Beating the Drum on One Side: Confusing the People on Both Sides

Lusungo,
Aliyeleta suala la Dr. Mwanjisi si mimi.
Soma post ya nyuma utaona hilo.

Mimi nimemjibu kuwa hapana haja ya kueleza habri zake.
Nahisi na wewe unakijua kisa cha huyu mzalendo.

Mkuu sio kwa hoja hiyo tu laa....
Muda mrefu Sana umekuwa ukijaribu kuchimbua haya mambo kwa undani na kujaribu kuifuta historia adhimu ya Nyerere ktk ukombozi Wa nchi hii dhumuni ni nini?

Unaamsha Sana hisia za udini kitu ambacho kwa MTU aliyestaarabika si vizuri kupigia upatu.
 
Ndiyo nini hicho? nilichokuwekea nyekundu.

Hebu fata hicho ulichokinukuu uone kamjibu nani na kaulizwa nini. Wacha kudandia treni kwa mbele, utaumia.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Si imeeleweka shida yako nini?
 

= kibla

Hebu tuoneshe hizo post alizo "refute"?
 

FF,
Nina umri karibia miaka 10 hivi.

Niko Kinondoni kwa bibi yangu Mwantum biti Rajab Mwinyimgeni.
Allah amrehemu.

Ni usiku tumetandika mkeka nje ya kibanda chake cha "full suit."

Wajukuu tuko pale anatuhadithia khabari za Hayati Bwana siku za likizo
shule zimefungwa wakati wa kwenda kwa bibi kula pepeta na
bwimbwi.

Huyu ni babu yangu Sheikh Mohamed Mvamila.

Bibi yangu anampamba marehemu mumewe anasema,"Basi Hayati Bwana
kashika kitabu anasomesha na watu wamemzunguka wanamsikiliza... tumehama
Mkamba tumekwenda Musoma huko kaanzisha zawia babu yenu anasomesha huko..."

Hii ilikuwa baada ya Vita Kuu ya Kwanza.

Nikisikia maneno yale mwili ulikuwa ukinisisimka kwani huyu ni babu yangu
Maalim Mohamed Mvamila anasifiwa kwa ilm...na mimi nimepewa jina lake.

Ahsante dada yangu FF umenipeleka mbali sana.

Mwenyezi Mungu awakunjulie makaburi yao wazee wetu walituwekea misingi
ya kuupenda Uislam na ayajaze nuru.
 
Pata darsa kiduchu hapa chini.
Ritz, naona ama umenogewa na ngano za Mohamed Said hadi zinaanza kutia kichefu chefu au wewe ni moja katika wanaomeza simulizi za barazani bila kuhoji. Kwako hadithi haina tofauti na ukweli.
Mwalimu Nyerere alipofika Dar es Salaam kwa mara ya kwanza mwaka wa 1952 kama mwalimu wa shule ya St. Francis' College, Pugu hakuna mtu aliyekuwa anamjua au kupata kusikia habari zake katika ulingo wa siasa.
Huu ni uongo ambao kama tu ungekuwa na kumbukumbu kidogo hungethubutu kuuandika humu JF kwani uliwahi kuletwa awali lakini ikagundulika ni simulizi tu kama za mgahawani. Mwalimu alikuwa ni Kiongozi wa TAA mkoani Tabora miaka mingi tu kabla ya huo mwaka 1952.
Kassela Bantu ambaye alikuwa akijuana na Nyerere kwa siku nyingi alimchukua Nyerere kwa Abdulwahid Sykes kumtambulisha.
Kama kuna mtu Dar es Salaam alikuwa hamjui Mwalimu, basi huyo mtu hakujua harakati zozote zilizokuwa zikifanyika nchini Tanganyika nje ya Dar es Salaam. Katika mkutano wa kitaifa uliofanyika kabla jimboni Tabora uliohudhuriwa na viongozi wa kitaifa wa TAA Mwalimu alikutana na wawakilishi kutoka sehemu mbali mbali nchini na Dar akiwamo Dossa Aziz na wengineo. Abdulwahid Sykes wakati huo labda alikuwa akijulikana tu kama mtoto wa baba, Klyst Sykes, na hakuwa na wadhifa wowote ndani ya TAA.
Wakati ule Abdulwahid alikuwa Rais wa TAA.
Hii ilikuwa baada ya mapinduzi ya vijana kuutwaa uongozi wa TAA na Dr. Vedasto Kyaruzi kuchaguliwa kuwa Raisi wake wa kwanza na Abdulwahid Sykes katibu. Abdulwahid Sykes hakuwahi kuchaguliwa hata mara moja kuwa Raisi wa TAA, alikuja kukaimu tu kwa muda hiyo nafasi baada ya Raisi wake, Dr. Kyaruzi kuhamishiwa mikoani na wakoloni.
Nyerere mara moja akajiunga na baraza la siasa lililokuwa likifanyika Mtaa wa Mbaruku nyumbani kwa Dossa.
Ni wajumbe na viongozi wa TAA Dar es Salaam waliomuomba Mwalimu kujiunga na baraza hilo kwa sababu hakuwepo mtu aliyekuwa na ujasiri, elimu, uwezo na sifa ambaye angeweza kuiongoza TAA katika mabadiliko ya kuigeuza chama cha siasa.
Ikawa kila Jumapili Nyerere anakuja kutoka Pugu kuja kumtembelea Dossa.
Mwalimu alikuwa akifuatwa huko Pugu na kuna baadhi ya mikutano iliyofanyika huko huko wakimshawishi akubali kuwa kiongozi wao.
Ilikuwa katika baraza hii ndipo Nyerere alipokutana na wanasiasa wengi wa wakati ule kama Ramadhani Mashado Plantan aliyekuwa anamiliki gazeti lililokuwa likijulikana kama Zuhra, John Rupia, Dunstan Omari, Zuberi Mtemvu na wanasiasa wengine.
Hapana, wanasiasa wengi alishakutana nao kabla ya kwenda masomoni Uingereza, Dossa Aziz akiwa mojawao. Labda useme alikutana na viongozi wakazi wa mji ambao hawakuwahi kutoka nje ya Dar es Salaam kwa sababu mbali mbali; hapo itaeleweka.
Fikra za Nyerere za kudai uhuru zilisikika kwa mara ya kwanza kupitia kalamu ya Mashado Plantan na gazeti lake la Zuhra lililokuwa likitoka kila siku ya Ijumaa.
Mwalimu alileta changamoto na fikra mpya ndani ya TAA na hapo ndipo sauti za kudai uhuru zikaanza kusikika kupitia magazeti kama Zuhura na kadhalika.
Fikra za Nyerere ziliingiza msisimko mpya katika baraza lile na haukuchukua muda mwaka 1953 uongozi wa ndani ukampendekeza agombee urais wa TAA.
Miezi sita tu toka ajiunge na TAA Dar es Salaam alichaguliwa kuwa kiongozi wake mkuu akimbwaga Abdulwahid Sykes aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo naye kujitosa kugombea.

Ritz, unapoambiwa jambo na wewe jipe fikra kidogo siyo unameza tu, hebu jiulize; huyu mtu ambaye hakuna aliyemfahamu anasafiri hadi Dar, anasema katoka Pugu, anakuta watu wamejipanga wanakiendesha TAA wakiwa na mipango lukuki, anatambulishwa na mtu moja na baada ya muda mfupi wanamkabidhi chama chao cha TAA walichokianzisha akiongoze! Ningekuwa wewe ningejiuliza, je hii iliwezekanaje?
 
Labda wengine wameelewa, mimi sijaelewa ndiyo maana nikauliza ningekuwa nimeelewa nisingeuliza.

Kama hukuelewa uliweza vipi tambua nilichomjibu mpaka ukasaidia kumjibia kuwa alikua akijibu hoja?

Ulijuaje nadandia treni kwa mbele ikiwa hukuelewa?
 

Amin Yaah Raab Al Alameen.
 

Jee, Nyerere aliwahi kukaa nyumbani kwa akina Sykes?
 
Lusongo,
Kuchimbua kwa undani ni kweli.
Kitabu changu kimebadili kabisa historia ya uhuru wa Tanganyika.

Kuifuta historia ya Nyerere hilo haliwezekani kabisa.
Huwezi kufuta historia ni kazi kubwa sana.

Hili nalijua kwa kuwa nina uzoefunalo.
Historia ya wazee wangu ilifutwa kwa takriban nusu karne.

Leo tuko hapa tunaizungumza.

Ikiwa unaona kuwa kwa mimi kuandika habari za wazee wangu naamsha hisia
za udini hiyo ni bahati mbaya sana kwako.

Siwezi kuacha kuwarehemu wazee wangu.
Nikiacha historia hiyo mimi nitabakia na nini katika nchi hii?

Nitakuwa muflis.
 

average minds discuss events,small minds discuss people....nakushauri tu ubaki kuwa muimba mapambio ya kumshabikia mohamed said.
 
Naona umejongea tartibu kwenye darsa kufyonza ilm.
 
Kama hukuelewa uliweza vipi tambua nilichomjibu mpaka ukasaidia kumjibia kuwa alikua akijibu hoja?

Ulijuaje nadandia treni kwa mbele ikiwa hukuelewa?

Nilielewa maneno mengine yote ila hilo ambalo mpaka sasa sielewi maana yake na ndiyo maana sijaligusia katika majibu yangu. Unaona tabu kutuelewesha lina maana ipi hilo neno?
 

Mzee Mohammed niwie radhi kwa kuiita TAA kijiwe cha soga, nilikosa neno mbadala nikidhamiria 'social club'.

Lakini yote hiyo haiondoi ukweli kwamba TANU muasisi wake ni Mwl Nyerere aliyeibadilisha TAA kuwa chama cha siasa TANU, mpaka akatuletea uhuru.

Nafikiri sasa ni wakati wa kujibu hoja za Prof maana tumekuwa na subira lakini umeonekana ukikwepa au kama imeshindikana au umekosa majibu unakuwa muungwana tu ili si jambo la mashindano.

Naona vijana wako nao wameamua kurusha matusi na maneno ya kibaguzi mpaka kumuita Prof 'mshia' na kutuita wengine 'mapagani' waonye haya si maneno ya watu wenye adabu naimani ata watu wa umri wako walishayaacha pale Maggoti.
 
average minds discuss events,small minds discuss people....nakushauri tu ubaki kuwa muimba mapambio ya kumshabikia mohamed said.

Naomba nisaidie hili swali langu dogo; Mau Mau walipigana na Wajerumani?
 

Naomba nisaidie hili swali langu dogo; Mau Mau walipigana na Wajerumani?
 
Naomba nisaidie hili swali langu dogo; Mau Mau walipigana na Wajerumani?

kutokana na tonation ya swali lako,yaonekana jibu unalo kichwani.huna sababu kuomba jibu toka kwa mtu mwingine.
 


Nakupongeza Sana kwa aya na simulizi zako zaidi Sana ustaarabu ktk kujibu.

Ila nna deni moja tu nalo ni kutaka kujua malengo yako hasa ni yapi?

Unaleta bayana tusizoziana ktk vitabu rasmi vya historia nchini tutakuamini vipi?

Mbona hukufanya haya Nyerere akiwa yu hai tusikie yakwake naye?

Unajitahidi kujificha lakini ni dhahiri unapandikiza mbegu za udini kwa watu.
 
average minds discuss events,small minds discuss people....nakushauri tu ubaki kuwa muimba mapambio ya kumshabikia mohamed said.


Mkuu Mohamed Said anaweza kuwa na hoja but anajikanganya Sana na article zake zipo too illogical na hazina ushahidi Wa kina.
 

Mag3.

Naona umeibuka kutoka chimbo mstuni teh teh.

Kukata mzizi wa fitna tuambieni basi kwa mara ya kwanza ni mwaka gani Nyerere alifika Dar es Salaam?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…