Mzee wa Rula
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 8,169
- 3,359
Ninahisi Diamond kawatosa kuperform final maana muda wote anapondwa sana.
Mara anaambiwa kumbi za vichochoroni kama Dar Live aachiwe Diamond, kuna mshindani anaitwa Walter baada ya kuimba akaambiwa ana sauti nzuri sana na Diamond atasubiri sana.
Hii ikoje?
Top5 ni hawa hapa
1.Nshoma
2. Nsami
3. Wababa
4. Salma
5. Walter
Diamond kwa saizi ana maadui wengi kutokana na jinsi anavyo make headlines. Ukitoa hilo pia dau la Diamond lipo juu, nasikia mkwanja anaoutaka ni kati ya 5-10ml sasa sidhani kama walikuwa wanauwezo wa kumlipa na ilibaki ni kumkandia ili wamshushe toka huko dogo anakojiona yupo.
Diamond kwa saizi ana maadui wengi kutokana na jinsi anavyo make headlines. Ukitoa hilo pia dau la Diamond lipo juu, nasikia mkwanja anaoutaka ni kati ya 5-10ml sasa sidhani kama walikuwa wanauwezo wa kumlipa na ilibaki ni kumkandia ili wamshushe toka huko dogo anakojiona yupo.
katika wote Walter ndiye wa ukweli kuliko hata sifa anazobebeshwa Wababa. Walter anaimba ametulia na hata uchaguzi wa nyimbo zake ni kiboko lakini mtindo wa kupanga matokeo unawafanya wampigie upatu Wababa zaidi na ni katika mtindo huo huo Norman aliondolewa.
Pili Husna kaondoka lakini nakwambia alikuwa mzuri kuliko Nsami aliyeimba kizembe wimbo wa kuboa sana na matumizi yake ya steji ni zero. Husna pia alimpiga fimbo Salma (kipenzi chao anayeandaliwa kuchukuwa hiyo 50M). Ni kweli kabisa kuwa Huyu Salma ni mbovu hata Salama leo kamkataa. Ni binti anashindwa hata kutamka maneno yanavyotakiwa ana'kithembe' na anaimbia puani. Kila siku anajificha nyuma ya gitaa. Yaani akiambwia kuimba live hata top 20 hakustahili kabisa! Hamna noma mchagueni tu huyo binti wenu wa EPIC ili mgawane naye hizo 50.
Wababa ndiyo msanii ambaye naona anajitahidi kidogo.
Na wewe ushalogwa. Wababa anafanya nin? hana lolote nahis analoga ashinde manake mh!
Top5 ni hawa hapa
1.Nshoma
2. Nsami
3. Wababa
4. Salma
5. Walter
Wakitoka hapo waje sokoni...
Manake sokoni ndipo tunapotofautisha kati ya nywele na vuzi...
Wababa ndiyo msanii ambaye naona anajitahidi kidogo.
Kiongozi kumbe na wewe umo kwenye haya mambo?
Wamefeli kabla hata hawajaingia sokoni kabisa hawa washiriki!!!! Ni Peter Msechu angalau aliyefuruku baada ya kutoka BSS.
Tofauti na Bongo Star Search ya mwaka jana 2011, BBS ya mwaka huu naona imekosa mvuto tokea ilipoanza hadi hii leo inapokaribia kilele chake hapo tarehe 09. Nov pale katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Nikiangalia washiriki washiriki hawachangamshi na hakuna mashamushamu kama yale tuliyoyazoea mwaka jana na miaka iliyotangulia.
Bado sijaelewa ni ubovu wa washiriki wa mwaka huu au ni ubovu wa chaguzi za baadhi ya nyimbo zao ambazo zinashindwa kuonyesha vipaji vyao???
Nawasilisha kama mtazamo wangu ni wa wengi.