huyo Nguru wa Kicheba!
Ahsanta sana.
Mkuu kuna vitu vingine viko open kabisa huhitaji kuambiwa ili uelewe au ujue.
EAMWS ilivunjwa na Nyerere na haihitaji elimu ya chuo kikuu kuelewa hilo.
Mkuu kuna vitu vingine viko open kabisa huhitaji kuambiwa ili uelewe au ujue.
EAMWS ilivunjwa na Nyerere na haihitaji elimu ya chuo kikuu kuelewa hilo.
Usiishie tu kusema vitu vipo open. Ingalikuwa ni vyema ukaja na facts za kukusuport kwamba EAMWS ilivunjwa na Nyerere. Lete vivid evidences usikurupuke.
Punguza mihemko mkuu hapa tunajadili kitaalam kwa facts, sio kilevi otherwise na wewe ubaki mshabiki.
Kama ni mwaandishi wa habari BASI NI MAJANGA HAYO kwa jamii.
Mtu wa namna hii mwenye dhima ya KUIILIMISHA JAMII, na KUIHABARISHA jamii mambo ya kweli bila CHUKI wala Ushabiki anaandika bila kufanya utafiti japo kiduchu.
Inna Lillahi wainna ilaihi rajihunna.
Naona shule uliyosoma wewe imekufundisha ujinga zaidi na kasi ya ujinga kwa kwenda mbele
Basi umepitwa na mengi Mkuu.
Huu sio mnaksha wa kwanza kufanywa humu JF kuhusu masuala kama haya,
Kma hujui sema ujuzwe usiishie kumshambulia mwenzako kwa ghilba na chuki zako.
Wanabarza,
Kuna mtu hapa yeye kaamua kuwa Launcelot Gobbo,
Ikiwa hamjui huyu ni nani aingie "Merchant of Venice," William Shakespeare.
Ananikejeli "name calling" ati mimi ni Mzee wa Boston.
Ugomvi hauko kwenye uzee.
By the way leo nimetimiza miaka 63.
Alhamdulilah.
Ugomvi uko hapo kwenye, "Boston."
Sasa namuongezea mji mwingine na atizame hii picha:
Hapo juu nipo UN Geneva.
Hiyo picha ni mashuhuri inaitwa "Broken Leg Chair."
Akipenda sasa na aniite Mzee wa Geneva au UN Geneva
au vyovyote vile.
Tutandendelea hivi In Sha Allah kila akitoa jina na mimi nampa mji mpya.
Nimepata kumuonya nikamwambia husda ni maradhi mabaya ya nafsi.
Mnakasha umenoga Faiza anadarsisha,
Mashaallah.
Angekuwa mwanamme ningempiga kilemba.
Kwa kuwa ni mama yetu namvisha ushungi wa hariri.
Allah amuongozee ilm na amjaalie umri tawil.
Ni kweli banian mbaya kiatu chake dawa.
Huyu ndio mwasisi wa TANU, baba wa taifa letu Mwl JK Nyerere aliyemwezesha ata Mohammed Said kwenda shule aloitaifisha akafute tongotongo. Bila hivyo Sydney, ata Boston angeisikia kwenye bomba.
Usiishie tu kusema vitu vipo open. Ingalikuwa ni vyema ukaja na facts za kukusuport kwamba EAMWS ilivunjwa na Nyerere. Lete vivid evidences usikurupuke.
Punguza mihemko mkuu hapa tunajadili kitaalam kwa facts, sio kilevi otherwise na wewe ubaki mshabiki.
Huu ni upotoshaji mwingine wa Mohamed Said. Kama kunaanyebisha kuwa si upotoshaji basi aje hapa tuongee naye. MS alishakubali kuwaalitetereka, sasa nasubiri dagaa Ndugu zangu, mumefungua pandora box,nitahangaika na MS machweo na mawio
thanks kaka, i still respect youSadoliki,
"It is the early bird who gets the worm."
Usiishie tu kusema vitu vipo open. Ingalikuwa ni vyema ukaja na facts za kukusuport kwamba EAMWS ilivunjwa na Nyerere. Lete vivid evidences usikurupuke.
Punguza mihemko mkuu hapa tunajadili kitaalam kwa facts, sio kilevi otherwise na wewe ubaki mshabiki.
Hebu tupe zako japo kiduchu basi, naona unahororoja tu bila kuwa na chochote zaidi ya porojo.
hakuna kitu kibaya kama uwongo, kwani hata mimi ni mngoni, mama yangu kasoma kichwele, babu yangu alikuwa medical supertendent sewa haji (ocean road) kuanzia mwaka 1948, na kuna vitu vitatu ambavyo ni uwongo mtupu, kwanza kuna historia kubwa sana ya wakristo kwenye kupigania uhuru, pamoja na michango ya hela na vitumbua ya babu na bibi zetu, hata mission quarter kwenyewe kuna wazee wengi ambao walishiriki kwa nafasi zao , kwani ni eneo amablo wakristo wengi walikuwepo. hili kama linatakiwa kunadikwa litaandikwa kwani watu wako canada , uingereza na hata tanzania wanakumbuka vitu vingi, pili wangoni ni accomplinces wa vita vya maji maji, kwa matazamo wangu ni kama babu zangu waliingia kichwa kichwa vita vilivyoanzia kilwa na maeneo ya liwale has kutokana na mpango wa wajerumani kutaka kulima karanga na pamba, uwongo huu mnaoleta leo unakinai na haulipeleki taifa hili mbele, nimesoma shule hapa dsm na kwa macho yangu nimeona watoto wa kike wakiisilamu waki tolewa shuleni na baba zao kwenda kuolewa, na wengine waume kwa wake kukatazwa kwenda shule kwani "mtalishwa nguruwe" leo miaka hamsini lawama zimetoka bila hata kuangalia waliokataa kusoma kwa hiyari yao ni % ngapi na wanaonewa kwa utashi wa wakristo ni % ngapi, other waise nchi hii tunaipeleka kubaya. you may think you know everything, but dont be surprised tukikuambia you know nothing
Prof Ngongo.Mkuu Nguruvi3 ikiwa African Assocition kilianzishwa na Bwana Abdulwahid Sykes mwaka 1929 kumbukumbu zangu zinaonyesha wakati huo alikuwa na miaka 5 tu je hili liliwezakana vipi ?.Kweli nimeamini Ustadhi Mohamed Said yupo daraja ya juu ya uongo.
naamini wakati umefika, bahati mbaya itachukua muda lakini tutafanya juhudi kubwa kuanza kuweka vitu sawa, najua wakati mwing umepita lakini archives ziko, wazee wachache wapo, watoto wasikivu na simulizi wapo. Lakini natoa angalizo ambalo lina methali moja , its an early bird who enjoy the fruits, Historia ya ku repeat inakuwa na matatizo makubwa sana ni heri kusahihisha historia iliyopo kulioko kuanza kufanya review ya mambo ya miaka ya hamsini au arobaini, hatari zake na athari zake wakati mwingine huwa hazifutiki.
mimi mohammed ni kaka yangu sana kwa umri, elimu na ufikiri, lakini bado mimi hoja yangu iko pale pale, huwezi kuringa na maisha ya mfumo kristo na upande wa pili unaulanni mfumo huo huo nyumbani, mimi naona huu ni unafiki wa fikira unaokuja na dini, nasema dini siyo kisomo, kama picha hii ingekuwa saudia au yemen, au misri, kweli ningekubali kuwa huo mfumo kristo unamatatizo, mimi kwa kweli nashindwa, na ninashindwa kwa sababu mara zote wenzangu hawaja niconvince kuwa utawala wa wakristo na wazungu ni mbaya kiivyo, wao hawakai arabuni au nchi zenye uislamu wa kutukuta, na wakaringa kuwa oneni uislamu huo, imagine utajiri waote saudia, hata wakimbizi wa kiisilamu hawaendi. leo vita iko somalia, sudan nchi ya kiisalamu haina vita , lakini wasomali waote wanakimbilia kenya, tanzania , southa africa na kutafuta njia ya kwenda sweden , norway nk, siyo njia ya kwenda saudia. same na vita vya syria, wote italy, uingereza, ujerumani, saudia ata, hawataki, lakini kucha wakristo na wazungu wabaya, makafiri nk. mimi nilikuwa na kaka yangu marehemu sasa mungu amrehemu, yeye alikuwa engineer wa kutukuta, na akakaa sweden miaka ya 70, na akaajiriwa na kampuni ya pripps, hii kampuni ndiyo ilikuwa imepewa tenda ya kutengeneza mecca, mind you wa kristo ndiyo walifanya kazi hiyo , majengo , tiling, ablution facilities , air conditioning , sanitation nk, lakini kutwa hawa makafiri , hawa makafiri. ahsanteni, picha mumeiona kaka yangu yuko boston, kamkumbuka sana dada yake na anamlaani kwa nguvu zote mwanamke wa kizungu, ambaye baba na babu zake wametngeneza mazingara ya kumhifadhi, shukurani ya punda , mateke. hongera kaka, keep it up